JK apongezwa kutatua migogoro Afrika

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
JK apongezwa kutatua migogoro Afrika

na Mwandishi Wetu

NCHI tatu za Afrika zimetoa shukurani kwa Tanzania, hasa Rais Jakaya Kikwete, kwa mchango wake mkubwa katika kutatua migogoro ya kisiasa katika nchi hizo.

Shukurani hizo zilitolewa na Burundi, Comoro na Kenya wakati wa kikao cha 11 cha wakuu wa nchi za Afrika, kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika eneo la kitalii la Sharm El Sheikh, Sinai, Misri.

Nchi hizo zilieleza bila Tanzania na hasa bila kujihusisha moja kwa moja kwa Rais Kikwete katika migogoro ya nchi hiyo, ingezichukua nchi hizo muda mrefu zaidi kwa migogoro hiyo kuweza kutatuliwa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), ilieleza shukurani hizo zilitolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika walipokuwa wanajadili hoja ya kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Afrika - moja ya ajenda kuu za kikao hicho.

Makamu wa Rais wa Burundi, Yves Sahinguvu, aliuambia mkutano huo: “Sisi wa Burundi tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa juhudi zake za miaka mingi kuweza kusuluhisha mgogoro katika Burundi, ambao umefikia mwisho kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa chama cha FNL-Palipehutu wanarejea nyumbani karibuni.

“Tanzania, na hasa Rais Kikwete, tangu alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, imehangaika na mgogoro wa Burundi kuliko nchi nyingine yoyote. Tunawashukuru sana Watanzania kwa mchango wao wa kindugu,” alikaririwa makamu huyo wa Rais.

Naye Rais Sambi wa Comoro alitoa shukurani kwa jumuiya ya kimataifa, na hasa kwa Rais Kikwete na viongozi wa Sudan na Libya, kwa kuweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani humo, uliosababishwa na uasi wa Kanali Mohammed Bacar katika Kisiwa cha Anjouan.

Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alitoa shukurani kwa Rais Kikwete, katibu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dk, Kofi Annan; Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Umoja wa Afrika (AU) na Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuchangia katika usuluhishi wa mgogoro wa Kenya mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

source Tanzaniadaima
 
Anahangaika na migogoro ya nchi zingine huku akiacha nyumbani kwake moto ukiwaka. Aaanze na ufisadi na mgogoro wa zanzibar akimaliza ndio aende nchi zingine.

Aibu tupu kwa Kikwete.
 
Kwanini Credit tunayostahili watanzania anapewa Kikwete? Hizo pongezi zilistahili kwenda kwa Tanzania na sio kwa raisi wa Tanzania,au kwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania. Hizo initiatives ni za watanzania na sio za mtu mmoja mmoja. Migogoro kama ya burundi ilianza kutatuliwa na Mwalimu Nyeyere foundation, ikaendelezwa na Mandela na ikaendelea na kuendelea why someone else should take this credit?? Hata JK mwenyewe sidhani kama anafurahia vilemba vya ukoka!
 
...nafikiri angetatua na hili la zanzibar angestahili hizo pongezi kinyume cha hapo....Bado zero tu!!
 
Ya kwao lakini kimya ETI kura ya maoni? huko alikoweza palikuwepo na kura ya maoni?. Mtu mzima .......
 
Nadhani JK anataka kujifariji na utatuzi wa migogoro ya wenzake ili aonekane kwake kuko shwari kumbe hola!!!!Nyumba yake inafuka moshi siku itakapolipuka nadhani hata hao wanaompongeza itabidi watuombe radhi....Hivi kweli hawajui kinachoendelea katika kibanda cha muungwana kweli????
 
Anantatua migogoro ipi?kwake yamemshinda ya wengine atayaweza?angeshughulikia ya nyumbani basi hata humu JF tungemtumia pongezi.
 
Viongozi wetu wa Africa wengi ni matatizo tu kwao lakini wakikutana kila mmoja anajifanya kwamba yeye ndiye wamo.
Kikwete hastahili sifa yoyote, na wale wanaomsifia ni kwamba hawajui tu kwamba na yeye ana matatizo lukuki hapa Bongo.
Hata hivyo tutabanana hapa hapa tu na mipesa yetu irudi.
 
Vibaraka wa MKOLINI NDIO WANAPEANA PONGEZI na kamwe si hatua ya AFRIKA!
Huto tunchi tuchache twenye kashfa za UFISADI kama KENYA,BURUNDI,COMMORO,UGANDA NK... KASHFA ambazo wamejitakia baada ya kuuza uhuru wetu mwafrika na kuanguka saini ambazo zimetugeuza watumwa na wakipanua mdomo tu na kuwapinga mabwana zao waliofunga nao ndoa basi wana hatari na wanatolewa madarakani na mabwana zao hao!

WANANCHI MKITAKA UHURU MUWAONDOWE HAO MADARAKANI NA MSISUBIRI MTU MWINGINE YEYOTE ZAIDI YENU KUWAONDOA MAFISADI MADARAKANI NA KUWAFIKISHA KUNAKO MKONO WA SHERIA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom