JK ampongeza Rais Samia maandalizi uzinduzi programu ya uwekezaji sekta ya maji Tanzania 2024-2030

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
JK AMPONGEZA RAIS SAMIA MAANDALIZI UZINDUZI PROGRAMU YA UWEKEZAJI SEKTA YA MAJI TANZANIA 2024-2030

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA) na Mwenyekiti Mwenza Mbadala (Alternative Co-Chair) wa Continental Africa Water Investment Programme High-Level Panel amempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kwa kukamilisha na kuanza maandalizi ya uzinduzi wa Program ya Uwekezaji Katika Sekta ya Maji Tanzania.

Akizungumza na viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji Mhe. Kikwete ameelezea furaha yake kwa Tanzania kupitia Wizara ya Maji kuandaa Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji Tanzania (Tanzania Water Investment Programme) katika kipindi cha mwaka 2024-2030.

Programu hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 15 inahusisha Sekta za Maji, Nishati, Mazingira, Afya, Uvuvi, Kilimo, Madini, Mifugo, Utalii, Mali Asili na Viwanda miongoni mwa Sekta nyingine.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumzia suala hili amesema Madhumuni ya Programu hiyo ni kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na usalama wa maji na uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame na mafuriko ili kuwezesha upatikanaji wa maji ya kutosha na yenye ubora kwa ajili ya matumizi ya watu, shughuli za uchumi na mazingira.

Programu hiyo yenye maeneo manne ya maji na jamii; maji na uchumizi; maji na mabadiliko ya tabianchi; na usimamizi na uongozi katika maji itaongeza msukumo katika ujenzi wa miradi mikubwa ya maji yakiwemo mabwawa kwa ajili ya mifugo na kilimo miongoni mwa matumizi mengine.

Programu hiyo ambayo ni agenda ya Umoja wa Afrika ina wadau mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa wakiwemo Mashirika ya UNDP, UNICEF, GWP na Global Centre for Adaptation na inaratibiwa na Taasisi ya GWPSA.
 

Attachments

  • IMG-20230627-WA0059.jpg
    IMG-20230627-WA0059.jpg
    76.9 KB · Views: 3
  • IMG-20230627-WA0063.jpg
    IMG-20230627-WA0063.jpg
    101.3 KB · Views: 4
  • IMG-20230627-WA0062.jpg
    IMG-20230627-WA0062.jpg
    108 KB · Views: 3
  • IMG-20230627-WA0064.jpg
    IMG-20230627-WA0064.jpg
    59.7 KB · Views: 3
  • IMG-20230627-WA0061.jpg
    IMG-20230627-WA0061.jpg
    99 KB · Views: 3
  • IMG-20230627-WA0060.jpg
    IMG-20230627-WA0060.jpg
    66 KB · Views: 2
Huo ni Uongo na ndugu yake Utapeli wa kisiasa. Huo upendo kwa Wananchi hawana.
 
Back
Top Bottom