Jinsi ya kuunganisha simu kwente TV ili kuangalia mpira live

Seth seth

Member
Jan 2, 2022
95
135
Wakuu natumai mu bukheri wa afya. Niliwahi kusikia kuwa ukiwa na SMART TV unaweza kuunganisha kwenye simu yako na ukaangalia mechi za mpira wa miguu live kupitia Link mbalimbali zinazorusha mpira live online. Cha ajabu Juzi nimejaribu kuunganisha lakini picha hazikuonekana kabisa na badala yake sauti tu ya watangazaji ndo ikawa inasikika.

Nilidhani labda Mimi ndo nimeunganisha vibaya konnikaona nije kwenye jukwaa hili lenye wabobezi wa haya Mambo ili wanielekeze jinsi ya kufanya.

Kwa upande wa picha nyingine za video tofauti na mpira huwa ziaonekana vizuri tyu yaani Kama vile zinavyoonekana kwenye simu.Tatizo linakuja pale ninapounganisha football match live naambulia sauti tyu bila kuona video.
 
Sasa mkuu, ukisema smart tv peke yake haitoshi sema ni brand gan, mfano samsung au LG. kuna baadhi ya smart tv OS yake ni ya kichina ( yaani zile feki zisizo na uwezo kivile)
 
Unaweza kufanya screen casting au mirror casting. Kwa maana ya screen ya simu yako itakuwa direct kwenye screen ya TV na hapo utaweza kuangalia events za simu kwenye TV.

Angalizo tu ni kuwa binafsi nilijaribu sana, live coverage nyingi zilikubali ila mpira live nilijaribu nikashindwa.

Ingia playstore angalia apps za ku screen cast image kwenye TV.
Screenshot_2022-05-01_212049.jpg
 
Kama unatumia Tecno au itel haiwezekani
Simu lazima ina uwezo wa infrared mfano Samsung Galaxy s6 au kama ni s8 na kuendelea kuna cable unaweza kuunganisha moja kwa moja
 
Simu natumia infinix hot 8, tv ni Hisense mkuu
Infinix nyingi hazina mirrorcast maana kabla ya kudowload app za casting ni lazima simu yenyewe iwe na uwezo wa kufanya mirror casting, hapo kitu pekee unaweza kukifanya ni ku share wifi na hotspots kutumia simu kwenda kwenye Tv ili uweze kufanya live streaming.
 
hili tatizo mm pia nilipata exact kabisa kama ulivyoeleza,hapo tv haina shida tatizo lipo kwenye hiyo simu unayotumia haina huo uwezo,samsung nyingi kuanzia android 8 zinakubali,kwa simu za apple ni lazima na tv nayo iwe ya apple
 
Okyy....Asante sana kwa ushauri huo. Lakini mbona program zingine huwa zinakubali kwa kutumia simu hiyo hiyo? Au zenyewe hazihitaji mirror casting except live football streaming
 
hili tatizo mm pia nilipata exact kabisa kama ulivyoeleza,hapo tv haina shida tatizo lipo kwenye hiyo simu unayotumia haina huo uwezo,samsung nyingi kuanzia android 8 zinakubali,kwa simu za apple ni lazima na tv nayo iwe ya apple
Doooh......Asante bro kwa ushauri
 
Program zip? Kwani Tatizo ni streaming au tatizo ni connection? Na hizo zilizo connect unatumia mode gan ? Mirror cast, au hotspot.?
 
Back
Top Bottom