Jinsi ya kupika wali wa Kichina

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Wali wa kichina.jpg

Vipimo
Mchele (Basmati) - 3 vikombe
Mbogamboga za barafu
(karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
Mayai - 2 mayai
Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
Paprika - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
Tangawizi - 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 1
Soy sauce - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
  1. Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.
  2. Tia mafuta kidogo katika wok (aina ya karai)
  3. Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.
  4. Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha na kupika Wali
  1. Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
  2. Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi
  3. Wacha uchemke asilimia 70%
  4. Chuja maji na weka kando
  5. Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu
  6. Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)
  7. Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga
  8. Kisha tia wali changanye vizuri
  9. Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive
  10. Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.
 
Tatizo lugha, mboga ya barafu najulia wapi Mimi, na hakuna hata mbadala kwa mazingira kwamba ukikosa kwamfano thomu au kidonge Cha supu uweke nini?

Na huo mchele wa basmati ni kitu gani?
 
Tatizo rugha, mboga ya barafu najulia wapi Mimi, na hakuna hata mbadala kwa mazingira kwamba ukikosa kwamfano thomu au kidonge Cha supu uweke nini?

Na huo mchele wa basmati ni kitu gani?
Ngoja nimsaidie kujibu

Thomu ni kitunguu swaumu

Basmat ni mchele maalum kwa ajili ya kupikia biriyan

Hapo kwenye mboga za barafu sijui alimaanisha nini ila unaweza tumia za kawaida... njegere, carrot unakata shape ya vibox, spring beans hizi zipo zinauzwa masokoni na mahindi yale mabichi.

Na kidonge cha supu sifahamu ila unatumia supu ya huyo kuku uliyemchemsha.
Nimeelezea jinsi ambavyo hua napika japo nilikua sijui kama ndo wali wa kichina.
 
Me huo mchele wa basmart siupendi siwezi tumia huu wa kawaida maana ni mtamu na una harufu nzuri.

Halafu kuhusu hivyo vipimo me siwezi kushiba😀. Nitaongeza kidogo hata ifike kilo ili nibakiwe na kiporo kwa ajili ya asubuhi.
Sawa sawa unaweza kuongezea kadri upendavyo
 
Ngoja nimsaidie kujibu

Thomu ni kitunguu swaumu

Basmat ni mchele maalum kwa ajili ya kupikia biriyan

Hapo kwenye mboga za barafu sijui alimaanisha nini ila unaweza tumia za kawaida... njegere, carrot unakata shape ya vibox, spring beans hizi zipo zinauzwa masokoni na mahindi yale mabichi.

Na kidonge cha supu sifahamu ila unatumia supu ya huyo kuku uliyemchemsha.
Nimeelezea jinsi ambavyo hua napika japo nilikua sijui kama ndo wali wa kichina.
 
Ngoja nimsaidie kujibu

Thomu ni kitunguu swaumu

Basmat ni mchele maalum kwa ajili ya kupikia biriyan

Hapo kwenye mboga za barafu sijui alimaanisha nini ila unaweza tumia za kawaida... njegere, carrot unakata shape ya vibox, spring beans hizi zipo zinauzwa masokoni na mahindi yale mabichi.

Na kidonge cha supu sifahamu ila unatumia supu ya huyo kuku uliyemchemsha.
Nimeelezea jinsi ambavyo hua napika japo nilikua sijui kama ndo wali wa kichina.
Sasa je mbona nimeelewa
 
Uko vizuri, kumbe unajua kuupika. Nitakuja unifundishe eti?
 
Ni wali mzuri sanaa, mwaka 2018 nilibahatika kula pale "Al baruch" mjini morogoro kwa upishi ule ikisindikizwa na rosti la firigisi natamani kurudia tena, ila kwa upishi wa nyumbani na hayo mahitaji tu tayari nishafeli.
 
😂😂usikubali kufeli tafuta angalau siku 1
 
Napenda sana wali kiukweli.
Basi pika huu simpo:
Mahitaji ni mchele
Vitunguu + carrot ikwangue

Then unakaanga vitunguu na carrot vikiikaangika vizuri weka mchele nao kaanga hadi mchele ukolee carrot then weka maji ya moto kiasi ambacho utaona yataivisha wali. Pika kwa moto wa wastan hadi wali uive.

Usisahau kuweka chumvi
 
Basi pika huu simpo:
Mahitaji ni mchele
Vitunguu + carrot ikwangue
Then unakaanga vitunguu na carrot vikiikaangika vizuri weka mchele nao kaanga hadi mchele ukolee carrot then weka maji ya moto kiasi ambacho utaona yataivisha wali. Pika kwa moto wa wastan hadi wali uive
Usisahau kuweka chumvi
Njegere pia na hoho si naweza changanya. Ila njegere lazima niwe nimechemsha kabla? Baada ya kuukanga siwezi kuuhamishia kwenye rice cooker?
 
Njegere pia na hoho si naweza changanya. Ila njegere lazima niwe nimechemsha kabla?
Baada ya kuukanga siwezi kuuhamishia kwenye rice cooker?
Yes unaweza changanya njegere zilizochemshwa.
Jikoni unaogopa kuunguza 😀😀
Unaweza hamishia mradi uweke tu kipimo cha maji sahihi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom