Jipu ukaguzi wa magari UK

Jipu ukaguzi wa magari UK

Hii issue ni kama repeat ya kilichotokea hapo awali, kwa kumbu kumbu zangu, Tender hii hapo awali ilipatiwa kampuni ya WTM.

Ilifikia step ya kumuandikia rais mstaafu barua ya wazi na kumpa vielelezo vyote vya ubatili na wizi wa uwazi kabisa uliofanywa kipindi hicho.

Kuwakumbushua pitieni hizi article na blog muhimu iliyopelekea kuhojiwa bungeni juu ya huu wizi na hatma yake kufutwa kwa tender baina ya WTM na tbs.

Fast foward Yale Yale !

Tanzanian Netizens

THE REAL DEAL
 
Wakati sukari iliwekewa bei elekezi ya shs 1800/- wale waliopandisha bei mpaka 3000/- au kufungia godown tons of sugar serikali imefanya nini kama upo makini?

Sasa bei elekezi ya ukaguzi wa magari imeainishwa na serikali ya wakoloni $35 huko ugaibuni alafu wewe unakuja na bei ya nyumbani kwako na mkeo ya $150 unataka raia afanyeje?

Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
 
Hili la kukagua Magari yanayotoka UK ni ulaji aliyopewa Lukosi wakishirikiana kula pesa bila jasho. Magari ya UK uwafanyiwa ukaguzi kila mwaka na huwezi kuliingiza gari lako barabarani kama halina cheti ya ukaguzi. Ukipatikana gari lako laweza kusagwa na wewe unachukuliwa point tatu au sita kwenye leseni yako pamoja na faini isiyozidi pound 500.

Ivyo siyo rahisi kwa mtanzania ambaye yupo UK akatuma gari ambayo haina MOT. Hili la ukaguzi ingewekwa uko nyumbani mfano unapoenda kulipia kodi zako wakati wa kutoa gari uonyeshe MOT yako. Siyo lazima MOT itoke kwa Lukosi kwani hapa UK sehemu pa kuangalia MOT ni karibu kila mtaa utawapata na wanatambulika kihali na serikali ya UK.

Usipoonyesha MOT wakati wa kutoa gari lako Dar ndio upigwe faini kali kwasababu itakuwa ni uzembe wako kuliko sasa unaambiwa ukitaka kutuma gari Tanzania lazima upeleke gari kwa Lukosi hata kama unakaa miles 100 ndio akupe MOT wakati yapo magarage kibao hadi mlangoni kwako.

Kwa kifupi MOT aliyopewa atoe Lukosi ni deal ya baadhi ya wakubwa uko Tanzania wanakula pesa pamoja. MOT hapa UK ni pound 30 hadi £45 lakini Lukosi na vibosile wake wanachaji pound 150. Inatuwia vigumu mfano unakaa Moshi inabidi uendeshe gari hadi Dar ndio ukapate MOT ya Lukosi Wakati hapo Moshi wa kuweza kukupatia MOT wapo zaidi ya 300.

Angalia tunavyonyanyaswa kwa ukiritimba za bongo bado wanaleta hadi huku. Hapa UK hakuna ujanja wa kusema kuwa utafanya kwenye MOT kwasababu gari lako likipata ajali ikaonekana ulicheza na MOT mwenye garage aliyetoa kibali inakula kwake pamoja na wewe.
Naunga mkono hoja yako .
 
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim jipu kubwa la UK ni la ukaguzi wa magari.

Kuna upotevu mkubwa wa pesa za serikali ambapo TBS wamewapa kampuni ya ubabaishaji inajiita Serengeti Global. Kwa kawaida UK kila gari linakuwa na kibali cha MOT (Ministry Of Transport) ambacho gharama yake ni Pound 35 hadi 45 tu, na ukaguzi wa kupata kibali hiko hufanyika garage.

Cha ajabu hawa wanaojiita Serengeti Global inayomilikiwa na Bwana Lukosi wanatoza Pound 150 kitu ambacho si sahihi, gharama ni kubwa mno na wala hawana garage ya kufanyia ukaguzi wa magari. Wanakwenda nyumbani kwa mwenye gari na kufanya ukaguzi bila wataalam kasha wanabandika sticker.

Serikali ya awamu ya tano inajali sana maslahi ya Wananchi wake hususan masikini, tunaomba muushughulikie wizi huu unaoendeshwa na hii kampuni ya Serengeti Global
Mkute hyo Lucos anavyobwata huko Facebook et anatetea Chama kw kutukana watu . Utafikir mzalendo kumbe mnafiki na mwiz tu. Jipu anastahili kutumbuliwa.
 
Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
Kuwaibia watu ndo kupambana? Mwizi wacha asemwe wazi wazi
 
Back
Top Bottom