Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,506
- Thread starter
- #21
Hii nchi ni ya kipumbavu sana.
Ili udumu katika ajira sharti uwe mjinga kama wao.
Hii nchi ni ya kipumbavu sana.
kaazi kweli kweli, kutoka katibu mkuu wizara mpk katibu tawala wa mkoa
Bi Zipora Liana ambaye amekuwa katika mgogoro wa mara kwa mara na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo na meya wa jiji pia la Arusha sasa amehamishiwa ofisi ya waziri mkuu Tamisemi akiondolewa jijini Arusha kuanzia leo. Juma Idd aliekuwa mkurugenzi jiji la Mbeya amehamishiwa kuchukua nafazi ya Zipora hapo Arusha.
Katibu mkuu uchukuzi bwana Omary Chambo ameshushwa cheo na sasa atakuwa katibu tawala mkoa wa Manyara kuanzia leo.
Dr John ndunguru aliekuwa naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi nae amesgushwa cheo na kupelekwa Kigoma kuwa katibu tawala wa mkoa huo.
Uamuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue usiku huu.
Leo Mulongo atakesha bar kusherehekea ushindiDuh jembe limetoka
Huyu mama wengi hawamjui vema. Nitakuja kuwapeni siri zake siku muafaka
Hii ni dangaya toto! Uhamisho huu lazima unaharufu/msukumo na Uchaguzi ujao wa madiwani .
Hizi ni habari za kusikitisha sana............ Sipora Liana ni zaidi ya mtumishi wa wananchi
Kama ni kweli, hakika tuna kazi. Yote haya ni mulongo kwa maslahi ya mkubwa. Yana mwisho!!!
Meya bandia mkuu wa mkoa mlinzi wa mafisadi. Wakati mwanri anakataa kufungua miradi ya kifisadi huyo meya aliwahi kuonekana kwenye tv akifungua caravat monduli eti ni daraja la milioni 60.nilimsikia akiojiwa na kibonde juzi kuhusu kumzalau meya. Pole mama wengi wape
huyu mama anapaswa kuwa waziri ni mtendaji mzuri sana lakini kwa kuwa serikali ni ya kichupi ndiyo maana kaondolewa Arusha..
Huyu mama wengi hawamjui vema. Nitakuja kuwapeni siri zake siku muafaka