meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,829
- Thread starter
-
- #21
una covermatibabu ya meningitis?
CHF ni moja ya social health insurence zinazoweza wakomboa wananchi kupitia risk pooling. Yaani wazima kuwachangia wagonjwa. Tatizo kubwa lililopo kwa sasa kwenye mfuko huu ni utaratibu mbaya wa matumizi ya fedha hizi. Zinalipiwa per diem badala ya kununulia dawa, maeneo mengi hazitumiki kabisa kutokana na ukiritimba wa sheria zake/za manunuzi. Watu walichanga na baadae kuona mfuko huu hauwasaidii kitu kwa kuwa fedha yake haiwarudii walengwa. Nyingi hubaki kama bakaa kwenye accounts za halmashauri.
Ili kuboresha mfuko huu, ni lazima halmashauri zitunge sheria na taratibu za mfuko huu zitakazosimamia ukusanyaji wake na matumizi yake. Vinginevyo hakuna mwananchi atakae changa na asione fedha yake imefanya nini.
Kujiunga na Chf si tatizo.tatizo lipo pale utakapo ugua na kwenda kituo cha afya au hospitali na kuandikiwa KIPIMO AU DAWA NA KUSHAURIWA AU KUTAKIWA UKANUNUE DUKA JIRANI TENA KWA BEI GHALI!
fika kwenye zahanati yako ya karibu ukiona wanakuzingua nenda kwenye ofisi ya mganga mkuu wa wilaya.Hii ni habari njema kwetu sisi tunaoishi huku vijijini. Naomba kufahamishwa endapo nitajiunga na mfuko huu wa CHF ni kituo gani cha afya nitakwenda kupata tiba katika hiki kijiji chetu cha Kibara wilaya ya Bunda
fika kwenye zahanati yako ya karibu ukiona wanakuzingua nenda kwenye ofisi ya mganga mkuu wa wilaya.
Waweza kujiunga katika kituo cha kutoa huduma za afya kilichopo karibu na wewe.hapa namaanisha zahanati,kituo cha afya na kwa sasa hata hospitali za wilaya na baadhi ya hospitali za mikoa.
Kuhusu matibabu ya gharama gani?
Hapa unaweza kujionea kuwa kutokana na mchango ulivyo..CHF ililenga matibabu katika ngazi za msingi hasa hasa zahanati na vituo vya afya.pia miongozo ilielekeza mgonjwa apewe huduma za kawaida kwa lugha rahisi na ngumu kidogo 'general OPD services'
ambapo kwa maeneo mengi ni kati ya shilingi 500-5000.Kwa uzowefu wangu kwa sasa kuna wilaya nyingi zimeamua kutoa huduma zote kwa ngazi zote za huduma yaani kama umejiunga na CHF basi utatibiwa bila kuingia mfukoni katika kituo cha huduma ''cha serikali au chenye mkataba na serikali'' kwenye wilaya husika.
Ni obvious kwamba kwa sasa huwezi kutegemea CHF ikufanyie vipimo vikubwa kama CT SCAN AU MRI!
kwa miundo mbinu iliyopo katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini unaweza kupata huduma ya magonjwa kumi yanayosababisha watu kufika hospitalini.
Ni vizuri kutoa 5000 kwa mwaka kuliko kutoa 3000 kwa kila unapohudhuria,Mfano kwa mwaka unaweza kuhudhuria hospitali mara moja,mke wako akahudhuria mara mbili,binti yako akahudhuria mara moja na katika kila hudhurio mlilipa 3000 mtakuwa mmetumia shilingi 12000.
una covermatibabu ya meningitis?
CHF ni moja ya social health insurence zinazoweza wakomboa wananchi kupitia risk pooling. Yaani wazima kuwachangia wagonjwa. Tatizo kubwa lililopo kwa sasa kwenye mfuko huu ni utaratibu mbaya wa matumizi ya fedha hizi. Zinalipiwa per diem badala ya kununulia dawa, maeneo mengi hazitumiki kabisa kutokana na ukiritimba wa sheria zake/za manunuzi. Watu walichanga na baadae kuona mfuko huu hauwasaidii kitu kwa kuwa fedha yake haiwarudii walengwa. Nyingi hubaki kama bakaa kwenye accounts za halmashauri.
Ili kuboresha mfuko huu, ni lazima halmashauri zitunge sheria na taratibu za mfuko huu zitakazosimamia ukusanyaji wake na matumizi yake. Vinginevyo hakuna mwananchi atakae changa na asione fedha yake imefanya nini.
Ina cover matibabu ya meningitis?
Unaweza ukadhani ni swali la utani !
Meningitis ni ugonjwa unaotibiwa kwa mgonjwa kulazwa,kufanyiwa vipimo ikiwa ni pamoja CSF analysis,kupewa dawa na matibabu saidizi!Kimuongozo CHF hatakiwi kuhudumia wagonjwa waliolazwa la uzoefu nilioupata kutoka kwa wilaya zilizofanikiwa katika CHF kwa sasa zinahudumia wagonjwa waliolazwa na hawajapata hasara au kushindwa kuwahudumia.
Mkuu nahisi bado unaongelea experiance ya miaka ya nyuma ambapo mapato ya mfuko huu yalitumika vibaya.
Matumizi ya mfuko huu yameelekezwa vizuri tu yaani asilimia 60+ inatakiwa kununua dawa na vifaa tiba,asilimia zilizobaki ni kwa ajili ya motisha(extra duty allowance),ukarabati mdogo na ajira.
Tatizo lililolalamikiwa sana ni kuhusu matumizi ya fedha inayoitwa tele kwa tele,hii ni fedha inayotolewa kwa halmashauri husika baada ya kuenroll wateja wa CHF yaani kama halmashauri imepata wanachama 100 *5000 =500000 basi central gov/NHIf itawaongezea 500000 nyingine(hii ndio ilikuwa inaliwa badala ya kupelekwa kwenye kituo)
kumbuka kila kituo kinatakiwa kuwa na account ya CHF na signatories ni mkuu wa kituo husika na mwenyekiti wa kamati ya kituo.
Usidharau nguvu ya uwepo wa fedha hizi,kwani kwa sasa ndizo zinazofanya huduma ziendelee katika vituo vyetu pamoja na kutokuwepo au kucheleweshwa kwa fedha za wahisani.
Nasisitiza kuwa CHF inaweza kuwa mbadala wa fedha za wahisani.
Sitoi hata senti kumi kwa sababu hizi ulizozieleza hapa mkuu! Nichangie mfuko unaoendeshwa na ukoo wa panya! Si bora wazo hili nilipeleke SACCOS yetu ili tuendeshe Health Fund yetu huku nikijua internal control imo mikononi mwetu wanachama?
Nashukuru sana kwa taarifa maana huku vijijini ni huduma hakuna njooni mhamasishe tunahamasa kubwa sana tatizo ni vituo vya tiba
Wasalaamu wana JF!
Baada ya kutafakari sana nimeona nije na mada hii hapa jamvini ili tujisaidie wenyewe kama watanzania na wanajamii,namaanisha tusisubiri serikali,wanasiasa au wahisani watusaidie!
UTANGULIZI
Nadhani tumesikia mara kwa mara kuhusu vilio vya wananchi kuhusu utoaji wa huduma katika vituo vya afya hususani vile vya serikali.Tumesikia kuhusu uhaba wa dawa na vifaa muhimu vya tiba bila ya kupata suluhisho la kudumu.
Pia tumesikia juu ya ukosefu wa fedha unaopelekea kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.Ukosefu huu umeelezwa na kuhusishwa na bajeti ndogo inayotengwa katika wizara ya afya mfano mzuri ni mwaka huu tumejionea bajeti ya wizara hii ikishuka kwa takribani 1/4 kulinganisha na mwaka jana kinyume kabisa na makubaliano ya Abuja ambayo yanapendekeza karibu asilimia 15 ya bajeti ya nchi ilenge afya.
Pia tumesikia kuhusu ucheleweshaji au usitishwaji wa bajeti za wahisani katika sekta hii.
Vile vile ni mara chache kusikia halmashauri imetenga au kutoa pesa zitokanazo na makusanyo ya ndani kwa ajili ya idara ya afya.
Serikali both local na central zinaamini fedha kutoka kwa wahisani zinatosha kuhudumia sekta ya afya!
KUHUSU UCHANGIAJI WA WANANCHI KATIKA HUDUMA ZA AFYA
Kuna mfumo uliowekwa kwa wananchi kuchangia huduma za afya;
1.Uchangiaji wa fedha wakati wa kupata huduma yaani papo kwa papo.hapa ni kama vile unavyohudhuria hospitali na kutakiwa kulipa fedha kwa ajili ya faili,vipimo au kulazwa wadini.
Mfumo huu ni mzuri lakini una changamoto nyingi hasa hasa rushwa.
2.Mfumo wa pili ni ule wa kutimia bima za afya,hapa naongelea wale waajiriwa.
NHIF yaweza kuwa ndio bima ya afya iliyofanikiwa au kutimiwa kwa wingi hapa nchini.
3.Mfumo wa tatu na muhimu kwa mada hii ni ule wa mfuko wa afa ya jamii (CHF aka community health fund).
Nitelezea zaidi kuhusu CHF hapo chini.
Kwa ufupi mfumo hii mitatu ndiyo mifumo muhimu ya jinsi gani mwananchi anaweza kuchangia huduma za afya nchini.Yawezekana kuna mingine lakini kwa ufupi na umuhimu hiyo hapo juu ndio mifumo ya kuchangia huduma za afya nchni.
KUHUSU CHF
Kama nilivyosema hapo juu huu ni mfuko wa uchangiaji huduma za afya kwa ngazi ya jamii.
Kila kaya hutakiwa kuchangia kiasi flani cha fedha kwa mwaka mara nyingi ni 5000 au 10000 kwa mwaka na hivyo mwanakaya atakapoumwa atatakiwa kutibiwa matibabu ya kawaida kwa mwaka mzima bila kutoa chochote katika kituo chake cha karibu.Tukumbuke kuwa wastani wa kaya nchini ni 4-6 hivyo mfuko utawajibika kwa watu wanne mpaka sita kwa kutegemea ukubwa wa kaya katika maeneo mbalimbali.
Mfuko huu ni mzuri kwa familia masikini zisizo na ajira rasmi.kuna maeneo kama singida wanasema 'kuku mmoja tiba mwaka mzima'
pia halmashauri yaweza kupewa fedha kulingana na idadi ya kaya zilizojiunga kwa mfano zimejiunga kaya 100 na kulipa shilingi 10000*100 ambayo ni shilingi 1000000 basi halmashauri itapewa nyongeza ya sh. 1000000.
Matumizi ya fedha zinazotokana na mfuko huu ni manunuzi ya dawa na vifaa tiba,posho na ukarabati katika kituo kilichoandikisha wanachama.
Kwa ufupi tu haya ndio yanayohusu mfuko huu wa afya ya jamii.
MAONI YANGU
Kwa kuwa jamii kubwa ya watanzania ni masikini lakini sio masikini wa kukosa 5000 au 10000 kwa mwaka ni vyema tukahamasishana kujiunga na mfuko huu.
Tatizo la dawa na vifaa tiba linaweza kumalizwa kwa kuwezesha kila kaya kuwa insured na mfuko huu.
Tujenge utamaduni wa kuchangia huduma za afya na tuondokane na kasumba ya kutegemea hisani za watu wa marekani!
Nipo tayari kwa ufafanuzi zaidi...!
Kumbuka:Sijatokea NHIF/MOHSW bali ni mdau katika sekta ya afya nimejitolea kuhamasisha kwa manufaa ya jamii yetu masikini.
KARIBUNI KWA MJADALA
mkuu hata huko kwenye saccoss kunatokea matatizo ya udhibiti wa mapato!kama alivyosema Iron Lady umiliki ni wa wananchi wenyewe.Sitoi hata senti kumi kwa sababu hizi ulizozieleza hapa mkuu! Nichangie mfuko unaoendeshwa na ukoo wa panya! Si bora wazo hili nilipeleke SACCOS yetu ili tuendeshe Health Fund yetu huku nikijua internal control imo mikononi mwetu wanachama?
Safi sana mkuu!Aidha Mchango wa kaya hutofautiana kutoka wilaya moja na nyingine. Kiwango cha mchango hupangwa kwa vikao na ushiriki wa wananchi na halmashauri husika kulingana na haki ya kiuchumi ya wakazi wilaya hiyo. Ipo michango ya 10, 000 kwa kaya 15000 kwa kaya 5000 kwa kaya hadi 20000.
Ni muhimu kujus wilaya yako mchango ni dh ngapi kwa kaya.
Pia wanafunzi wa sekondari hilipia 2000 na wakiwa watano hutoa 10000 na kutengeneza kama kaya hivyo nao kupata huduma hizi kwa mwaka mzima. Kwa uchangiaji huu
Safi sana mkuu!
Mkuu hili ni swali la ki-NHIF zaidi hapa tunaongelea CHF ,pamoja na kwamba NHIF imepewa jukumu la kusimamia CHF halmashauri zina uhuru wa kuamua ni huduma gani zitatolewa kupitia CHF!Mojawapo ya mafao yenu ni FAO LA KUTIBIWA KINYWA NA MENO...
Katika fao hilo NHIF imeeleza kwamba haitatoa huduma ya jino bandia kwa kuwa huo sio ugonjwa ni kama anasa.
Je, kama jino la mwanachama wenu limeoza kabisa na kumfanya ashindwe hata kufanya kazi zake za kila siku, hamuwezi kumpatia matibabu ya kung'oa jino hilo na kumpatia jino lingine? au nalo ni la anasa?
Kama kipato chako kiko vizuri nenda ofisi za NHIF,Kama kipato chako ni kidogo nenda ofisi ya mganga mkuu wa wilaya unayoishi ingia kwenye CHF!mkuu mleta mada,
nimejiahiri na natamani sana niwe na bima ya Afya,nina family watu wanne.
_ningekushukuru sana kama utanielekeza mfuko sahihi wa kujiunga nao na taratibu.
nipo mwanza
Huu mfuko ungeweza kusaidia sana watu wasio kwenye ajira rasmi.Nafikiri kuna tatizo kubwa kwenye uhamasishaji,ntafanya mpango nijiunge