Jipu la utapeli Chuo Kikuu Dar (UDSM)


Umenifanya nikushangae sana kwa fikra zako zilivyo.
 
Hizi za mwisho na za nani sasa?
 
Nimekupenda bure kwa kuwa transparent kiasi hiki mpo wachache, wahusika wataona na naamini uzi utaleta mapinduzi BICO.
Umri wetu hauturuhusu kufanya kazi hizo kwa sasa na wala hatufikirii hilo la ukuu wa wilaya.

Tumeamua kuwekeza nje ya mji kazi ambazo tunaweza kusimamia lakini kama uonavyo, wasomi wanatuangusha.
 
Na kama ngekamatwa akaulizwa risiti ya mashine zake angafanyaje?
 
Dada Zainab,hongera sana kwa uzalendo wako na mumeo na pole kwa usumbufu.
Kusema kweli ufisadi wa pale UDSM ni mkubwa kuliko tunavyofikiri,na si idara moja ya BICO tu,kila mahali pamejaaa ufisadi mpaka basi.
Kuna tenda ya kuendesha UDASA nilikuwa nafuatilia,niliyokutana nayo ni balaa.
Kama kutakuwa na tume huru ama chombo kinachotaka kujua matatizo ya pale UDSM,nipo tayari kushirikiana nacho/nao kwani mimi ni mdau mkubwa sana pale kwa miaka mingi tu.
 

Nimeipenda sana signature yako.
 
Sasa ipi ilikuwa bora kwako ni risiti au machine?wewe ungemalizana nao na ukachukua ulichotaka ungepungua nini?au una uchungu sana na pesa zisizokuhusu?
 
Hili si tukio la kwanza kusikia kuhusu hawa jamaa wa chuo. Kuna rafiki yangu alitaka atengenezewe mashine ya juice ya miwa walimsumbua kinoma ilifika karibu miezi mitatu. Ikabd mshkaji aende na polisi ndo wakaandikishiana baada ya siku 5 aje kuchukua mashine.
Ila kikweli pamoja na usumbufu jamaa wanaijua kazi yao. Mashine za ukweli
 
Sasa ipi ilikuwa bora kwako ni risiti au machine?wewe ungemalizana nao na ukachukua ulichotaka ungepungua nini?au una uchungu sana na pesa zisizokuhusu?

Kijana, mashine za thamani ya shillingi million mbili laki saba zitengenezwe ndani ya chuo kikuu, kwa mashine za chuo kikuu, kwa muda wa chuo kikuu, na wataalam wa chuo kikuu halafu zitoke bila idhini, kiwizi-wizi apewe bila risiti, huoni kuwa ni tatizo hilo?
 
Nimesoma nimeelewa na nakupongeza kwa ujasiri wako. Mambo kama haya yanaoaswa kukemewa kwa nguvu zote ili huu utapeli uishe.
 
Waaache kuzungusha watu na watapata wateja wa kutosha. Kuwasumbua watu kunashusha hata hadhi ya watengenezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…