Jipu la utapeli Chuo Kikuu Dar (UDSM)

Zainab Tamim

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,293
583
Nimeamua kwa roho safi kabisa kuliweka hili hapa JF kwani sielewi pengine pa kulipeleka.

Napenda ieleweke kuwa mimi ni muhanga wa hili tukio na kwa kuwa nilihusika na mume wangu, nimemuomba aelezee yeye kisa hiki, ingawa amenisihi kuwa "achana nao" lakini nimeona kuwa si vyema kuliacha tu kwani leo yametukuta sisi na tumeshaingia hasara ya muda, kuna wengine wengi na pia kuna mali nyingi za Watanzania zinatumika bila huruma kwa faida ya wachache na isitoshe na linaloniuma zaidi, huwa ninajiuliza "ikiwa waalim wa chuo kikuu ni namna hii, hao wanafunzi wanaowazalisha hapo wakoje?" Endelea:

Ntajaribu kukifupisha hiki kisa kadiri iwezekenavyo:

Tulikuwa tumeamua kuanzisha mradi wa kufyatua matofali huko Kibaha. Katika kutafuta sehemu za kutengeneza mashine za matofali za "vibrating block machines", nikaelekezwa sehemu moja iliopo hapo Sinza, pembeni na kituo cha mafuta cha BIG BON, nyuma ya kontena wanalouza burgers. Tulipofika hapo tukakuta kweli wanaunda unda mashine lakini kulikuwa hakuna mashine za matofali na waliopo hapo wakatupa namba ya muhusika (Anaitwa Makurunge namba zake ni 0719371874) wakatueleza kuwa hayupo ametoka kwa wakati huo. Tukampigia simu, baada ya kumueleza mashine tuzitakazo huyu ndugu Makurunge akasema yeye kweli anatengeneza hizo lakini kwa sasa hana nafasi ana kazi za watu nyingi, tukamuelewa na kumuomba atuelekeze kama kuna sehemu nyingine anajua tunapoweza kutengenezesha hiyo mashine. Huyu ndugu akatueleza kuwa pale Chuo Kikuu upande wa engineering huwa wanatengeneza hizi mashine na kuna Mwalimu anamjua, tukaomba namba za huyo Mwalimu ili atuelekeze zaidi na akatupatia namba za Ndugu Cosmas Wadelanga 0786424007.

Mume wangu akampigia ndugu Wadelanga na Wadelanga akamwambia kuwa ni kweli hapo chuoni wanatengeneza hizo mashine na tukamuomba atuelekeze vipi tufike na kuonana nae kwani tulikuwa tunataka hiyo mashine kwa haraka. Akatuambia kwa sasa yupo nje ya chuo na atatupigia akifika, akatuuliza kwani "mpo wapi kwa sasa?" tukamueleza kuwa sisi tupo Sinza si mbali na chuo na muda wowote akifika tutakwenda. Baada ya muda akapiga simu kusema kuwa hayupo mbali na Sinza na anaweza kuja kusikiliza mahitaji yetu, basi wakaagana na mume wngu wakutane hapo "Loliondo Sinza. Mume wangu akaenda kuonana nae na mume wangu akamwambia anataka kuona samples za mashine na Ndugu Wadelanga akaagana nae siku ya pili asubuhi tarehe 5/12/2015 wakutane hapo Loliondo ili waende chuo kikuu. Siku ya pili asubuhi takafatana wote na kwenda chuo kikuu tukapelekwa kwenye karakana na tukaoneshwa vifaa vingi tu vinavyotengenezwa hapo na tukaridhika na "quality" ya hivyo vifaa na tukapelekwa ofisini (hapo hapo ndani ya karakana za BICO).

Tukapatana bei na kukubaliana kuwa tutatengenezesha mashine mbili, moja ya umeme (vibrating block machine) na moja ya manual, ili kama tumeshachanganya udongo wa matofali na umeme umekatika ghafla basi usiharibike na tutengeneze tofali kwa hiyo mashine ya manual (si ya umeme) ili tusipate hasara.

Bei tulizokubalina ni mashine ya umeme kwa Shillingi Million mbili laki tatu na mshine isio ya umeme ni shillingi laki 4 na tukakubaliana tulipe advansi ya shillingi 1,700,000/= na million moja inayobaki wakimaliza kazi. Na tukakubaliana kuwa watatupatia mashine ya manual baada ya wiki moja na mashine ya umeme baada ya wiki mbili. Tukalipa advansi na tukapewa na invoice ya BICO (original iliyoandikwa kwa mkono ninayo mpaka leo). Mimi ndio nililipa pesa nikauliza risiti, huyu ndugu Wadelanga akasema risiti mkimalizia pesa zzote kwa sasa lipeni kwa hii invoice. Hatukutilia shaka kwani tupo chuo kikuu ndani ya karakana zao.

Ikapita wiki tukaenda kufata mashine zetu tukakuta bado, tukalalamika kidogo ndugu Wadelanga akatuwacha na kijana mmoja (jina simjui) wa hapo karakana kuwa huyu ndie anashughulikia na yeye ana kazi za kufundisha kwa muda huo, yule kijana akasema tumpe siku tatu ile ya manual itakuwa tayari na wiki mbili ile ya umeme itakuwa tayari, tukaenda tukaikuta kweli ipo tayari lakini haijakauka rangi na kuna kitu kidogo walikuwa hawajakiweka tukakubaliana wakiweke ili twende siku ya pili tukachukuwe. Kwenda siku ya pili hatukumkuta Wadelanga wala huyo kijana. Tukauliza nani mkubwa wa karakana tukapelekwa ofisi ya Dada mmoja anaitwa Alida ambae hatukumkuta lakini tukapewa namba zake 0754665913.

Mume wangu akampigia Dada Alida na kumuelezea kuwa yeye anatoka mbali shamba na kuahidiwa kuwa mashine tayari na kuzikuta bado inamgharimu muda na pesa za mafuta, yule akamjibu kuwa atafatilia na atamjibu, hakumpa jibu lolote baada ya hapo.

Ikawa kila siku mume wangu anampigia Wadelanga kujua kama mashine tayari na Wadelanga akamwambia subiri uchukuwe zote kwani na ile ya umeme bado kidogo tu. Baada ya siku kadhaa tarehe 31-12-2015 ndugu Wadelanga akampigia mume wangu na kumwambia "mashine tayari lakini tumepata tabu kweli kuzitoa" mume wangu akamuuliza kwanini mpate taabu kuzitoa na vitu ni vya halali mngenambia ningekuja tu kuvichukua si mtengeneze "gate pass" tu? Ndugu Wadelanga akamjibu, "mambo siku hizi magumu" Mume wangu akanieleza alichoongea na ndugu Wadelanga nikamwambia mueleze kuwa wewe unanunua mashine kihalali kwa hiyo asikuletee hayo mambo ya "mambo magumu". Mume wangu akamtumia sms inayosomeka hivi: "hizo mashine tulilipia advance ya 1.7m ofisini chuo kikuu, risiti nnayo na zimebaki 1m ambazo ninashangaa unataka nilipie mitaani. Mimi sitaki mambo ya mitaani nataka nilipie kihalali kule kule nilipofika nikalipia advance".

Ndugu Wadelanga hakujibu hiyo sms akapiga simu na kumwambia "njoo utapata risiti zako na usiwe na shaka tumewahi kuzitoa ili tuokoe muda tuliokuchelewesha na sikukuu zinaanza itabidi uzingoje mpaka tarehe 5 Januari, njoo Sinza pale walipokuelekeza kwangu utazikuta na risiti tutakupa".

Mume wangu aliponieleza hayo nikamwambia nenda lakini kama hawajakupa risiti za BICO usichukuwe hizo mashine.

Na kweli ikawa hivyo, alipoenda alizikuta mashine lakini hawana risiti za BICO na wakadai wapewe ile invoice ya BICO waliyotoa, mume wangu akawaambai kama hamna risiti za BICO hizo mashine sizilipii na sikukuu zikisha ntakwenda chuo kikuu kudai mashine zangu. Wakamwabia "nenda utakako" na hizi mashine kama hutaki sisi tunaziuza ukienda chuo kikuu sana sana tutakurudishia pesa zako, hauna cha kutufanya.

Mumewangu akaondka hapo na huyu Wadelanga akaanza kumpigia simu mara kwa mara mimi nikamwambia usimjibu, huyo anatafuta matatizo.

Basi Jumatatu iliopita tukaenda chuo kikuu kwa yule Dada Alida ambae tulielekezwa kwanza nae akamkaribisha mume wangu ofisini na kwa kuwa ofisi ni ndogo na milango haijafungwa mimi nikawa nasikia maongezi yao yote.

Yule dada alichosema ni kuwa hiyo kazi si ya chuo kikuu kwani haikupitia kwake na akawa anauliza mara mbili mbili "hizo mashine ziko wapi, unazo wewe kwa sasa", licha ya mume wangu kumueleza kuwa hajachukua hizo mashine alizikataa na ndio sababu ya kwenda kumuona yeye. Yule akamuita Wadelanga, akamwambia Wadelanga kama anamjuwa mume wangu na yule Wadelanga akasema "nnamjuwa" akamwambia ana malalamiko yake, Wadelanga akasema huyu mzee ni mkorofi tulipatana kazi mitaani sasa amezikataa mashine, mimi pesa zake nnazo hizi hapa achukuwe", Mume wangu akauliza mitaani mnatoa invoice za BICO? Yule Dada akaingilia kati na kusema kama anakurudishia pesa zako "wewe chukuwa tu yaishe". Mume wangu akachukuwa pesa zake na kuondoka.

Cha kushangaza, Dada Alida hakuwa na wasiwasi na Wadelanga wala hakuwa na wasi wasi kuwa katumia invoice za BICO.

Nikaona ingawa wale wamefanya kila njia tuchukuwe pesa zetu haraka ili yaishe, lakini cha kushangaza, ni vipi chuo kikuu kitumiwe na watu kama hawa kutapeli? Ni mali ngapi na muda upi wa kazi uliopotezwa kutengeneza hizo mashine kisha zikatolewa kinyemela?

Sisi wameshatupotezea mwezi mzima na ni wawekezaji wadogo, mwisho wa siku walipoona "dili" lao limeingia mchanga wakaona tukose wote.

Rais Magufuli alisema wawekezaji wasicheleweshwe, ingawa ni kwa kiwango kidogo lakini nasi pia tulikuwa tunawekeza kihalali, tunaomba wahusika waelewe hilo.

Tunaomba wahusika walishughulikie hilo jipu la pale BICO chuo kikuu na mume wangu yupo tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ili kukomesha hii tabia mbaya kwenye chuo chetu kikuu, namba zake ni 0756803528.

Nawasilisha.
 
Last edited:
Zainab asante kwa kuwa mzalendo wa kweli, ikiwa tutaendesha mambo yetu kwa kufuata uhalali namna hii naamini tutafika mbali ndani ya muda mfupi.

JPM ameona na bahati nzuri namba za Mumeo zipo! Si haba uteuzi wa Wakuu wa wilaya anaweza kuwemo.
 
Kila kitu ni dili hapa Tanzania. Hata degree unaweza kuipata kwa dili pale Mlimani. Awamu ya nne imeharbu hii nchi xana.

Inasikitisha na kushangaza sana mahala pa mwisho ambapo tunapategemea kuwa kuna wasomi na wao ndio watatatua matatizo yetu kuliko mitaani, tunakwenda huko kutatuliwa yetu tunakuta kuna utapeli kuliko mitaani.

Sisi tumepotezewa muda na Rais Magufuli alisema wanaowekeza wasipotezewe muda. Fikiri ni hasara ngapi tumepata kupitia hawa wapuuzi wachache waliowekwa pale chuo kikuu ukizingatia kuwa vi mtaji vyetu ni vya hali ya chini.

Tena mpaka mume wangu alimueleza dada Alida kuwa tumeuza gari kuanzisha huu mradi lakini inaonekana hakuwa na wakati wa kuelewa.
 
Last edited:
Dada pole sana! Ila iko hivi the beautiful one are not yet born..! Magufuri na ssm wote ni kijani tu kelele za majipu sijui vidonda upele ni sababu anataka mhula mwingine 2020.
 
inawezekana hata ile mitungi ya pale BICO na yenyewe huwa ya dili,isije ikalipukia wateja
 
Inasikitisha na kushangaza sana mahala pamwisho ambapo tunapategemea kuwa kuna wasomi na wao ndio watatua matatizo yetu kuliko mitaani, tunakwenda huko kutatuliwa yetu tunakuta kuna utapeli kuliko mitaani.

Sisi tumepotezewaa muda na Rais Magufuli alisema wanaowekeza wasipotezewe muda. Fikiri ni hasara ngapi tumepata kupitia hawa wapuuzi wachache waliowekwa pale chuo kikuu ukizingaia kuwa vi mtaji vyetu ni vya hali ya chini.

Tena mpaka mume wangu alimueleza dada Alida kuwa tumeuza gari kuanzishaa huu mradi lakini inaonekana hakuwa na wakati wa kuelewa.

Ni jambo la kusikitisha xana. Ila hongera kwa uzalendo uliounyesha kwa kuamua kufuata uhalali ktk mambo yako. Heri watz wengi wangekuwa km ww hz dili za kimagumashi zingeisha. Na heri umestuka mapema maana ungekuta unauziwa mashine bomu. Hawa jamaa wamelelewa xana. Kilq sehemu pameoza. Vyuoni kumeoza!! Yaani kila idara ya serikali imeoza. Na huo mradi unakuta ni wa mtu binafsi wakati karakana za chuo. Yaani hii chi ni tabu tupu. Ila pole kwa usumbufu ulioupata.
 
Zainab asante kwa kuwa mzalendo wa kweli, ikiwa tutaendesha mambo yetu kwa kufuata uhalali namna hii naamini tutafika mbali ndani ya muda mfupi.

JPM ameona na bahati nzuri namba za Mumeo zipo! Si haba uteuzi wa Wakuu wa wilaya anaweza kuwemo.

Umri wetu hauturuhusu kufanya kazi hizo kwa sasa na wala hatufikirii hilo la ukuu wa wilaya.

Tumeamua kuwekeza nje ya mji kazi ambazo tunaweza kusimamia lakini kama uonavyo, wasomi wanatuangusha.
 
Hongera sana dada Zainab kwa UZALENDO. Pongezi kubwa pia kwa kuweka mambo bayana ili hao wadhalimu washughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Wenye mamlaka huwa wanapita humu natumaini wataliona hili. Usisahahu kutuletea mrejesho kwa yatakayojiri kwa hao Wahujumu UCHUMI.
 
Unakomaa na risiti ili iweje? kwamba ww ni mtakatifu sana?? au unataka umaarufu wa kitoto humu?

Mimi nilijua umetapeliwa ela zako kumbe Mashine tayari, ila unataka haki?
Kwa taarifa yako hakuna haki duniani, hapa ni unyama unyama tu.
Msilete hoja za kuchafuana humu
 
Unakomaa na risiti ili iweje? kwamba ww ni mtakatifu sana?? au unataka umaarufu wa kitoto humu?

Mimi nilijua umetapeliwa ela zako kumbe Mashine tayari, ila unataka haki?
Kwa taarifa yako hakuna haki duniani, hapa ni unyama unyama tu.
Msilete hoja za kuchafuana humu
Uko sahihi kama ''id'' yako inavyoonyesha
 
kisa kinasikitisha sana. poleni watanzania wenzangu. sijui uhusiano wa hiyo BICO na udsm, ila kwa vyovyote vile iwavyo ni kitendo cha kipuuzi sana walichokifanya (kama ni kweli iko kama ilivyo). Tunaziomba mamlaka zinazohusika zifatilie jambo hili haraka maana ukiona hivyo ujue wengi wameshalizwa kwa utapeli wa namna hiyo na wanazidi kupaka matope udsm
 
kisa kinasikitisha sana. poleni watanzania wenzangu. sijui uhusiano wa hiyo BICO na udsm, ila kwa vyovyote vile iwavyo ni kitendo cha kipuuzi sana walichokifanya (kama ni kweli iko kama ilivyo). Tunaziomba mamlaka zinazohusika zifatilie jambo hili haraka maana ukiona hivyo ujue wengi wameshalizwa kwa utapeli wa namna hiyo na wanazidi kupaka matope udsm

Kisa ni kama kilivyo naimejaribu sana kufupisha kejeli na mabishano yalioendelea baada ya kuzikataa hizo mashine bila risiti.
 
Back
Top Bottom