JK agawa mifugo kwa waathirika wa ukame

tembeleh2

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
765
165
Kwa mujibu wa blog ya mpiga picha na rafiki wa JK (MICHUZI), serikali imegawa jumla ya ng'ombe 25,000 na mbuzi 15,000 kwa wafugaji waliopoteza mifugo yao katika wilaya za Longido, Ngorongoro, na Monduli. Huu ameuita mradi kabambe wa uwezeshaji wa mifugo. Ngugu JK ameonekana akigawa mifugo hiyo. Sasa wana JF, kwa waliowahi kufika/kutembelea wilaya zile, hali ya mazingira ni ile ile na wafugaji karibia wote wamehama kwenda kutafuta malisho, kwa hiyo ninavyofikiri mimi na ng'ombe hawa watakufa. Hizi siasa zinatufanya tufanye mabo bila kufikiri sawa sawa. Ng'ombe hawa wamegawiwa ili wafuge kwa mtindo uleule wa kwenda kutafuta majani (kuchunga). nilitegemea wataalam wa ndugu JK wangewafundisha watu hawa utaratibu mwingine wa kufuga.
 
Back
Top Bottom