Huu ni mtindo unaojitokeza kutokana na style ya uongozi. Huenda ni maagizo ya Waziri Mkuu kwamba waende wakampokee maana ameshamfahamu ndivyo anavyopenda kupokewa. Na huenda ni yeye mwenyewe. Lakini huu ni mtindo wa kizamani sana na hauna tija kabisa haswa kwa nchi changa na isiyo na barabara zenye uwezo wa kuhudumia magari ipasavyo kwani mpaka hao wote wafike pale airport Dar ilisimama kwa muda.
Ingekuwa jambo la busara, na hapa ndipo utafahamu viongozi wachapa kazi wanavyojipanga, kama angeliwaita kuhudhuria Mkutano ili kuwapa briefing ya safari yake. Hilo lingekuwa ni ujenzi wa nchi, sasa huko airport sijui kunaongelewa nini na kinanukuliwa wapi? Na utekelezaji utakuwa lini? "common sense is not that common"