Sehemu ya 17
Kitasa kilicheza kuashilia mlango unafunguliwa ila mwili ulinisisimka nikahisi kuna kitu nikabadili mada fasta.
"Shomy angalia kwa hapo juu ipo."
Shomy naye alicheza kama pele fasta akajiongeza,
"jirani siyioni,"
"Kwenye msumali hapo haipo?."
"Siyioni jirani,"
mala sauti ikatoka nyuma yangu.
"niliipeleka chumbani Taulo,"
"sasa mbona huku niambia mpaka namsumbua jirani?"
"Nilipitiwa,"
Nilitoka eneo la bafuni nikaenda sebureni,
*mh!!! Kidogo nibambwe sababu zote zingehamia kwangu*
Baada ya dk5 shomy alitoka bafuni,
Alipofika sebuleni alinisota na kidole akanionesha ishara ya kuchapwa,
Baada ya dk10 sms iliingia kwenye simu yangu ilikuwa ikitoka kwa shomy.
*seif ungeshikwa ugoni leo,*
*ningeshikwa ugoni au tungeshikwa ugoni?.*
*sijui ingekuwaje ungeombwa talaka leo,*
*hana jeuri hiyo,*
*haya usiku mwema seif,*
*na wewe pia,*
*ila kesho usiniache nataka rifti,*
*sawa,*
*haya usiku mwema,*
******** ***
Na mimi niliingia chimbani nikaenda kulala zahara alikiwa jikoni akikangaa mayai na kuandaa mkate,
Nilipofika kitandani nilipitiwa na usingizi nikawa nimelala mida saa nne usiku zahara alinifuata kitandani.
"Mme karibu tukale,"
Nilimnyamanzia akarudia tena.
"Mme wangu karibu chakula,"
"Mimi nasikia usingizi bana niache nilale,"
Alikuwa mpole akarudi kukaa sebureni hata kula alishindwa akarudi kulala,
Palikucha siku hiyo aliamka mapema kuliko siku zote.
Alijianda fasta kisha akaniaga.
"Mimi nakwenda,"
"Sawa, unaenda na usafiri gani?."
"Napanda bajaji hapo nje,"
"Ndivyo ulivyoamuwa?"
"Hapana nawahi,"
"Sawa nenda,"
Aliondoka nilichukua simu nikamtumia sms shomy.
*vp umejiandaa?.*
*Ndio nataka kwenda kuoga,*
*mzee yuko wapi?.*
*kaondoka,*
*basi tukutane bafuni nikusugue,*
*dokta hayupo?.*
*kaondoka,,*
*mh!!!... leo sitaki kusuguliwa labda kesho,*
*kwanini*
*acha niwahi kuoga twende bana,*
Nilimpimia nikatoka chumbani kwangu nikasimama mlangoni na shomy wakati huo alikuwa akitoka chumbani kwake.
"Nikusalimie tena seif au salam ya kwenye sms inatosha,,"
"Njoo karibu yangu,"
Alinisogelea bila kupinga nikamkumbatia akalalia kifua changu nikampitishia mkono kiunoni kwake.
"Se....if "naam,...."
"Acha nikaoge,"
aliongea huku akijitoa kwenye mwili wangu na kwenda bafuni niliishia kuangalia maboga yanavyo tikisika siyo siri uchu wa mapenzi ulinishika nikakosa cha kufanya nikamfuata bafuni shomy.
"Shomy....,,"
"abeee....,,"
"Niko vibaya mw..e..nzi..y...o,,"
alijibu kwa sauti raini ya upole iliyojaa huruma.
"se.....iif sina cha kukusaidia kwa sasa.....,, "kwa...ni...ni.."
"Se.....if ja..na umeniletea nini?..."
"Basiii fungua mlango.."
"Se...if jamani....,,"
"Nihurumie shomy..,,"
"Seif na..kuhurumia ilaaa.....,,,"
"Ilaaa...ni...ni..shomy?.."
"Se...if,, "
"naaam shomy,,"
Nilisikia kwikwi ya kulia kwake.
"Shomy mbona unaliyaaa?.."
"Se...if nakupenda lakini??..."
"Lakini nini shomy?.."
"Nimechelewa... na wewe umechelewa.."
"Kivipi??... "
"Una mke seif na mimi nina mme japo kila mmoja anaonesha hana furaha na ndoa yake,"
"Unajua shomy kuna kukosea kuoa na kukosea kuolewa,,"
"Hayo ndio yaliyonikuta mimi seif,,"
"Shomy mimi sikuwa na nia ya kumuowa Dokta nilipeleka posa kwao ili nimuowe ndugu yake anayeitwa Nasra ila nikajikuta nabadilishiwa mke napewa zahara nilitaka kumkata ila alilia sana nikamuonea huruma nikamuowa lakini leo najutia kumhulumia kwa haya anayonifanyia amekuwa sio msikivu amekuwa yeye na simu tu,"
"Pole sana seif, mimi niliwahi kupendana na kijana mmoja hivi wakati nasoma siyo siri alinipenda sana na ndiye mwanaume aliyenitoa bikira na yeye siku hiyo ndio ilikuwa mala ya kwanza kukutana na msichana tulifurahia siku hiyo nilimpenda sana huyo kijana japo alikuwa ni kijana wa mtaani na kwetu tulikuwa matajiri nilimpa nilichokuwa nacho ili aonekane vizuri mama yangu alimpenda sana huyo kijana.
"Rita Ritaaaaaaa."
Nilimkumbuka ndie aliyekuwa chaguo langu toka nasoma kwa msaada wa tuleane mwanza, nilipomuita jina lake alilokuwa anatumia kipindi cha utoto wake alishituka na mimi akaniita jina langu la zamani.
"Jarudiii jarudiiiii...."
Shomy alifungua mlango wa bafu tukakumbatiana kwa furaha kwani ni miaka mingi sana tangu tulipoachana,,
Tukiwa tumekumbatiana gafla sauti ya mlango kufunguliwa ulisikika .
Itaendeleaaa.....