Mwaya J
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 238
- 82
Jana ilibidi nisubiri hotuba ya mwisho wa mwaezi na mwaka toka kwa Rais.Hamasa yangu kubwa ilikuwa nisikie serikali inatoa tamko gani juu kadhia inayoendelea kule kusini hasa Mtwara juu ya kusafirisha gesi kwenda Dar.Kwa werevu waliofuatilia sakata hili siku ile ya maandamano pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na wataalam na wasomi tofauti(mfn.Zitto,Prof.Lipumba) na wananchi kwa ujumla,utaona jinsi rais Kikwete anavyokwepa kujibu hoja za Wanamtwara.
Wanamtwara wanagomea kusafirishwa gesi kwenda Dar wakihoji mantiki ya kufanya hivyo ni ipi? Kwa nini vinu vya kuzalisha umeme toka kwa gesi hiyo visijegwe kule ili kuwaletea fursa za kiuchumi watu wale waliosahaulika kimaendeleo miaka 51 sasa tangu uhuru.Ni rais huyohuyo alietamka kuwa Wanamtwara wajiandae eneo lao kuwa ukanda wa viwanda.Leo anaitoa gesi viwanda hivyo vinajengwaje hapa kama sio usanii ni nini!
Wanamtwara wamesema tukio hili ni mwendelezo wa matukio mengine ya kuhujumu maendeleo ya eneo la kusini kwani miradi mingine imefanyiwa umafia hivyohivyo.
(a)reli ya Nachingwea-Mtwara iling'olewa kwenda Mikumi-Kilosa,lakini hawakuboreshewa barabara kule,Nachingwea ni vumbi tupu
(b)mradi wa Mtwara corridor umekufa bila maelezo,badala yake bandari mpya inapangwa kujengwa Bagamoyo.bandari ya Mtwara haihitaji kuchimbwa ina kina asilia,sasa mradi huu unaanzaje na ule wa Mtwara hauna majibu.
(c)barabara ya Dar-Lindi miaka 51 sasa haijakamilika,bomba la gesi miezi 18.Je,mradi wa gesi unachukua muda mfupi kwa vile unaenda Dar lakini barabara inayokwenda kusini nusu karne!! Haya ni baadhi tu.
Sasa kwa majibu ya JK jana nilitegemea atajibu hoja hizi,kinyume chake anaelekeza shutuma kwa wanasiasa kwa uchochezi,haiingii akilini hata chembe.Yaani rais anadhani kusini bado wapo gizani hat bongo zao na hivyo hawawezi kuona dhulma wanazofanyiwa na serikali hii iliyotawala nusu karne.Hapana hapa amechemsha.Leo anatumia ubabe kufanikisha malengo yake,lakini apime athari za udikteta huo siku za usoni.Anadhani madhila yanayotokea kwa wenzetu yalitokana na watu hao kudhulumiwa kwa muda mrefu na mwisho wakasema,HAPANA INATOSHA!!tunaona kinachoendelea sasa.
Yale majibu alotoa eti wananchi wale wajiandae kwa maendeleo ya viwanda mbona hasemi ni kwa namna gani,mbona anatoa majibu rahisi kwa maswali magumu.Aache usanii kwa hili maana wale watu wamechoka,asifikilie kama wawakilishi walio serikalini toka kusini wanakubalika tena hamna anaewapenda tena maana ni wasaliti.
AU NIMALIZIE KWA KUHOJI,KWA VILE JK HII NI NGWE YAKE YA MWISHO AMEAMUA KUENDELEZA ZILE FALSAFA ZAO ZA "CHUKUA CHAKO MAPEMA,KILA MTU ATABEBA MSALABA WAKE MWENYEWE,HATA WATANZANIA WALE NYASI NDEGE YA RAIS ITANUNULIWA".Hizi nukuu chache zinazowafanya Wanakusini wapoteze imani na serikali yao.Lakini pia JK atambue kuwa wanasiasa anaowalalamika wameenda kwa wananchi wakawapa elimu wakatambua haki zao na namna serikakli hii inavyowapuuza.Kwa hiyo asidanganye umma eti wanachochea vurugu, siyo kweli.Kwani ufisadi,rushwa,na maovu kama hayo yanayoimaliza taifa hili yanaibuliwa na nani,sio hao wanasiasa anaoowaita wachochezi?
Wanamtwara wale wameshaona hila wanazofanyiwa,hivyo hawadanganyiki tena.TAFAKARI NAMI......