Jinsi ya kuweka subtitle kwenye movie yeyote ile

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
801
2,121
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza. Najua kuna watu wengi ni wapenzi wa muvi za hollywood na bollywood humu jamvin, pia naelewa kuwa kuna watu wanapenda subtittles ili kuelewa na kufurahia movie zaidi hasa zile za kihindi ambazo hazina subtittle na wanaongea kihindi tupu. Ni rahisi sana, cha muhimu ni kuwa na VLC media player tu. Kama unayo then fata step zifuatazo
  1. Fungua www.subscene.com then tafuta subtitle ya movies unayoitaka kisha idownload. ANGALIZO: Download subtitles inayoendana na format ya muvi uliyokuwa nayo.. mfano wa format za movies ni kama vile.. DVDrip... avi... xvdi... BRrip. Blueray etc.. so unapo download subtitle hakikisha znaendana na format ya muvi uliyokuwa nayo
  2. Baada ya kudownload li copy na u paste sehemu ambapo muvie husika ipo
  3. Nenda kwenye file ulilodownload kisha bonyeza OPTION kwenye mouse ya computer yako... utaona neno "extract here"bonyeza hapo
  4. Sasa nenda kwenye muvie husika click option... rename.. then "copy"the name
  5. Sasa nenda kwenye file la subtittle click option.. rename... then "paste" the name then click OK.
  6. Sasa play muvi yako uanze kuinjoy..NOTE, Ni VLC PLAYER tu ndo itakubali.... vilevile waweza iweka kwenye flash na ukaiangalia kwenye FLAT SCREEN vzr kbs ikiwa na SUBTITLE zake.... mtanipa mrejesho
 
Dah maelezo kilo Mia mpk nimechanganyikiwa
Sikujua km kuna utalaam wa kufanya hii makitu
Ngoja nii some tena nikishindwa Kunielewa ntakuchek pm
 
Format ya muvi utaipata kwenye title ya muvi.. au nenda kwenue details za muvi husika... ukiingia kwenye subscene.com kuna subtittle kwa lugha kibao. Chagua lugha unayoitaka manake kuna wengine wanajua kiarabu kuliko kingereza humu jamvini
 
hatua ya 3 namaanisha hilo file ulilolidownload linamwonekano km wa kitabu hv.. sasa ili lifanye kazi inabd uende kwenye mouse yako ya computer. . kuna vidude 2 pale... bonyeza kile cha kulia.. utaona maneno kibao..unalotakiwa kulichagua ni lililoandikwa EXTRACT HERE..
 
km ukishindwa hz process n PM nikurushie VIDEO ndo utaelewa zaidi na kwa haraka.. nimeshindwa kuiweka humu
 
Process ndefu sana hizo simple process kwa watu wenye uelewa wowote.

Download MPC https://www.google.co.tz/url?q=https://mpc-hc.org/downloads/&sa=U&ved=0ahUKEwjvkqm_5drKAhWCuRQKHZ0gBfcQ0gIIOSgAMAg&usg=AFQjCNFcj5Q1hEAoob54U7XqbMRwLXKjvA then install baada ya hapo play movie unayotaka subtitles then press ctrl+d italeta list ya subtitles in different languages unachagua unayoitaka
Hii njia nimeielewa lkn hauwezi kuitumia kwenye flat screen ni kwa computer peke yake
 
Dah mkuu umenisaidia maaana napenda movie za kiindi sema sub ndo zilikuwa zinazingua
 
Kaka kwa mfano mi natumia simu kudownload Subtitle kisha naitoa iyo subtitle na kuipeleka kweny laptop yangu nikisha fanya hivo tu kila nikijaribu ingiza inagoma wats wrong?
 
Kaka kwa mfano mi natumia simu kudownload Subtitle kisha naitoa iyo subtitle na kuipeleka kweny laptop yangu nikisha fanya hivo tu kila nikijaribu ingiza inagoma wats wrong?
ni pm.... nikuelekeze kwa simu
 
Mm nilijaribu kwenye pc ina play vizuri lkn nikija play kwenye tv haileti subtitle.
 
Back
Top Bottom