JK anaenda Hijja Suudia mwaka huu 2012

Kwa jina la Allah (SW) Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo. Kuna taarifa kuwa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete akijaaliwa uzima na Uhai Inshallah atajumuika na mahujaji wengine waliotangulia kula Suudia (Saudi Arabia).

Sasa sina hakika kama habari hizi zina ukweli lakini kama waaminivyo waislam kuwa Hijja ni mpaka uitwe ndio maana utakuta majajiri na marais wengi tuu waislam lakini hawajawahi kwenda hijja.

Mimi namuomba Allah amjaalie safari njema, na pia ingependeza zaidi akawachukua na wanae na hususana yule Ritz maana mahasidi wamemzunguka na mitihani ya kila namna na kila kukicha.

Hili ni jambo la kheri na nawatakia safari njema na Allah awafanyie wepesi kwenye mambo yao yoote.

Amin.

wenye wivu na majungu wajinyonge,
 
AKIONDOKA TU TUNAPINDUA NCHI..... Huu ni upuuzi hajawahi kukaa hata mwezi nyumbani kila siku safari
 
Haya mnaanza tena mabishano yale yale ya 'kujolea Kurani'!!!! Visasili vya imani za Kiislamu vitakuja kusababisha watu kutoana ng'eo.

Mtu apotoshe ukweli alafu atizamwe? Eti "nijuavyo" hajui na hajui kama hajui mpaka ajulishwe kama hajui
 
Hapo vyeo vingine itabidi uviweke baada ya neno Kikwete....

AL HAJJ ni Moja
DR. GENERALI - Ni Moja- Kwasababu atakuwa ni Dr Generali Pekee Duniani
Ph.d Hon President - ni Moja - Kwasababu ni Rais kuliko marais wengine - Ph.d Hon President

Mwisho ESQ...
 
huko inatakiwa uende na hela yako halali
na inayobaki home iwe hela halali, angalieni tusije mkosa mtu wakati wa kutupa mawe.
 
Anataka title iongezeke, kama kweli ameitwa kwenda hijja kheri na iwe kwake

Hijja sio ya kuchezea; kwa madudu anayoyafanya huku bongo na wakina Subash Patel anaweza akaenda halafu asirudi!! Mshaurini asiende asije akafia huko!!
 
Hapa kama unafki unahusika


[h=1]Mashambulizi ya kuogofya Nigeria[/h]
16 Oktoba, 2012 - Saa 10:20 GMT



120501184938_maiduguri_304x171_bbc_nocredit.jpg
Waathiriwa wa mapigano mjini Maiduguri


Milipuko ya sauti ya juu pamoja na milio ya risasi ilisikika leo mjini Maiduguri, Kaskazini mwa Nigeria, mji ambao umeshuhudia ghasia na vurugu zinazosababishwa na kundi haramu la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Taarifa kuhusu mashambulizi hayo bado hazijatolewa , lakini inaarifiwa angalau watu kumi wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom