Jinsi ya kuwaridhisha wazazi...

Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
994
Likes
8
Points
0
Me370

Me370

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
994 8 0
Haya wakuu wa jukwa embu tuongelee jambo tofauti leo. Badala ya kuamuru kesi za watu leo tufanye kitu ambacho kidogo kipo tofauti. Topic ya leo ni :-

JINSI YA KUWARIDHISHA WAZAZI

1. Waonyeshe umekuwa mkubwa
Biashara ya mambo ya kitoto mbele ya wazazi punguza na kama ikiwezekana hata utani wa kijingajinga usio na kichwa wala miguu achana nao. Fikiria kabla ya kuongea na ukumbuke hawa ni matured adults.

2. Beba Majukumu na Saidia Nyumbani Ukiweza
Una mdogo wako anasoma lipa ada, umeshindwa nunua hata madaftari na Uniform tu. Umeona mdogo wako kamaliza shule yupo nyumbani tu mlete mjini alafu msomeshe hata ka kozi ka computer. Baba au mama anajiskia vibaya tuma nauli aje atibiwe Dar na lipa hospital Bills, misaada mingi tu unaweza fanya. Usitegemee kaka au dada zako jitahidi uwe wa kwanza wewe. e.t.c

3. Muda
Tenga muda maalum wa kuwa nao, Imefika Christmass panda basi kakae nyumbani wewe na familia yako. Umepitisha wiki hujawasiliana na mama au baba mpigie simu hata kila weekend. Wafanye wajivunie kuwa wana mtoto anayewajali.

4. Timiza Ahadi na Usidanganye
Hata kama maji yapo vipi shingoni kuwa mkweli kwa wazazi wako. Jitahidi ufunguke mwanzo mwisho. Wamepitia maisha na mambo mengi wanayajua zaidi yako. Umeahidi ntakupigia baadae mama jitahidi upige hiyo simu timiza ahadi. Kuna kitu huwezi fanya wajulishe na sababu utoe sio unaweka ahadi za uongo alafu ukibanwa unazidisha uongo kama mwezi huu hatujalipwa e.t.c

5. Jitume Kwao
Saidia kazi za nyumbani sio unajitia busy na masomo wakati wote. Mama ana mzigo nenda mpokee sio mpaka uitwe. Kama mzazi anasafisha labda chumbani kwake achia unachofanya mshirikiane kwa pamoja. Unajua kupika saidia. Ukiwa na muda osha vyombo nyumbani.

6. Never Say NO
Umetumwa nyanyuka na fanya hapo hapo. Mzazi anavyokwambia kitu ukampotezea ni jambo linaloumiza sana mioyo yao. Huwa wanahisi wamedharaulika na hujihisi wanyonge kwako. Usithubutu kupuuza hata kama wapole vipi kwako. Mara nyingi huwa hawawezi kukwambia kitu ambacho wao wanajua hukiwezi. Hivyo jibu liwe ndio wakati mwingi. Mwanangu nina shida ya hela mjibu ntakutafutia sio sitaki au siwezi.

7. Wajulishe Hatua Unazopitia Zote
Umenunua kiwanja waambie wawemo kwenye furaha yako. Umemuona mchumba unataka KUMUOA mpeleke nyumbani ukamtambulishe. Umepata kazi nzuri waambie na ukihama pia wajulishe. Mke wako kashika ujauzito sema. Baki ya kwamba wazazi wengi wanafurahia sana mafanikio ya watoto wao pia Hili hujenga imani kwao kuwa unawaamini vya kutosha.

8. Rekebisha Tofauti
Umekasirishwa na mzazi ongea nae kwa upole bila kupandisha sauti. Kakuonea ana hasira muache rudi baadae mueleze kinyongo chako. Kununa au kuwaongelea vibaya kwa majirani haifai. Mfano mama amekuudhi sana na una feel comfortable kwa baba basi mueleze baba linalokukera.

9. Zawadi
Mama hana kanga nzuri jitoe kimasomao ndo ukubwa. Nunua hata ndala tu za mzazi kama zinaonyesha dalili ya kuisha. Zawadi ndogo ndogo ni silaha kubwa sana kwa wazazi maana huonyesha unawajali toka ukiwa na umri mdogo. Umeenda likizo nyumbani na watoto hakikisha unabeba chochote. Ukitaka kujua wazazi wanathamini sana zawadi ni wakati unarudi kwako lazima utafungashiwa tu chochote kile kwenye kiroba hata machungwa tu.

10. Sifa
Mmekaa wawili na mzazi toa shukrani kwake kwa kila jema alilokutendea. Msifu kwa wema wake na umwambie kwanini unajihisi una bahati kumpata yeye kama mzazi. Kumbuka wazazi wamefanya mengi sana kwako kuliko hata unayoyajua. Usichoke kushukuru na kuwamwagia sifa. Wafanye watambue kuwa wao ni mfano mzuri sana wa kuigwa na hawajakosea hata kitu kimoja katika malezi yako. Shukrani zikiambatana na vitendo kama Kumkumbatia mama au baba wakati zinatolewa huwa zinapendeza zaidi.

SOURCE:- ME370's Brain.

Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
6,864
Likes
180
Points
160
Mapi

Mapi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
6,864 180 160
kweli wazazi ni Mungu wa hapa duniani bahati na mafankio yako ipo chini ya nyayo zao
 
Public Enemy

Public Enemy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2011
Messages
2,123
Likes
573
Points
280
Public Enemy

Public Enemy

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2011
2,123 573 280
hii kitu imekaa njema mpaka nakosa maneno ya kuongeza.
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
193
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 193 145
^^
Nzuri sana, tatizo ni kuwa tunasema sana kuliko kutenda. Maneno hula vitendo.
^^
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,243
Likes
335
Points
180
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,243 335 180
Me370,

Maneno mazuri saana hii. Ingawa ka namna moja nakubaliana na Himidini ya watu kusema sana bila kutenda, ila bado inapendeza sababu inatukumbusha na kila mmoja wetu anajipima kwa nafasi yake namna anavyowajibika kwa wazazi wake.

Naomba nizungumzie hicho kipelengele cha 6. (Never say NO);

Tukumbuke wazazi wetu nao ni binadamu tu kama walivyo wengine. Pamoja na kuwa tunastahili kwa kiasi kikubwa na uvumilivu mkubwa kuwaelewa, kuwakubalia na kuwanyenyekea; ni muhimu kutambua pia tabia zao.

Kuna wazazi ukiwaendekeza ni mtihani, kuna vitu kama mtoto ni lazima uwe na msimano na use 'No' kwa baadhi ya mambo; la sivyo wengine usipoangalia inaweza kuwa kero na wakawa wanakuumiza katika baadhi ya maamuzi na hali unaweza kukataa huku ukiwaelewesha taratibu sababu zako za msingi kukataa.
 
Last edited by a moderator:
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
19,176
Likes
219
Points
160
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
19,176 219 160
Kujifunza hakuishi!!!!!!

Thanks
 
Sure dada!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Deo Corleone

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
14,920
Likes
2,914
Points
280
Deo Corleone

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2011
14,920 2,914 280
Tungekuwa tunapata mada kama hizi angalau hata mara moja kwa wiki,hili jukwaa la mmu lingekuwa jukwaa boro katika kutuimarisha katika maisha.
 
miss chagga

miss chagga

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
57,572
Likes
31,022
Points
280
miss chagga

miss chagga

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
57,572 31,022 280
nzur sana mkuu asante.
 
A

Apitakujilamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Messages
203
Likes
0
Points
33
A

Apitakujilamba

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2013
203 0 33
Me370, asante sana, umenikumbusha nipige simu home leo home baada ya kimya kingi. be blessed.
 
Last edited by a moderator:
charger

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Messages
2,322
Likes
72
Points
145
charger

charger

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2010
2,322 72 145
Dah mkuu umenichekesha kwenye hicho kipengele cha nne cha kudanganya eti mwezi huu hatujalipwa.ha ha haaa
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,712
Likes
3,377
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,712 3,377 280
Wenye wazazi someni hayo mpate kuelewa namna kuenenda na wazazi wenu, wasio na wazazi someni hayo mpate hekma ya kuishi na walezi wenu.
 
sexologist

sexologist

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Messages
2,295
Likes
48
Points
135
sexologist

sexologist

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2010
2,295 48 135
Tungekuwa tunapata mada kama hizi angalau hata mara moja kwa wiki,hili jukwaa la mmu lingekuwa jukwaa boro katika kutuimarisha katika maisha.
Naomba niamini hukudhamiria, ni typng error.. Right??
 
h120

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Messages
2,052
Likes
1,759
Points
280
h120

h120

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2012
2,052 1,759 280
Dah umenikumbusha leo nimeongea na mzee anaishi huko mkoani, baada ya salamu na kujuliana hali akaniambia ngoja nikuimbie nyimbo ya msalaba. Kesho msalaba unapita kwenye jumuiya yao, na kweli akaimba kama dk1 na nusu hv kwenye simu. Nimefurahi sana,
 
E

engmtolera

Verified Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
5,116
Likes
89
Points
145
E

engmtolera

Verified Member
Joined Oct 21, 2010
5,116 89 145
Haya wakuu wa jukwa embu tuongelee jambo tofauti leo. Badala ya kuamuru kesi za watu leo tufanye kitu ambacho kidogo kipo tofauti. Topic ya leo ni :-

JINSI YA KUWARIDHISHA WAZAZI

1. Waonyeshe umekuwa mkubwa
Biashara ya mambo ya kitoto mbele ya wazazi punguza na kama ikiwezekana hata utani wa kijingajinga usio na kichwa wala miguu achana nao. Fikiria kabla ya kuongea na ukumbuke hawa ni matured adults.

2. Beba Majukumu na Saidia Nyumbani Ukiweza
Una mdogo wako anasoma lipa ada, umeshindwa nunua hata madaftari na Uniform tu. Umeona mdogo wako kamaliza shule yupo nyumbani tu mlete mjini alafu msomeshe hata ka kozi ka computer. Baba au mama anajiskia vibaya tuma nauli aje atibiwe Dar na lipa hospital Bills, misaada mingi tu unaweza fanya. Usitegemee kaka au dada zako jitahidi uwe wa kwanza wewe. e.t.c

3. Muda
Tenga muda maalum wa kuwa nao, Imefika Christmass panda basi kakae nyumbani wewe na familia yako. Umepitisha wiki hujawasiliana na mama au baba mpigie simu hata kila weekend. Wafanye wajivunie kuwa wana mtoto anayewajali.

4. Timiza Ahadi na Usidanganye
Hata kama maji yapo vipi shingoni kuwa mkweli kwa wazazi wako. Jitahidi ufunguke mwanzo mwisho. Wamepitia maisha na mambo mengi wanayajua zaidi yako. Umeahidi ntakupigia baadae mama jitahidi upige hiyo simu timiza ahadi. Kuna kitu huwezi fanya wajulishe na sababu utoe sio unaweka ahadi za uongo alafu ukibanwa unazidisha uongo kama mwezi huu hatujalipwa e.t.c

5. Jitume Kwao
Saidia kazi za nyumbani sio unajitia busy na masomo wakati wote. Mama ana mzigo nenda mpokee sio mpaka uitwe. Kama mzazi anasafisha labda chumbani kwake achia unachofanya mshirikiane kwa pamoja. Unajua kupika saidia. Ukiwa na muda osha vyombo nyumbani.

6. Never Say NO
Umetumwa nyanyuka na fanya hapo hapo. Mzazi anavyokwambia kitu ukampotezea ni jambo linaloumiza sana mioyo yao. Huwa wanahisi wamedharaulika na hujihisi wanyonge kwako. Usithubutu kupuuza hata kama wapole vipi kwako. Mara nyingi huwa hawawezi kukwambia kitu ambacho wao wanajua hukiwezi. Hivyo jibu liwe ndio wakati mwingi. Mwanangu nina shida ya hela mjibu ntakutafutia sio sitaki au siwezi.

7. Wajulishe Hatua Unazopitia Zote
Umenunua kiwanja waambie wawemo kwenye furaha yako. Umemuona mchumba unataka KUMUOA mpeleke nyumbani ukamtambulishe. Umepata kazi nzuri waambie na ukihama pia wajulishe. Mke wako kashika ujauzito sema. Baki ya kwamba wazazi wengi wanafurahia sana mafanikio ya watoto wao pia Hili hujenga imani kwao kuwa unawaamini vya kutosha.

8. Rekebisha Tofauti
Umekasirishwa na mzazi ongea nae kwa upole bila kupandisha sauti. Kakuonea ana hasira muache rudi baadae mueleze kinyongo chako. Kununa au kuwaongelea vibaya kwa majirani haifai. Mfano mama amekuudhi sana na una feel comfortable kwa baba basi mueleze baba linalokukera.

9. Zawadi
Mama hana kanga nzuri jitoe kimasomao ndo ukubwa. Nunua hata ndala tu za mzazi kama zinaonyesha dalili ya kuisha. Zawadi ndogo ndogo ni silaha kubwa sana kwa wazazi maana huonyesha unawajali toka ukiwa na umri mdogo. Umeenda likizo nyumbani na watoto hakikisha unabeba chochote. Ukitaka kujua wazazi wanathamini sana zawadi ni wakati unarudi kwako lazima utafungashiwa tu chochote kile kwenye kiroba hata machungwa tu.

10. Sifa
Mmekaa wawili na mzazi toa shukrani kwake kwa kila jema alilokutendea. Msifu kwa wema wake na umwambie kwanini unajihisi una bahati kumpata yeye kama mzazi. Kumbuka wazazi wamefanya mengi sana kwako kuliko hata unayoyajua. Usichoke kushukuru na kuwamwagia sifa. Wafanye watambue kuwa wao ni mfano mzuri sana wa kuigwa na hawajakosea hata kitu kimoja katika malezi yako. Shukrani zikiambatana na vitendo kama Kumkumbatia mama au baba wakati zinatolewa huwa zinapendeza zaidi.

SOURCE:- ME370's Brain.

haya yatasaidia angarau,kwani hatuna cha kuwalipa hawa wazee wetu,wamefanya yao na hatuna budi kukubali kuwa bila wazazi tusingekuwepo mazingira haya
asante Mama,Mwal. Mtolera in God we trust
 
Forum statistics

Threads 1,249,419
Members 480,661
Posts 29,697,492