Jirani huyu kiboko

Jirani huyu kiboko

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,348
Hellow JF

Jirani ni mtu muhimu sana kwenye makazi kwa sababu yeye ndiye mtu wa kwanza kukusaidia pale unapopatwa na shida na unahutaji msaada ,ujirani ni muhimu sana kwa binadamu yoyote yule.

Huyu jirani yangu sijui ananijaribu kwa sababu anamtuma sana mwanaye kuja kuomba hapa home kuomba sio kosa kila mtu anahitaji msaada lakini huyu sijamuelewa.

Picha linaanza ikawa inaletwa simu kuchajiwa na kumbuka hapa sisi tumehamia hivi karibuni tu sio wenyeji kabisa kuna siku umeme wetu wa magumashi huu walikata tukawa kwenye Giza siku 2 hamna umeme dogo akatumwa alete simu mama kasema nilite simu ikae tu umeme ukija umchajie,baadaye akaja tena mama kanituma kama una sukari kidogo anaomba.

Siku nyingine akaja mama anaomba kitunguu kimoja kama unacho umpatie.
Jana sasa ndo kali akaja usiku mida ya saa moja hivi mama kasema anaomba umkopeshe mia tano nikamuuliza tena shilingi ngapi amekwambia akasema shilingi mia tano umkopeshe.Aisee Mungu anisamehe tu nikamwambia sina.

Halafu hapo anavuka nyumba kama 3 ndiyo inakuja nyumba ninayo kaa sasa wakat wa story na jiran mwingine akaniambia yaan hiyo nyumba ya chini hapo wakishakuzoea wanaomba hadi kero sabuni ya kuogea wanaomba sabuni ya kuoshea vyombo wanaomba mafuta ya kupakaa wanaomba yaan ni shida ,nikasema duh hapa kazi ipo kama ndiyo hivyo hapa inabidi kuwa kauzu sasa hivi.
 
Na wewe tafuta vitu unavyo hisi hana ili skikunyima kiwe chanzo cha wewe kumnyima.
Ila uchoyo uache siyo mzuri unanyima jirani mia tano?
weee kwanza nimeogopa unakumbuka enzi zile tukiona shilingi tano njian tunaambiwa tusiokote watu watakuwa wameifanyia mambo
 
Sioni ubaya wowote kama unacho mpatie tu na sio kumsaidia mtu mpka umtangazie huo msaada hauna maana

Na vile vile Kama hutaki kuombwa unamwambia tu
Maisha sio complicated kiasi hicho ushindwe kufanya maamuzi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
kusaidiana kupo sikatai hata mimi huwa ninasaidiwa ila kuna namna zake
 
Hellow JF

Jirani ni mtu muhimu sana kwenye makazi kwa sababu yeye ndiye mtu wa kwanza kukusaidia pale unapopatwa na shida na unahutaji msaada ,ujirani ni muhimu sana kwa binadamu yoyote yule.

Huyu jirani yangu sijui ananijaribu kwa sababu anamtuma sana mwanaye kuja kuomba hapa home kuomba sio kosa kila mtu anahitaji msaada lakini huyu sijamuelewa.

Picha linaanza ikawa inaletwa simu kuchajiwa na kumbuka hapa sisi tumehamia hivi karibuni tu sio wenyeji kabisa kuna siku umeme wetu wa magumashi huu walikata tukawa kwenye Giza siku 2 hamna umeme dogo akatumwa alete simu mama kasema nilite simu ikae tu umeme ukija umchajie,baadaye akaja tena mama kanituma kama una sukari kidogo anaomba.

Siku nyingine akaja mama anaomba kitunguu kimoja kama unacho umpatie.
Jana sasa ndo kali akaja usiku mida ya saa moja hivi mama kasema anaomba umkopeshe mia tano nikamuuliza tena shilingi ngapi amekwambia akasema shilingi mia tano umkopeshe.Aisee Mungu anisamehe tu nikamwambia sina.

Halafu hapo anavuka nyumba kama 3 ndiyo inakuja nyumba ninayo kaa sasa wakat wa story na jiran mwingine akaniambia yaan hiyo nyumba ya chini hapo wakishakuzoea wanaomba hadi kero sabuni ya kuogea wanaomba sabuni ya kuoshea vyombo wanaomba mafuta ya kupakaa wanaomba yaan ni shida ,nikasema duh hapa kazi ipo kama ndiyo hivyo hapa inabidi kuwa kauzu sasa hivi.
Take it in positive ways..
 
Back
Top Bottom