Elections 2010 JK aanza rasmi uteuzi wa safu ya uongozi wake

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE amemteua Jaji Frederick Werema kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
 
kwani ni lini aliachia ngazi

Kaka Rais akiisha apishwa , ina maana serikali inakuwa inaanza upya kaka. Ndio maana ameanza na uteuzi wa Mwanasheria mkuu halafu wanafuatia wengine mawaziri nk
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE amemteua Jaji Frederick Werema kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Vipi hajakukumbuka? Amka wewe, Werema alikuwa mwanasheria mkuu hata kabla ya uchaguzi.
 
kaka rais akiisha apishwa , ina maana serikali inakuwa inaanza upya kaka. Ndio maana ameanza na uteuzi wa mwanasheria mkuu halafu wanafuatia wengine mawaziri nk

jamani naomba tuwe tunafikiri kwanza kabla ya kukurupuka kutoa mada ambazo ki ukweli hazina uhakika.
Jibu maswali yafuatayo kisha utoe hitimisho:
  1. baraza la mawaziri lilivunjwa lini?
  2. je raisi alipokuwa anaenda kuapa alikuwa kama raisi au alikuwa raia wa kawaida aliechaguliwa kuiongoza nchi??
  3. kama wateule wa raisi wanafikia kikomo pale raisi anaposita kuwa raisi,unafaham wangapi wangehiatji ku step down??(kuanzaia wakurugenzi wa wilaya mpaka judge mkuu).
  4. katiba inasema raisi anakoma kuwa raisi wakati upi na vp kuhusu wateule wake??
nimejadili, nasubiri majibu
 
Vipi hajakukumbuka? Amka wewe, Werema alikuwa mwanasheria mkuu hata kabla ya uchaguzi.

Kaka sikujua kama huijui katiba kiasi hiki. Nimeamini kweli wewe ni mkenya aisee. Kwani JK hakuwa rais kabla ya uchaguzi ? hakuapa ? mbona leo ameapa tena ?. Katiba inasema Rais atakapo chaguliwa na baada ya kuapishwa mojawapo ya jukumu lake ni kumteua mwanasheria mkuu wa serikali, hilo ndilo amelifanya. Ametekeleza katiba mzee. Soma katiba, acha longo longo.
 
jamani naomba tuwe tunafikiri kwanza kabla ya kukurupuka kutoa mada ambazo ki ukweli hazina uhakika.
Jibu maswali yafuatayo kisha utoe hitimisho:
  1. baraza la mawaziri lilivunjwa lini?
  2. je raisi alipokuwa anaenda kuapa alikuwa kama raisi au alikuwa raia wa kawaida aliechaguliwa kuiongoza nchi??
  3. kama wateule wa raisi wanafikia kikomo pale raisi anaposita kuwa raisi,unafaham wangapi wangehiatji ku step down??(kuanzaia wakurugenzi wa wilaya mpaka judge mkuu).
  4. katiba inasema raisi anakoma kuwa raisi wakati upi na vp kuhusu wateule wake??
nimejadili, nasubiri majibu

Kwa faida yako nenda kasome katiba kuanzia ibara 42-59 majibu yote yako wazi. Ila kwa ufupi tu nakupa kuwa ndani ya katiba imesema kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali atashika madaraka yake mpaka mara tu kabla ya Rais Mteule kushika madaraka ya Rais ( Ibara ya 59(5)(b), sasa baada ya JK pale leo kumaliza kuapa kulikuwa hakuna mwanasheria mkuu wa serikali, ndio maana amemteua tena. Na kuhusu mawaziri wao watashika madaraka yao hadi siku ambapo RAIS mteule ataapa kushika kiti chake, kwa maana hiyo kwa hivi sasa nchi haina mawaziri kaka. Ila katiba inasema ndani ya siku 14 Rais lazima awe amemteua mtu kushika nafasi ya uwaziri mkuu ambapo atathibitishwa na bunge kwa wingi wa kura za bunge.
 
Tuwekee Katiba hapa,or a link to katiba page,and the page where it says urais unakoma saa ngapi,na uteuzi wa watendaji muhimu wa Jamhuri unaanzia wapi
 
Kaka sikujua kama huijui katiba kiasi hiki. Nimeamini kweli wewe ni mkenya aisee. Kwani JK hakuwa rais kabla ya uchaguzi ? hakuapa ? mbona leo ameapa tena ?. Katiba inasema Rais atakapo chaguliwa na baada ya kuapishwa mojawapo ya jukumu lake ni kumteua mwanasheria mkuu wa serikali, hilo ndilo amelifanya. Ametekeleza katiba mzee. Soma katiba, acha longo longo.

Ibara ya ngapi ya katiba niisome sasahivi ndg yangu? hapo ndipo ninapokupenda ukinipa ibara inayosema mara rais akiapishwa anamteua mwanasheria mkuu, kwa sababu sikusikia amemwachisha kazi, wala hata siku aliyovunja baraza la mawaziri. Najua kuwa alivunja mbunge.

Wewe ndiyo siyo mtanzania ndiyo maana unajipendekeza kwake, angalia asije akakuomba kitu. mimi ni mtanzania halisi ndiyo maana sina uoga kutete maslahi ya nchi yangu.
 
Tuwekee Katiba hapa,or a link to katiba page,and the page where it says urais unakoma saa ngapi,na uteuzi wa watendaji muhimu wa Jamhuri unaanzia wapi

Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti
hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;
au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii.

Ibara ya 42 (3)
 
mwenye katiba atumwagie humu ili na sisi 'taburra rassa' wa katiba tuingize kitu ndani ya vichwa vyetu!
 
"jini-ass Brain" Vipi kuhusu raisi akae nje ya nchi kwa kipindi cha zaidi ya miezi 6????????????????
 
Wanasheria hebu tupeni mchakato, huu utaratibu mpya wa kutovunja baraza la mawaziri na kila mtu kubaki madarakani tathmini yake mnaionaje?

Mi naona kama ni nzuri kwa chama kilichoko madarakani, ila tuseme chama fulani tofauti kiwe kimeshinda, itakuwa rahisi kweli kukabidhi mikoba? Lipo angalizo kweli? Hakuna mahali pennye kasoro hebu rusheni vipengele vya katiba hapa wataalamu wa sheria
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom