JK analipiza Kisasi kwa Watanzania?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Jamani mie nashindwa kuelewa hivi kwa hali ngumu ya maisha na ufisadi huu uliokithiri nashindwa kumuelewa Rais wetu JK au ndio analipiza kisasi kwa sie kutompigia kura maana kihalali aliambulia less than 40% wakati Dr. Slaa alipata more than 60%???

Na ndio kwanza mwaka wa kwanza wa awamu yake ya pili je wakati anamaliza muda wa miaka mitano sijui hali zetu zitakuwaje?
 
Eeeee huyu mtu haeleweki kabisaa alishashindwa toka siku nyingi sana basi tu.
 
Ni mapito ya maisha tu. Ipo siku tutayasahau yote haya. Tukaze buti kubuni njia halali za kuingizia kipato familia zetu na maisha yatasawazika.
 
Sidhani kama analipa kisasi, ni mipango tu imemshinda ya kuweka maisha ya Watanzania kwenye mstari.
 
Hana haja ya kufanya lolote tena, awamu ya kwanza at least kulikuwa na presure ya re-election inamsukuma. Sasa hivi anaweza kutulia tu na kupiga trip zake za nje, nothing to lose.
 
aliingia ikulu bila agenda ya namna ya kuboresha maisha bora kwa kila mtanzania-alivyo dai!! ukimuuliza hata leo kwa namna gani maisha yaweza kuwa bora???-hana jibu-maana hajui kwa nini wa tz ni maskini.
 
Ila kwa kasi hii ya kutuchosha na kutunyong'onyeza CCM watapata taabu sana 2015

Kwani hata hilo yeye analikumbuka?? Tuvumilie tu wandugu, cha moto tutakiona miaka hii mitano!!
 
Jamani mie nashindwa kuelewa hivi kwa hali ngumu ya maisha na ufisadi huu uliokithiri nashindwa kumuelewa Rais wetu JK au ndio analipiza kisasi kwa sie kutompigia kura maana kihalali aliambulia less than 40% wakati Dr. Slaa alipata more than 60%???

Na ndio kwanza mwaka wa kwanza wa awamu yake ya pili je wakati anamaliza muda wa miaka mitano sijui hali zetu zitakuwaje?

Ugumu wa maisha hauletwi na JK, una-sababishwa na mambo mengi sana, moja kutokujituma. Kuhusu ufisadi, nadhani JK ndie aliefichuwa mafisadi na kuwashughulikia kuliko awamu yeyote ile kuanzia kwa Nyerere.
 
We! acha fix aliyefichua ufisadi ni dr slaa, alithubutu kuwataja majina hadharani akiwemo jk mwenyewe. Sidanganyiiiiiiki!
 
Mbona avatar yako hainyeshi kama unashida katika maisha yako?[, au ndio husi-judge kitabu kwa cover lake!!
 
Jamani mie nashindwa kuelewa hivi kwa hali ngumu ya maisha na ufisadi huu uliokithiri nashindwa kumuelewa Rais wetu JK au ndio analipiza kisasi kwa sie kutompigia kura maana kihalali aliambulia less than 40% wakati Dr. Slaa alipata more than 60%???

Na ndio kwanza mwaka wa kwanza wa awamu yake ya pili je wakati anamaliza muda wa miaka mitano sijui hali zetu zitakuwaje?[/QUOTE]

Hata maliza muda wake kwasababu watanzania hatuwezi kumvumilia kwa haya maisha magumu ya sasa hata CCM yake imemchoka. Alizoea mambo ya zamani ya ndiyo mzee na akadhani atauweza urais sasa anachemsha mbaya!!
 
Ugumu wa maisha hauletwi na JK, una-sababishwa na mambo mengi sana, moja kutokujituma. Kuhusu ufisadi, nadhani JK ndie aliefichuwa mafisadi na kuwashughulikia kuliko awamu yeyote ile kuanzia kwa Nyerere.

inaelekea humjui Nyerere ni bora usimtolee mfano kama kilaza wenu J.k anajitolea mfano..Matatizo hayata isha alikuwepo Mzee Nyerere pambafu sema Baba wa Taifa. watu walikuwa wanaitwa mahujumu uchumi (Mafisadi Sikuhizi) Wajua Kulikuwa na FAGIO LA CHUMA au wewe ni dogo samahani kwa hayo uzila kwanza, hujui ati jk kafichua ufisadi oi oi oi wakati katika watu list ya mafisadi wa kwanza yeye ni mmoja wa mafisadi
 
Jamani mie nashindwa kuelewa hivi kwa hali ngumu ya maisha na ufisadi huu uliokithiri nashindwa kumuelewa Rais wetu JK au ndio analipiza kisasi kwa sie kutompigia kura maana kihalali aliambulia less than 40% wakati Dr. Slaa alipata more than 60%???

Na ndio kwanza mwaka wa kwanza wa awamu yake ya pili je wakati anamaliza muda wa miaka mitano sijui hali zetu zitakuwaje?

Mambo yamemshinda! Sidhani kama ana uwezo wa kieledi wa kupanga ugumu kama huu kwa maksudi. Wakati anamfuata RA kupata ufadhili hakujua kama jinamizi na Muajemi huyo lingemwandama for lifetime. Unaambiwa jamaa alikomba 40 bil. kupitia Kagoda chama kikaambulia 10 bil peke yake na akiwa Mweka hazina akatia ndani alizoweza katika hiyo 10bil. Kichaa ananyonya lakini haridhiki (RA huyo).
Sasa jaribu kutafakari mtu asiyeridhika kama RA anapokuweka madarakani wakati bado anataka kupora nchi! Unadhani utapata nafasi ya kuwatumikia raia wako kweli? Kwanza kwa kuchanganyikiwa itabidi utumie hata hicho kidogo kilichopo kusafiri nje kupata japo faraja ya watu wa huko.
 
Back
Top Bottom