Mahitaji
1) Binzari ya pilau 250g
2) Karafuu kijiko kimoja cha kulia
3) Iliki 125g
4) Pilipili manga 100g
5) Mdalasini vijiti 10 vikubwa, vunja vunja
Namna ya kutayarisha
- Weka sufuria katika moto
- Kaanga viungo vyote taratibu visiungue
- Weka vipoe
- Saga alafu hifadhi katika chupa yako
Mchanganyiko huu unaweza tumia kupikia pilau, biriani n.k