Jirani sio mstaarabu

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,838
Nimekaa katika nyumba ya kupanga huu mwaka wa nne. Na nimekaa kwa amani sana. Miezi mitano iliyopita kunampangaji mpya kaja jirani yangu, yeye ni mwanamziki fulani hapa nchini.
Mimi huwaninachoka sana nikiwa kazini kwahiyo nina hita ji mda wa kupumizika.
Kinachonisimbua huyu jirani yangu sio mstaarabu yaani ikifika saa tatu au zaidi usiku anafungulia mziki mkubwa kiasi kwamba ninashindwa kulala.
Nimekuwa nikimuambia apunguze huwa anapunguza lakini baada ya siku kadhaa anarudia tena kitendo hicho.
Kilichonikera zaidi jana mida ya saa 5 usiku kaja kusimama dirishani kwangu akiongea na simu kwa sauti ya juu huku akiongea kingereza kilicho vunjika vunjika. alichukua mda mrefu kweli anaongea, anacheka

Hivi nimfaye nini huyu?
Nimechoka kumueleza kila siku. Isitoshe sisi sote ni vijana tumekuja kutafuata hapa Dar.
 
Inabidi ufanye uhame mzee kama muda umebaki mfupi.

Au kama unataka kuendelea kukaa mwambie mwenye nyumba kama hilo swala linakukwaza.
 
tafuta vipaza sauti kama vile vya msikitini weka nje kuelekea chumba chake halafu unganisha kwenye wufer yako na ukitaka kulala fungua volume hadi 70 ataacha
 
loh umenikumbusha sinza na wacongo
na wewe fungulia kwa nguvu tena weka spika usawa wake
 
loh umenikumbusha sinza na wacongo
na wewe fungulia kwa nguvu tena weka spika usawa wake
Tatizo nimetoka job nimechoka. Vile vile wakianza kupiga story kwa sauti ya juu kweli halafu wanaongea lugha yao ya kg.
 
Muwekee tangazo kwenye radio yake akiona tu atakuwa anaheshimu au mpeleke polisi kwani anakusumbua na sauti ya radio yake au anunue sound proof materials
 
Aiseeee babaangu kwanza nikupe pole sana chamsingi we mfate umchane live kwamba anachokifanya kinakukera
 
Fuatilia ujumbe wa sugu::
«Dawa ya bishoo ni kua bishoo zaidi yake»

Kama anapiga mziki mzito,jipinde na wewe fungua mziki wako hadi mwishooo,kama mbwai mwai msikize kifulambute kamaliza kila kitu.
 
Fuatilia ujumbe wa sugu::
«Dawa ya bishoo ni kua bishoo zaidi yake»

Kama anapiga mziki mzito,jipinde na wewe fungua mziki wako hadi mwishooo,kama mbwai mwai msikize kifulambute kamaliza kila kitu.
Ninaweza nikafanya hivyo lakini unajua wanamziki wa bongo wao mchana wanalala so nitakuwa kama najiumiza sana vile. Kumbuka mimi huwa nafanya kazi mchana na ninachoka sana.
 
Ndugu yangu kwanza pole sana hawa watu wapo kila mahali, naomba muone mwenye nyumba amkataze akigoma mwambie mwenyekiti wa Serikali za mtaa na kuwaambia utamfungulia mashtaka (sikumbuki km ni sound pollution au harrasment)
Nafahamu km ndio umeanza kazi kwa dsm na kulipa kodi ya mwaka huwezi tena nunua music mkubwa wa Wofer na kumfungulia mipasho angenyamaza.
ww mpeleke Mahakamani
 
Mfate mwambie tabia yake inakukera an mwambie kwa kumaanisha sio kishkaji.Nadhani ukifanya hivyo atajirekebisha.
 
Nimekaa katika nyumba ya kupanga huu mwaka wa nne. Na nimekaa kwa amani sana. Miezi mitano iliyopita kunampangaji mpya kaja jirani yangu, yeye ni mwanamziki fulani hapa nchini.
Mimi huwaninachoka sana nikiwa kazini kwahiyo nina hita ji mda wa kupumizika.
Kinachonisimbua huyu jirani yangu sio mstaarabu yaani ikifika saa tatu au zaidi usiku anafungulia mziki mkubwa kiasi kwamba ninashindwa kulala.
Nimekuwa nikimuambia apunguze huwa anapunguza lakini baada ya siku kadhaa anarudia tena kitendo hicho.
Kilichonikera zaidi jana mida ya saa 5 usiku kaja kusimama dirishani kwangu akiongea na simu kwa sauti ya juu huku akiongea kingereza kilicho vunjika vunjika. alichukua mda mrefu kweli anaongea, anacheka

Hivi nimfaye nini huyu?
Nimechoka kumueleza kila siku. Isitoshe sisi sote ni vijana tumekuja kutafuata hapa Dar.

Hizo ni changamoto za kawaida kabisa za watu wanaoishi nyumba za kupanga. Utapata amani na kuishi the way unavyotaka wewe pale tu Mungu atakapokupa neema ya kuwa na kwako.

Kwa sasa unaweza kumweleza mwenye nyumba aingilie kati kwa either kutoa muongozo wa wapangaji (kuna badhi ya wenye nyumba hufanya hivi) au akamwita na kuongea naye ili apunguze vurugu hizo za kitoto.

Ikishindika itakubidi uvumilie maana unaweza kuja kuzoea na ukishindwa kabisa unaweza kuhama ingawa kuhama pia kunaweza kukupeleka kwend kuishi na wapangaji wengine wenye tabia mbaya kuliko za huyo mwanamziki!!!
 
Watu kama hao usishindane nao kabisa, ukiona mjinga anafanya ujinga usiwe mjinga kama yeye.

Hama tu.
 
Yanini nidhamu ya uwoga!!!! We muite mkae wewe, yeye na mwenyenyumba tena time hiyo saa 5 mziki ukiwepo kabisa ili kiushahidi kiwepo, alafu mchane live mbele ya faza house. Na faza house nae aseme msimamo wa nyumba yake.
 
Miaka minne unapanga?

mungu kamleta huyu akusumbue ili ujenge

shukuru kwa kweli........ingekuwa full amani usingeshtuka

wenzio woote walioteseka na nyumba za kupanga
sasa wamejenga
 
Ningekuwa naishi uswazi ningekuwa napigana kila siku.

Hapana vumilia huo upuuzi mimi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom