Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
JK apongezwa kutatua migogoro Afrika
na Mwandishi Wetu
NCHI tatu za Afrika zimetoa shukurani kwa Tanzania, hasa Rais Jakaya Kikwete, kwa mchango wake mkubwa katika kutatua migogoro ya kisiasa katika nchi hizo.
Shukurani hizo zilitolewa na Burundi, Comoro na Kenya wakati wa kikao cha 11 cha wakuu wa nchi za Afrika, kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika eneo la kitalii la Sharm El Sheikh, Sinai, Misri.
Nchi hizo zilieleza bila Tanzania na hasa bila kujihusisha moja kwa moja kwa Rais Kikwete katika migogoro ya nchi hiyo, ingezichukua nchi hizo muda mrefu zaidi kwa migogoro hiyo kuweza kutatuliwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), ilieleza shukurani hizo zilitolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika walipokuwa wanajadili hoja ya kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Afrika - moja ya ajenda kuu za kikao hicho.
Makamu wa Rais wa Burundi, Yves Sahinguvu, aliuambia mkutano huo: Sisi wa Burundi tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa juhudi zake za miaka mingi kuweza kusuluhisha mgogoro katika Burundi, ambao umefikia mwisho kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa chama cha FNL-Palipehutu wanarejea nyumbani karibuni.
Tanzania, na hasa Rais Kikwete, tangu alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, imehangaika na mgogoro wa Burundi kuliko nchi nyingine yoyote. Tunawashukuru sana Watanzania kwa mchango wao wa kindugu, alikaririwa makamu huyo wa Rais.
Naye Rais Sambi wa Comoro alitoa shukurani kwa jumuiya ya kimataifa, na hasa kwa Rais Kikwete na viongozi wa Sudan na Libya, kwa kuweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani humo, uliosababishwa na uasi wa Kanali Mohammed Bacar katika Kisiwa cha Anjouan.
Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alitoa shukurani kwa Rais Kikwete, katibu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dk, Kofi Annan; Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Umoja wa Afrika (AU) na Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuchangia katika usuluhishi wa mgogoro wa Kenya mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
source Tanzaniadaima