Jipu ukaguzi wa magari UK

Jipu ukaguzi wa magari UK

Hili la kukagua Magari yanayotoka UK ni ulaji aliyopewa Lukosi wakishirikiana kula pesa bila jasho. Magari ya UK uwafanyiwa ukaguzi kila mwaka na huwezi kuliingiza gari lako barabarani kama halina cheti ya ukaguzi. Ukipatikana gari lako laweza kusagwa na wewe unachukuliwa point tatu au sita kwenye leseni yako pamoja na faini isiyozidi pound 500.

Ivyo siyo rahisi kwa mtanzania ambaye yupo UK akatuma gari ambayo haina MOT. Hili la ukaguzi ingewekwa uko nyumbani mfano unapoenda kulipia kodi zako wakati wa kutoa gari uonyeshe MOT yako. Siyo lazima MOT itoke kwa Lukosi kwani hapa UK sehemu pa kuangalia MOT ni karibu kila mtaa utawapata na wanatambulika kihali na serikali ya UK.

Usipoonyesha MOT wakati wa kutoa gari lako Dar ndio upigwe faini kali kwasababu itakuwa ni uzembe wako kuliko sasa unaambiwa ukitaka kutuma gari Tanzania lazima upeleke gari kwa Lukosi hata kama unakaa miles 100 ndio akupe MOT wakati yapo magarage kibao hadi mlangoni kwako.

Kwa kifupi MOT aliyopewa atoe Lukosi ni deal ya baadhi ya wakubwa uko Tanzania wanakula pesa pamoja. MOT hapa UK ni pound 30 hadi £45 lakini Lukosi na vibosile wake wanachaji pound 150. Inatuwia vigumu mfano unakaa Moshi inabidi uendeshe gari hadi Dar ndio ukapate MOT ya Lukosi Wakati hapo Moshi wa kuweza kukupatia MOT wapo zaidi ya 300.

Angalia tunavyonyanyaswa kwa ukiritimba za bongo bado wanaleta hadi huku. Hapa UK hakuna ujanja wa kusema kuwa utafanya kwenye MOT kwasababu gari lako likipata ajali ikaonekana ulicheza na MOT mwenye garage aliyetoa kibali inakula kwake pamoja na wewe.
Mbaya zaidi kituo cha Ukaguzi ni kimoja tu
 
Hili ndio deal lililomtoa lukosi chadema.aliaidiwa atapewa ulaji
 
Hilo kweli ni tatizo kubwa. Inaniuma sana sababu cos nimeagiza gari toka UK, natakiwa niwalipe Serengeti £150 kwa ukaguzi wao wakati limekaguliwa na wataalamu Kwa £50.
Huyo aliyewapa Serengeti tenda ya kukagua magari ya UK yanayoingia nchini ni nani? Bila shaka hiyo extra 100£ wanagawana wote
 
Hapa kuna chembe chembe za rushwa yaani unatembea masaa manane njiani kwenda kupeleka gari likakaguliwe ukifika huko hawafanyi Ukaguzi wowote, unalipia pesa then unapewa sticker, halafu unarudi kwenu mwendo wa masaa manane tena. Tunacholalamikia siyo tu hizo Pound 150 zinazolipwa bila sababu bali pia hata mafuta yetu kwenda na kurudi umbali mrefu kufuata huduma ya Ukaguzi
Kwa hiyo jamaa ana ukiritimba yaani monopoly ya hiyo shughuli? Mlioko huko si muombe kuifanya hiyo shughuli ili kuwe na ushindani? Niliona jana PM kaongea na watu wa huko hamkuwasilisha hii kero?
 
Hii kampun n miongon mwa zile zilizobebwa na ule utawala uliopita. Huo n wiz mkubwa ukiangalia fee za ukaguz WA magar kwenye makampun meng sio kubwa hivyo. Jipu Hilo watumbuliwe tu
 
Huyo aliyewapa Serengeti tenda ya kukagua magari ya UK yanayoingia nchini ni nani? Bila shaka hiyo extra 100£ wanagawana wote

hahaha! sio 100 tu, ni yote. kwa sababu hamna wanachofanya zaidi ya kubandika stika!
 
TBS ni Jipu Mkurugenzi wake ni Nani kwanza? Nasikia eti hana Taaluma ya kumfanya aongoze Shirika Nasikia Toka Enzi za Mwalimu Shirika huongozwa na mwanasayans au Engineer lakini kwa Ubabe Taratibu zikabadilishwa enzi za JK
 
Hii kampun n miongon mwa zile zilizobebwa na ule utawala uliopita. Huo n wiz mkubwa ukiangalia fee za ukaguz WA magar kwenye makampun meng sio kubwa hivyo. Jipu Hilo watumbuliwe tu
Huku kubebana kwao ni chanzo cha unyonyaji na umasikini wa taifa letu. Hatuwezi kukubali
 
TBS ni Jipu Mkurugenzi wake ni Nani kwanza? Nasikia eti hana Taaluma ya kumfanya aongoze Shirika Nasikia Toka Enzi za Mwalimu Shirika huongozwa na mwanasayans au Engineer lakini kwa Ubabe Taratibu zikabadilishwa enzi za JK
Hizi nafasi za uteuzi naomba ziangaliwe upya, kuteuana kwa kudumisha urafiki na ujirani ndo kunatufikisha hapa tulipo. Maslahi ya taifa lazima yawekwe mbele
 
Ukweli huu ni mradi wa watu wachache pale Dar na ikichunguzwa kwa karibu utakuta kuna watu wa ubalozi wanausika kwenye hili kwani ili jibu aliwezekani limeota huku UK wakati tunawatu wa ubalozi wapo.
Nakubaliana na wewe, hakuna ufisadi mkubwa unaofanywa na mtu mmoja. Lazima tuchimbue mnyororo wake wote
 
Pauni 150 ni wizi, kwanza nchi zilizoendelea ikiwemo Uingereza, wanakagua magari yanauzwa, yanayotumika barabarani na yanayosafirishwa, tena alafu ukaguzi mwingine kwa Pauni 150, yani wakina Lukosi wana utaalamu kuliko wataalamu wa serikali ya Uingereza. Hili litakuwa dili, TBS ni Jipu. Sio kwa hili tu, kuna madudu mengi TBS
 
Uwii, acheni mkataba wake uishe jamani, huyu Lukosi ameisitea sana hiyo Tender, kumbukeni hiyo Tender ilikuwa chini ya WTM ambayo inamilikiwa na Wilson. Pakatokea figisu figisu WTM ikanyang'anywa leseni.

Sasa mkileta figisu figisu tena Serengeti Global itanyang'anywa leseni , na Kisaikolojia itamuathiri sana Lukosi ambaye aliamini kama Tender hii ingemuondoa kwenye umasikini, Kumbukeni ametumia zaidi ya Pound £100,000 katika mchakato wa kutafuta tenda hiyo kiasi kwamba ikabidi Serengeti freight ifungwe kutokana na madeni makubwa pesa ambayo alipewa kama mtaji kutoka kampuni za usafirishaji za Kenya.

Kama mna mapenzi ya kweli na ndugu yenu Chris Lukosi tafadhali msameeni hadi tenda iishe, au amalipe kulipa deni la Range Rover.
 
Hapa kuna chembe chembe za rushwa yaani unatembea masaa manane njiani kwenda kupeleka gari likakaguliwe ukifika huko hawafanyi Ukaguzi wowote, unalipia pesa then unapewa sticker, halafu unarudi kwenu mwendo wa masaa manane tena. Tunacholalamikia siyo tu hizo Pound 150 zinazolipwa bila sababu bali pia hata mafuta yetu kwenda na kurudi umbali mrefu kufuata huduma ya Ukaguzi
Niliposoma wadau halo juu gharama pound 150 out call nikaona ni fair kwa sababu UK kuna gharama za kumtoa mtu ofisini kwake ingawa MOT kufanya nje ya garage sijui wanafanyaje!!

Kumbe hata ikiwafuata bado bei ni ile ile pound 150 ambayo ni karibia 4 times ya gharama za garage nyingine!!

Hana bahati Magufuli hapendi kusafiri la sivyo kwenye mkutano wa uliopita ingekuwa "nitumbue ni si tumbue".
 
Pauni 150 ni wizi, kwanza nchi zilizoendelea ikiwemo Uingereza, wanakuawa magari yanauzwa, yanayotumika na yanayosaforishwa, tena alafu ukahuxi mwingine kwa Pauni 150, yani wakima Lukosi wana utaalamu kuliko wataalamu wa serikali ya Uingereza. Hili litakuwa dili, TBS ni Jipu. Sio kwa hili tu, kuna madudu mengi TBS
Hivi justification ya TBS kukataa kutambua MOT za garage ngyingine za UK ni ipi?
 
Back
Top Bottom