Rais wetu JK yupo busy sana na mambo ya nje kuliko ya nyumbani......hapa nyumbani hatulii kabisa ndo maana mafisadi wanapumua na kujiimarisha zaidi na zaidi......kwa kupaa paa hivi sijui kama hawa mafisadi atawaweza wengine anapaa nao huko huko anako elekea.
Whats new here? hizi ni routine za kawaida za rais mna sensationalize mambo tu...
kwa wale msioelewa tafteni taarifa Raisi wa Botswana anasafiri mara ngapi kwa mwaka! Halafu linganisheni maendeleo ya Botswana na ya kwetu! Na mipango yao Baada ya Miaka 10 ijayo wanataka kufanya nini!
Kiufupi ni kuwa hatuna raisi! ivi unataka kuniambia atasoma lini report alizopewa?
Ripoti anazisoma akiwa safarini..kwani huko anapata muda mwingi wa kuzipitia...Safari si Mbaya kama anapata muda wa kujifunza mazuri walionayo wenzetu....Hata vasco Dagama hakuwa akitembea tu for leisure...Kama JK na Timu yake safari zao haziwasaidii kujifunza mazuri....hapo tena utakuwa mushkeli mkubwa!!!.... ivi unataka kuniambia atasoma lini report alizopewa?
Siyo lazma Rais wa nchi aitikie mwaliko wo wote anaweza akatuma viongozi wengine.Ya ndani yanamshinda ndiyo maana anona apoteze mawazo huko nje.
he! kunani tena?
Ukiwa na issue huna sababu ya kusafiri, wenyewe watakufuata. Angalia wanavyopigana vikumbo hapo Tripoli kwa mzee Muamar, ingawa walimuita gaidi na kumsakizia ushenzi mwingi tu, lakini leo hii hawaishi kwenda kwake.
Halafu anarudi tena US, after all this!
sioni ubaya JK kwenda Swaziland
Nchi inaendelea vizuri tuuu
Baada ya siku mbili kurejea kutoka kwenye mazishi ya Levy Mwanawasa......Rais wetu JK amepaa tena jana jioni kwa ndege ya serikali kwenda kwa Mfalme Mswati-Swaziland kuhudhulia sherehe za uhuru wa nchi hiyo pamoja na Birthday ya mfalme huyo ambaye anatimiza miaka 40 wao wanaita ni 40-40.Ambazo zitaligharimu taifa hilo $40 milion
Imethibitishwa kuwa akitoka huko anaunga moja kwa moja kwenye mkutano wa nchi za Afrika ...................
Halafu anarudi tena US, after all this!
Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilipata nafasi ya kuwa mmoja wa watanzania tuliokutanishwa na balozi Ombeni Sefue, balozi wetu hapa Marekani katika kikao cha kuratibu uanzishwaji wa Diaspora Association of Tanzanians Abroad (DATA), kikao kilichofanyika Hilton Americas Hotel, Houston, Texas. Habari zaidi ya nini kitaendelea baada ya pale zitatolewa baadaye. Tulipata input nzuri tu toka kwa Bw. Ole Naiko (TIC), Bw. Dunstan Mrutu (Baraza la Biashara), Bw. Elvis Musiba (chamber of commerce), among others ... kamati maalum iliundwa ili kuratibu mambo ya chama hiki.
Anyways, nilichotaka kusema ni kwamba kitaitishwa kikao cha watanzania wote waishio Marekani siku ya uzinduzi wa hiki "chama", na Rais ndiye anategemewa kukizindua, hivyo atakuja Marekani, sijui itakuwa wapi exactly, ila itakuwa sometime in Novemba.