Kuulizwa unapika nini na umenunua kiasi gani nayo imekuwa kesi? wengine wanauliza ili wapate ufaham wajichangishe wakatafute vya kwao, ukitaka usiulizwe kaishi masaki mama, sipati picha ukiishi nyumba yenye watoto alafu waombe kuangalia TV kwako
Nashindwa kumuelewa jirani yangu na ananifanya nisiwe comfortable.... Nyumba ninayoishi tupo watano kila mtu na kwake anaijtegemea wote ni vijana na hakuna mwenye familia. Tupo wadada wawili tu. Huyu dada jirani yangu alinikuta wakati akihamia hapo na mwanzoni alipata matatizo nikamsaidia kama kama ambavyo ningemsaidia binadamu yoyote. Aliumwa na hakuwa na ndugu karibu (kwao Shinyanga) hivyo nilimhudumia kwa ukarimu wote nilimpikia, na kumsaidia kufanya usafi hadi alipopata nafuu.
Baada ya kupona maisha yaliendelea japo hatukua na ukaribu zaidi ya salamu na mambo basic kama kushare bills. Kumbuka sisi ni vijana na pretty much ndio tumeanza kujitegema so hatujajiestablish kihiivyo...ila nimegundua huyu jirani yangu ni kama anawivu ama sijui ni kitu gani. Alipokuja kwangu kila alichokiona alitaka kujua ni menunua bei gani na vingine alidiriki kuniuliza umenunuliwa na mpenzi wako? Sikumbuki nilipotezeaje coz sionagi kama ni sawa ku disclose mambo yangu binafsi kwa mtu ambae sio wa karibu.
Ila naona ni kama tabia kila tukionana akiona nimebadilisha style atauliza umesuka bei gani, juzi kaniona na simu kaniuliza mbona hujanionyesha kitu kipya. yani hata nikinunua maybe kiblouse kipya lazima atauliza. Kinachonimaliza ni kwamba hata kama niko ndani napika ataongea from her room eeeeh jirani leo unapika samaki au leo unapika kitu flani? Hua namjibu kwa maneno machache tu.
Bottom line ni kwamba she makes me uncomfortable!!!!!!! Yani very uncomfortable!!!!! Akiona mpenzi wangu wangu yupo ndani atakuja kunigongea either aombe kitunguu au kibiriti.
Nisaidieni jirani wa hivi naishije nae?????
