sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,285
Jiwe kubwa (asteroid) lililopewa jina la Apobhis kupita karibu na dunia(flyby) mwaka 2029. Jiwe hilo liligundulika na Wanasayansi wa anga mwaka 2004 likiwa na takribani mita 340 za Kipenyo na litapita karibu na dunia kiasi cha umbali wa Km 31,000 kutoka duniani.
Ingawa Wanasayansi bado wanaamini jiwe hilo halitakuwa na madhara yoyote kwa dunia ila wanaamini ni moja ya nafasi chache zitakazowawezesha kujifunza zaidi juu ya mawe haya yanayopita karibu na dunia.
Kwa ukubwa wa jiwe hili inasemekana kuwa kiasi cha watu billion 2 wataweza kuliona kwa macho bila kutumia kiona mbali. Bado hakuna maelezo kamili juu ya muda na mahali gani haswa litaonekana ila wanasayansi bado wanajipanga namna ya kuweza kukusanya data na kujifunza zaidi juu ya jiwe hilo.
Pamoja na kuwa Wanasayansi wanaamini kuwa jiwe hilo halitakuwa na madhara yoyote ila bado wanaamini kuna uwezekano mkubwa miaka mingi ijayo dunia ikaja kugongwa na mawe ya angani kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mawe haya yanayopita karibu na dunia.
Source :

Huge Asteroid Apophis Flies By Earth on Friday the 13th in 2029. A Lucky Day for Scientists
Planetary defense specialists and asteroid scientists are already looking forward to a 2029 close approach of a relatively large asteroid called Apophis.
www.space.com