JK ampa pole Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ampa pole Dr Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Halisi, Aug 1, 2010.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS[/FONT]
  [FONT=&quot]UNITED REPUBLIC OF TANZANIA[/FONT]

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.  [FONT=&quot]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]

  [FONT=&quot]Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Julai 31, 2010, amemtumia salamu za pole Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mheshimiwa Wilbroad Slaa, kufuatia habari kuwa kiongozi huyo amevunjika mkono.[/FONT]

  [FONT=&quot]Aidha, Rais Kikwete amemtakia Mheshimiwa Slaa aweze kupona haraka na kupata nafuu ya kuendelea na shughuli zake za kila siku katika kutumikia umma wa Watanzania.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika salamu hizo, Mheshimiwa Rais amemwambia Mheshimiwa Slaa: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuumia kwako kwa kuvunjika mkono. Kwa dhati ya moyo wangu, nakutumia salamu nyingi za pole na kukuhakikishia kuwa niko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu cha maumivu.”[/FONT]

  [FONT=&quot]Ameongeza Mheshimiwa Rais: “Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe uwezo wa kupona haraka ili uweze kurejea katika shughuli zako za kutumikia umma wa Watanzania.”[/FONT]

  [FONT=&quot]Imetolewa na:[/FONT]

  [FONT=&quot]Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,[/FONT]
  [FONT=&quot]Ikulu,[/FONT]
  [FONT=&quot]DAR ES SALAAM[/FONT][FONT=&quot].[/FONT]

  [FONT=&quot]31 Julai, 2009[/FONT]
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Namshukuru sana JK kwa kulitambua hili,ni uungwana na kukomaa kisiasa,ingawa kama rais wetu,ni kitu ambacho alitakiwa kufanya....Makamba angekua rais,angechuna tu.....teh teh
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Classic,

  Ingawa wengine tutasema kipapai kilitoka Bwagamoyo na hii inaweza kuwa ni kujikosha tu. (kidding, you know I don't put any stock in that stuff)
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Bila kujalali whether he was sincerely or not, ni jambo zuri amelifanya Rais.
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kikwete huwa yupo sincere. Jamaa ni muungwana saana na submissive hata Dr Slaa anafaham.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sasa hii ni barua ya copy and paste au ni templete linalotumika kuedit baadhi ya vitu tu, hiyo tarehe imeniacha hoi au ndio hivyo umakini wetu pale mjengoni ni zero?

  anyway kama ni ya kweli basi kikwete kajitahidi kuwa muungwana, nadhani asiishie hapo bali awape pia jamaa wa TBC waraka wa kuwaambia wawe neutral katiak mchakato huu wa uchaguzi
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ameonyesha uungwana mkubwa sana katika hili. Though JK ni so creative katika suala zima la namna ya kuwateka wananchi. Hapa keshoongeza credit kadhaa kisiasa.
   
 8. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya tarehe kali. Back-dated a year ago.

  Lakini ni uungwana kutoa pole, walau wakati jua linawaka.
   
 9. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kama kuna mtu ana barua rasmi kama hii kutoka kwa raisi ya kuwapa pole wale wananchi walio pata ajali kwenye hile ajali iliochukua maisha ya watu 18 waiweke hapa ndani hili inibadilishe mawazo ya kwamba hii pole ni ya kisiasa zaidi wakati huu wa uchaguzi.


  Si maanishi kwamba ni kosa kutoa pole lakini sidhani kama ilitakiwa hiwe "taarifa kwa vyombo vya habari" huko huko walipofanya ingetosha na waandishi wa habari wangeweza kujua kwa kumuuliza swali la jambo hilo Dr.Slaa, kwa kutaka kuwapunguza wananchi hasira zao wakati huu tunaelekea uchaguzi wakaona bora wawape taarifa waandishi wa habari kwamba "nimempa pole mpinzani wangu kaumia mkono" kwani itawafikia wananchi.


  Nita badilisha mawazo yangu kama kulikuwa na taarifa rasmi kwa waandishi wa habari kama hii kutoka ikulu kuhusu hile ajali ilichokua maisha ya watanzania 18.
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo, hii sio barua ya hivi karibuni, ilishatolewa zamani (31 Julai 2009) kwa hiyo imepitwa na wakati. Kama asemavyo Wenger, ni vyema angewapa pole hawa waliopata ajali juzi kwenye basi.
   
 11. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  umakini wa watu wa Kurugenzi ya Ikulu unatia shaka sasa hapa ni kutafuta kuwapa habari watu wa magazeti hiyo Jumatatu! Mweeh Mungu anajua!
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda walijua tangu wakati huo kuwa itatokea ajali wakaiandaa kabisa... lol...
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ofcourse JK masuala kama haya ya kutoa pole ndiyo kwake haswaaa lakini siyo uongozi!!!!!!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mmmmmh hapo walijua kuwa jamaa atavunjika mkono??
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huko ikulu kuna watu wenye akili timamu kweli?makosa ya kijinga kabisa haya...Huyu rweyemamu anafanya kazi gani pale?????shame
   
 16. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi nimeshangaa sana, kweli mtu anakosea tarehe akitegemea sisi tujue hiyo pole imetoka kweli, mbona hilo kosa ni technical, hvii mtu ataminije kuwa hiyo pole ni ya kweli? hapa siwezi hata kukomenti kuwa raisi amekuwa sincere, make tarehe haiendani na tukio halisi, labda kama kuna mtu ameiedit.
   
 17. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ila huko Mwanza kuna mambo mengi haswa kwa wanasiasa! Hata JK mwenyewe alishaonja jito ya jiwe huko kama sijakosea ni mara mbili hivi!! Dr Slaa asingekuwa mkristo mwadilifu ningemshauri aende huko Bagamoyo kwa wataalam wakamweke sawa!!
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haijasainiwa ni draft tu iliyochomolewa kwa secretary kwa mtindo wa copy and paste, si unajua uvivu wa watu wa pale ofisini? Mambo mengine JK asilaumiwe, Chief Administrative officer ndiye mwenye dhamana ya kuangalia haajiri mambumbumbu, kwani hiyo ilikuwa barua ndefu kiasi cha kushindwa kuichapa? Kama ingesainiwa au angalau paandikwe "signed by...." ningedanganyika kwamba wakubwa wa secretary nao wameiona. Kukosea secretary sio jambo la ajabu hata hivyo, lakini kila tupatapo kitu kutoka Ikulu kina utata, ina maana reflection ya ajira za kiundugu na sio kitaaluma. Shame on you! Bora yule polisi aliamua kujikosoa kwa risasi Tarime kuliko wachapiaji wa Ikulu nenda rudi kutwa kuchwa. Mtakuwa waungwana mkikitoa mnamchafua mno Raisi wetu. Au mmumzoea sana kwa tabasamu lake na upole? Ndio maana mnamkalia kichwani anapata matusi yasiyokuwa yake.
   
 19. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kilemi
  dah! umenifanya nicheke mwenyewe
  Yaani umekuwa convinced kwamba nguvu za giza zaweza kuhusika kumwangusha Dr. Slaa huko Mz.
   
Loading...