Jinsi ya kuwadhibiti wachawi na wanga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Ni usiku tena muda wa kupumzisha mwili na akili, wengine huita nusu kifo kwakuwa unapolala fofofo hujui kwa hakika nini kinaendelea, ni muda huu ambapo kila mmoja kwa imani yake huomba ulinzi kwa Mungu au kile anachokiamini na kukiabudu!Hata Mimi mshana jr sipo mbali na wao au na nyie au na wewe.!Lakini pamoja na sale na maombezi yetu yote ibilisi shetani haachi kutusumbua kupitia kwa mawakala wake wachawi na wanga.

Sasa haya ni mambo upaswayo kufanya kulingana na imani yako;
-Sala na maombezi kwa Mungu mkuu huku ukitumia maji ya baraka, Rosary iliyoombewa na Bible
-Au kidunia zaidi ukifanya kila kitu kwa kinyume Kama kugeuza ndani nje au nyuma mbele nguo unazolala nazo
-Au kugeuza ndala au makubazi unapotoka kwenda maliwatoni
-Au kutoka kinyumenyume mlangoni na kuingia mlango wa maliwatoni kinyumenyume
-Kulala Kichwa chini miguu juu nk nk

Wanga na wachawi ni watu wa kinyume, hutenda kinyume na hata matokeo yake huwa kinyume.Kwahiyo ukitaka kuwakomesha na kuwadhibiti nawe tenda kinyume ila fanya hivyo inapobidi

Hivi unajua ni kwanini wachawi na wanga wote waangukao safarini huwa uchi? Hii ni kwasababu ya kutenda kinyume na mazoea

Hivi unajua ndani ya ule ungo, wasafiri huangalia walikotoka na sio waendako? Kwenye kanuni za usafiri hili ni kinyume na mazoea

Hivi unajua kwanini wanga na wachawi wawapo angani safarini hawapigi story? Hii ni kinyume na mazoea Haiwezekani msafiri pamoja wengi Halafu mshindwe hata kusalimianaHivi unajua ni kwanini kwenye kusafiri ardhini hutumia fisi na angani hutumia ungo?

Bado ni mule mule. Katika hayawani wote wa Ulimwengu huu fisi anashika namba moja.Kumtumia Kama chombo cha usafiri ni kutenda tofauti na mazoea ungo kazi yake ni kupepeta nafaka unapotumika Kama chombo cha usafiri ni kukengeuka mazoea.

Lala ukijua kuna watu ni wakati wao kufanya yao wakifanya tofauti na kawaidaukisoma post hii na ukiona kuna dalili za kusumbuliwa dawa yake nawewe ni kutenda kinyume cha mazoea, kinyume cha kawaida kama wao Watakoma kukusumbua.
 
mkuu mshana, hapo kwenye kulala kichwa chini miguu juu, hapo si utakuwa unajikomoa mwenyewe au uta practice vipi zoezi hilo, all in all believe in JESUS.

Hapana kwanza hiyo ni dawa bora ya hangover, yaani miguu inakuwa kitandani Halafu vingine vinakuwa chini .....lakini hapa inabidi uwe na carpet chumbani
 
Siku ukitaka kumuua mwanga au mchawi, bila kujali yupo kwenye umbo gani Chukua kisu au panga kisha mkate nalo kule kusikokuwa na makali.. Ni ni kanuni mojawapo ya kutenda kinyume

Mkuu mshana ni wakati gani ntajua kuwa hapa kuna mchawi??.......i need to apply this method.
 
Mkuu mshana ni wakati gani ntajua kuwa hapa kuna mchawi??.......i need to apply this method.

Nitajuaje kama sasa mchawi kaingia ndan Na kama kweli kaingia naweza nifanyeje nimdhibiti

Mchawi huwezi kumuona kwa macho ya kawaida, ni mpaka ufanye mambo fulani ili akiingia tu unampa....na hata umuumizeje hataugulia pale bali atarejea kwake na kukipambazuka utapata habari
 
Back
Top Bottom