JK aikokota Tanzania Mnadani-G8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aikokota Tanzania Mnadani-G8

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, May 18, 2012.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa amka na BBC leo asubuhi, Katika mkutano wa G8 unaofanyika huko Camp David Marekani Rais Obama amewakaribisha wageni maalum ambao ni marais wanne kutoka nchi 4 za Afrika akiwemo Jakaya Mrisho Kikwete wa TZ. wengine ni Rais wa Ghana, Rais wa Ethiopia na Benin.

  Why Rais wa Tanzania na si mwingine wa East Afrika aalikwe katika mkutano wa nchi 8 tajiri kuliko zote duniani ili hali nchi yetu iko maeneo ya mkia kwa umaskini wa kipato?

  According to BBC ni kwamba JK ame qualify kuhudhuria mkutano huo kutokana na nchi yetu kuongoza katika KUUZA ARDHI yetu kwa WAWEKEZAJI WA KIGENI na si sababu nyingine. Hayo ni maneno ya mchambuzi wa BBC na si ya kwangu" Kama ukweli wenyewe ndio huo basi wamemwita ili kumpongeza , kumtia moyo kwa juhudi zake za kuuza nchi na pia kumwomba maeneo zaidi. HII IMENISHTUA sana kama mtanzania mpenda nchi yangu na nimejiuliza maswali mengi sana likiwamo la kuhusu future ya watoto wetu.

  Inakuwajei Rais bila aibu wala woga anathubutu kuuipeleka nchi kwenye mnada wa matajiri bila wenye nchi kuhusishwa?

  Kwa hiyo tutarajie wananchi kuhamishwa kwa kigezo cha uwekezaji. Je makosa waliyofanya Kenya miaka 1964 ya land alienation bado hayakuwa soma kwetu na matokeo yake tunayarudia karne hii?."THIS TIME TOMORROW" ni kitabu alichoandika Ngungi wa Thiong'o kuelezea jinsi ardhi ilivyoporwa na wazungu na kuwaacha wenye ardhi wakihaha na kuishia mtaa wa mabanda. Leo rais wa TZ kana kwamba hajasoma historia au hana mtazamo wa baadaye anarudia yaleyale tena kipindi hiki sio wakaloni wanakuja kupora ardhi bali anawapelekea huko huko mnadani kwao. HALI HII INATIA SHAKA SANA KUHUSU DHAMIRA ZA VIONGOZI WETU KWA MUSTAKABALI WA NCHI NA KIZAZI KIJACHO CHA WA TANZANIA.
  Muda umefika kwa Watanzania kukataa kuitwa nchi inayoongoza kwa kuuza ardhi kwa wageni kwani hii sifa ni mbaya sawa na Kuitwa MAMA HURUMA.
  SWALI NINALOJIULIZA JE HAKUNA NJIA NYINGINE YA KULETA MAENDELEO BILA KUUZA NCHI? Nataka niamini kwamba Ubinafsi na Uvivu wa kufikiri ndo unatufikisha tusikokutaka.
   
 2. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Guys Ethiopia inatisha....ina uchumi unaokua karibu kwenye maeneo yote. Ubinafsishaji umetekelezwa kwa uangalifu mkubwa ili kuepusha wahindi kugeuza viwanda nyeti kabisa kuwa magodown yao.
  Tanzania tunaenda kuuza sura...au kutafuta "mabwana" wa kuwekeza maana hatujiwezi...tunalia misaada na njaa na vitu vinavyofanana na hivyo
   
 3. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo watanzania tumekuwa wapole kupitiliza,hivi sasa wananchi wengi wanahamishwa vijijini
  kwa kisingizizo cha uwekezaji,wanateseka na hakuna mtu wa kuwatetea,na hiyo inafanywa kwa
  maslahi ya wachache kufaidika wao na familia zao."Mungu tusaidie Watanzania na Tanzania yetu"
   
 4. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ebu mwenye hiyo clip/youtube atuwekee tuchanganyikiwe kwa pamoja.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ah,,,ikipatikana wataiweka,ila binafsi niliishia kuguna tu,,,,yule mchambuz amejibu vizur maswali ya mtangazaj wazir HAMSINI,ametamka waz kwamba j.k ana uswahiba wa karibu sana na bwana obama,na obama anampenda sana j.k kuliko kibaki,ila akasema kuwa huwenda kwa sababu ya ugawaji wa ardhi kiholela,,,,,,kwa wagen
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunayoyaona ni manyunyu tusubiri Elnino kwani kama hadi leo kuna Rais asiyetambua hila za wazungu na badala yake kuwaona watu wema basi tumepata hasara.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Madai ni kuwa hii nchi ina hekta mil 2 za kilimo wakati zinazotumika ni laki 2 tu, so watakuja sana tupende tusipende. Labda tuharakishe kubadili mfumo
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Aisee!!!!!:angry:
   
 9. m

  mayere Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kIKWETE KAAMUA KUKOMOA COZ ANAJUA ANAMALIZA MDA WAKE WA UONGOZI ..... ILA IKO SIKU MAMBO YATAWATOKEA PUANI
   
 10. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  EPZ na MRADI WA KIGAMBONI, hivi ni kweli Kigamboni imeuzwa kwa wamarekani ?
   
Loading...