Jipu ukaguzi wa magari UK

Msal

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
218
67
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim jipu kubwa la UK ni la ukaguzi wa magari.

Kuna upotevu mkubwa wa pesa za serikali ambapo TBS wamewapa kampuni ya ubabaishaji inajiita Serengeti Global. Kwa kawaida UK kila gari linakuwa na kibali cha MOT (Ministry Of Transport) ambacho gharama yake ni Pound 35 hadi 45 tu, na ukaguzi wa kupata kibali hiko hufanyika garage.

Cha ajabu hawa wanaojiita Serengeti Global inayomilikiwa na Bwana Lukosi wanatoza Pound 150 kitu ambacho si sahihi, gharama ni kubwa mno na wala hawana garage ya kufanyia ukaguzi wa magari. Wanakwenda nyumbani kwa mwenye gari na kufanya ukaguzi bila wataalam kasha wanabandika sticker.

Serikali ya awamu ya tano inajali sana maslahi ya Wananchi wake hususan masikini, tunaomba muushughulikie wizi huu unaoendeshwa na hii kampuni ya Serengeti Global
 
Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
 
Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
Kujitoa kwa kuwaibia maskini?
Kama ni majungu mleta mada asinge hainisha utofauti wa hizo mbili. Mbona mleta mada amebainisha wazi kuwa bei halali ni Paundi 35 mpaka 45 lakini hao Serengeti wanachaji paundi 150. Huu siyo wizi wa mchana kweupe?
 
Haya sio majungu hilo ni jipu haswa tena linalohitaji kuwekewa kitunguu swaumu.. Wapi na wapi bei ya UK iwe 35 -45 pound wao waweke 150k??? Kama sio wizi ni nini hio.. Kama wameshindwa kubeba mabox warudi tubanane huku lakini sio kuwaibia wabeba mabox kirahisi rahisi hivyo!
 
Hilo kweli ni tatizo kubwa. Inaniuma sana sababu cos nimeagiza gari toka UK, natakiwa niwalipe Serengeti £150 kwa ukaguzi wao wakati limekaguliwa na wataalamu Kwa £50.
 
Na ww anzisha yako omba tenda sio kuleta fitina
Nyie watu mbona mnakuwa wa ovyo kuliko ovyo yenyewe? Mtu anaelezea jinsi watu wanavyofisadi fedha za walalahoi bila kufanya kazi yoyote wewe unamwambie nae akaibe? Ni ujinga gani huu unaandika? Watu wenyewe hawafanyi ukaguzi wowote bali wamehonga fedha wakapewa tenda ya kukusanya fedha halafu wewe unaleta ujinga wakati watu wanaumia?
 
Hili la kukagua Magari yanayotoka UK ni ulaji aliyopewa Lukosi wakishirikiana kula pesa bila jasho. Magari ya UK uwafanyiwa ukaguzi kila mwaka na huwezi kuliingiza gari lako barabarani kama halina cheti ya ukaguzi. Ukipatikana gari lako laweza kusagwa na wewe unachukuliwa point tatu au sita kwenye leseni yako pamoja na faini isiyozidi pound 500.

Ivyo siyo rahisi kwa mtanzania ambaye yupo UK akatuma gari ambayo haina MOT. Hili la ukaguzi ingewekwa uko nyumbani mfano unapoenda kulipia kodi zako wakati wa kutoa gari uonyeshe MOT yako. Siyo lazima MOT itoke kwa Lukosi kwani hapa UK sehemu pa kuangalia MOT ni karibu kila mtaa utawapata na wanatambulika kihali na serikali ya UK.

Usipoonyesha MOT wakati wa kutoa gari lako Dar ndio upigwe faini kali kwasababu itakuwa ni uzembe wako kuliko sasa unaambiwa ukitaka kutuma gari Tanzania lazima upeleke gari kwa Lukosi hata kama unakaa miles 100 ndio akupe MOT wakati yapo magarage kibao hadi mlangoni kwako.

Kwa kifupi MOT aliyopewa atoe Lukosi ni deal ya baadhi ya wakubwa uko Tanzania wanakula pesa pamoja. MOT hapa UK ni pound 30 hadi £45 lakini Lukosi na vibosile wake wanachaji pound 150. Inatuwia vigumu mfano unakaa Moshi inabidi uendeshe gari hadi Dar ndio ukapate MOT ya Lukosi Wakati hapo Moshi wa kuweza kukupatia MOT wapo zaidi ya 300.

Angalia tunavyonyanyaswa kwa ukiritimba za bongo bado wanaleta hadi huku. Hapa UK hakuna ujanja wa kusema kuwa utafanya kwenye MOT kwasababu gari lako likipata ajali ikaonekana ulicheza na MOT mwenye garage aliyetoa kibali inakula kwake pamoja na wewe.
 
Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
Bishana kwa hoja,mwenzio kaweka hoja na kaitetea kadiri anavyoweza.Wewe unaleta ulalamishi.Tuwekee hoja pingamizi kama unayo na uitetee tukuelewe,huu sio uwanja wa kulalamika.
 
Mbona hili jipu ni rahisi kulitumbua kuliko munavyofikiria. Pigeni simu HM Revenue & Excise Dept na Consumer watchdog muwape details za hawa watu wawachunguze

1. Wamekata leseni ya kufanya hiyo kazi kutoka kwa Ministry of Transport?
2. Wanao wataalamu waliokubalika kufanya hiyo kazi?
3. Hiyo kazi wanaifanya kweli?
4. Wanalipa kodi kutoka kwenye kipato chao?
5. Fee wanayo charge ni proportional na kazi yenyewe?

Wao watawachunguza kwa kuwapelekea gari bovu na kwa ujinga wao watalipasisha. Wataishia hapo. Mimi nilifikiri kusafiri ndio kusoma kumbe bado mmelala tu. Am very dissapointed. Kama hamuiwezi hiyo kazi nipeni mimi hizo details zao nikufanyieni. Uliwahi kumsikia Mandela akilalamika kwa Peter Botha alipokuwa akinyanyaswa?
 
Afadhali mmelizungumzia hii issue. Jadilini, ila mwisho wa siku mtambue Kuna wahuni na matapeli Dar wako nyuma ya hii kitu. Wanadai tena kwa kujigamba kwamba wao ndio. Wakaguzi wa Magari UK. Nina uhakika hii kitu itawaumbua watu wengi sana. Usalama wa Taifa wanalijua hili issue
 
Mbona hili jipu ni rahisi kulitumbua kuliko munavyofikiria. Pigeni simu HM Revenue & Excise Dept na Consumer watchdog muwape details za hawa watu wawachunguze

1. Wamekata leseni ya kufanya hiyo kazi kutoka kwa Ministry of Transport?
2. Wanao wataalamu waliokubalika kufanya hiyo kazi?
3. Hiyo kazi wanaifanya kweli?
4. Wanalipa kodi kutoka kwenye kipato chao?
5. Fee wanayo charge ni proportional na kazi yenyewe?

Wao watawachunguza kwa kuwapelekea gari bovu na kwa ujinga wao watalipasisha. Wataishia hapo. Mimi nilifikiri kusafiri ndio kusoma kumbe bado mmelala tu. Am very dissapointed. Kama hamuiwezi hiyo kazi nipeni mimi hizo details zao nikufanyieni. Uliwahi kumsikia Mandela akilalamika kwa Peter Botha alipokuwa akinyanyaswa?

Je Hicho kiwango wanachotoza ni Halali? Lukosi nadhani unaipata?
 
MOT inafanywa garage ambayo imeunganishwa kimtandao na serikali, wanapokagua kwa mwaka kama kuna dosari unarekebisha ili upate cheti.

Kudai hela na cheti unacho ni kero ila wanapiga hela kwenye malori wakati mengi huwa MOT imeisha hapo inakulazimu ulipe tu lakini bila ukaguzi wowote.
 
Back
Top Bottom