N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,990
- 12,019
"Roho mbaya" ni neno subjective. Hata hivyo kuna viashiria vya msingi kabisa ukiona unavyo, basi jitambue una roho mbaya, anza mkakati wa kujirekebisha. Mambo hayo ni kama ifuatavyo:-
1. Unafurahi unapowaona wengine wakipata matatizo. Ndugu yangu kama unafurahia watu wanaposhindwa au kuumia, hiyo ni ishara ya roho isiyo na huruma na ndiyo roho mbaya yenyewe. Kumbuka roho mbaya "ni uchawi".
2. Hufurahii mafanikio ya wengine.
Badala ya kuwapongeza, unawachukia na kuanza kusambaza maneno ya kuwashusha.
3. Kila jambo kwako ni mashindano. Kwa kifupi ni kwamba huwezi kufurahia kilicho chema kwa mwingine bila kujilinganisha au kutafuta jinsi ya kumpiku.
4. Unapenda kusambaza umbea, fitina na chuki. Mara nyingi unakuwa chanzo cha migogoro kwa kusema mambo yasiyofaa kuhusu wengine.
5. Husaidii bila masharti au bila kutaka sifa. Kila msaada unaotoa, unautangaza au unataka kulipwa fadhila.
6. Hutaki kuomba msamaha hata ukikosea. Kiburi kimekuzidi kiasi kwamba huoni umuhimu wa kusema “samahani.”
7. Kukosa huruma kwa walio katika hali ngumu. Huwezi kuguswa au kuonyesha utu kwa walio katika matatizo makubwa kv. Wanaouguliwa, waliofiwa, wenye magonjwa makubwa, yatima, nk.
8. Unaficha au kuzuia taarifa zitakazosaidia wengine(hii inawagusa sana baadhi ya maafisa wa taasisi za umma). Kwa sababu ya wivu au hofu ya wao kufanikiwa, huwezi kuwapa msaada wa maarifa au nafasi.
9. Unafanya mambo mazuri kwa ajili ya sifa tu. Hakuna uchaji wala nia njema, unafanya ili upewe pongezi au ujionyeshe kwa wengine. Wakati fulani hata hujafikia hadhi ya hicho unachofanya kv kumiliki gari wakati huna mapato ya kuhudumia gari ilimradi tu uwe gumzo kwa watu wanaokuzunguka.
10. Unachukia watu wanaokupita kimaendeleo. Badala ya kujifunza kwao, unawachukia kimya kimya au hadharani. Mara zote unawabatiza majina mabaya kv wachawi, wevi nk.
MY TAKE:
Kama umejikuta kwenye baadhi ya haya, bado kuna nafasi ya kubadilika na kuboresha kiwango cha utu wako.