Jinsi ya kuua moyo wa mwanamume

Jinsi ya kuua moyo wa mwanamume

Wakuu habari ya leo. Nina imani afya zenu Ni njema kabisa. Mimi si mwanachama hai wa jukwaa hili, lakini leo nimeona nitoe mchango wangu kama njia ya kuboresha mahusiano.

Kuna tabia ambazo kwa namna moja ama nyingine zinachangia sana kuua mapenzi kati ya mke na mume. Sababu kubwa Ni kuwa ghafla mume humwona mkewe kama mgeni moyoni mwake. Baadhi ya tabia hizo zinaweza zisiwe za ajabu sana, lakini zina madhara makubwa moyoni mwa mume.

1. Kumlinganisha mumeo na mwanamume mwingine. Mfano unamwambia mbona wewe hauko kama flani? Usidhani itampa motivation. Badala yake utamfanya ajione hatoshi kuwa mwanamume. Kumbuka kuwa mumeo Ni yule yule ambaye ulimjua kabla hajakuoa. Mara nyingi tamaa ya kuolewa huhadaa ufahamu, kiasi cha kutia upofu usiweze kuona udhaifu wa mwenzi wako. Hii hupelekea watu kuoana pasipo kujua kama kweli wanafanana. Kumbuka ndoa si kufaana bali Ni kufanana. Unapomlinganisha mwanamume na mwanamume mwingine unaufunga moyo wake kwako. Moyoni atakuwa akiwaza, kwa nini basi kuolewa na mimi? Ina maana amemwona yule mwanamume kuwa bora kuliko mimi!!?

Itaendelea........

2. Kumtazama kwa dharau. Baadhi ya wanawake siku hizi wamekuwa na tabia ya kumtazama mwanamume kwa dharau, kunyonga midomo, kumtazama juu mpaka chini kwa dharau. Kitendo hiki unaufunga moyo wa mumeo. Ni kama kumwonyesha kuwa hana thamani tena kwako. Kabla hajakuoa ulikuwa mwepesi wa kuomba msamaha hata pale anapokosea! Yes, anapokosea yeye, ulimweleza kwa lugha ya upole akakukasirikia, ukamwomba akusamehe. Lakini baada ya muda akarudi kukiri kwamba ni kweli ulichomwambia. Mwishowe mshindi ukawa ni wewe mwanamke. Sasa baada ya kuolewa unataka kila unachotamka kifuatwe kwa utii. Umesahau msingi ulioujenga wakati wa uchumba. Mume anakuona kuwa mgeni kwake, si yule waliyerekebishana kwa upole, kwa nafasi. Asilimia kubwa ya wanaume hawawezi kukiri makosa moja kwa moja. Pia Pia mnapopishana mitazamo anatarajia mwanamke ajishushe, Kisha yeye atakuwa anafanyia marejeo hoja zake. Badala yake mke anamtazama mume kwa dharau, anampima chini mpaka juu. Hii inaujeruhi moyo wa mwanamume.

3. Kumwonyesha kuwa humhitaji sana kwenye maisha yako. Kabla ya kuolewa ulikuwa ukilia na kusaga meno kutaka uolewe. Baada ya kuolewa unaanza kumfanyia dharau mumeo, ukidai kwa Mfano, hukufukuzwa kwenu na kwamba asikubabaishe. Kila mkipishana kidogo tu, unajidai kumwonyesha kuwa hakuna jipya unalopata kwake. Je, Ulipata kujiuliza Kabla ya kuolewa, ni kitu gani hasa unachohitaji kwake ambacho huna? Sio kwa habari ya sex tu. Je, ni nini ambacho ungependa akupe ili ujione umekamilika kuwa mwanamke? Au ndio ndoa za fasheni? Mfanye mume wako ajione mwanamume, hakika utauteka moyo wake.

4. Kubadili mfumo wa maisha. Kabla hajakuoa ulikuwa ukivaa mavazi fulani na kujipamba kwa namna fulani. Ni kwa mwonekano huu mumeo alijikuta ametekwa bakunja! Akanasa kwenye mtego, asione mwingine zaidi yako. Sasa baada ya kuolewa, unadhani umemaliza jukumu. Ghafla ukabadili utaratibu wa kujipamba. Sasa tena hujipambi ili kumfurahisha mumeo, bali unajipambamba kuwafurahisha wanaokutazama huko barabarani. Ghafla mumeo hamwoni tena yule aliyekuwa akiichanganya akili yake. Anabaki kujishangaa ilikuwaje akakuoa wewe? Anahisi labda kuna uchawi ulitumika. Mumeo alikupenda ukiwa hujichubui, huweki makeup, yeye alipenda kukuona uko simple tu. Baada ya kuolewa unaanza kukimbizana na wanawake wengine mtaani. Hakika utawavutia wakware wengine, lakini mumeo hatokuwa na furaha na wewe. Huishi tena kwa ajili ya mumeo, bali unatafuta sifa kwa mapapa wa mtaani. Hapo lazima utajiweka majaribuni na hakika utahatarisha ndoa yako.
6064bbb2185f11d34105b5b121740c99.jpg

5. Mawasiliano na wapenzi wako wa zamani. Hili nalo Ni jambo ambalo litamfanya mumeo asiwe na imani na wewe asilani. Kabla ya kuolewa uliua mawasiliano yote na wanaume wako wa kale, baada ya kuwekwa ndani ukaanza kufufua mahusiano. Jiulize, kama hao unaowasiliana nao, ambao huenda walioa kabla hata hujachumbiwa, wamekuwa wanakupenda hivyo, kwa nini walichagua wanawake wengine badala yako? Ungetarajia wakuoe wewe basi! Walikuchezea, ulipofika wakati wa kuoa, wakaachana na wewe, wakaenda kutafuta wanawake ambao wangewafaa kuwa wake wa ndoa. Sasa wewe umeolewa unaendelea kuwa kipozeo kwao. Muheshimu mumeo aliyekutoa kwenu akakujengea heshima mbele ya jamii. Hakuna mwanamume atakaye vumilia urafiki wa mkewe na mwanamume mwingine. Usijiweke kuwa easy target. Utakapoachika, hao hao wanaokudanganya watakaa mbali nawe kwa kukwepa aibu ya jamii. Mheshimu mumeo, mtunzie heshima yake kwa kuzuia tamaa. Ndicho kiapo cha ndoa.

6. Marafiki. Mke mwema hawezi kuwa na wanawake marafiki mashangingi, wasio na maadili ya familia. Kabla ya kuolewa ulijipambanua kama mwanamke mwenye hekima na ujuzi wa kuchagua marafiki. Baada ya kuolewa unaanzisha urafiki na wanawake wasio na mwelekeo. Hakika utatekwa na Ujinga wao. Lazima utafanya kile wanachokifanya wao.

Itaendelea.......
Hakika umeongea vitu vya msingi sana, katika vitu ambacho sikipendi kulinganishwa na hii inatokea kwa sababu ya onjwa onjwa kabla ya ndoa inakera sana, wenye akili wamenote kitu ambao akili zao zinaenda fasta kwenye kukoment bila kusoma ujumbe watabaki kama walivyo, haya mambo siku hizi hayafundishwi sijui kwenye kitchen party wanafundishwa kukata mauno tu sijajua, any way ubarikiwe sana
 
Wanaume mmezid kulalamika siku hizi, pambaneni na hali zenu mbona wanawake wamekandamizwa karne na makarne hawaongei.

Mtoto wa kiume kulinganishwa na mwanaume mwingine aliyekuzid maendeleo unaanza kulia lia mitandaoni. Hii inatokea kwa wanaume wa Dar tu[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama haujaelewa maada ungesoma tu, kila siku mnalalamika ooh wanaume hawatulii sijui wanaume wako hivi Leo unaambiwa mambo ambayo huwavunja moyo wanaume katika mahusiano mtaendelea kuachika, kwa asilimia kubwa ukiangalia hao michepuko wanayafanya hayo ndo maana wanaume wanatulia kwao
 
Sijui umeelewa? Yamemkuta yapi?
Ni mwanaume aliyekutwa na matizo ya wanawake wa aina hiyo anaeweza kuelezea vizuri kama mleta uzi alivyofanya. Kumbuka huwezi shauri vizuri jambo ambalo hujali experience. Over

666
 
Mnaangalia movie starring ana six pack mwanamke anasema eeeeeeh sasa huyo ndo mwanaume

Mko ktk ki vitz chenu anakatiza jamaaa na vogue asema eee hizo ndizo gari za wanaume

Afu siku umemtibua akuuliza hivi wakiambiwa wanaume watoke mbele na wewe utatoka?

Tupambane tu na hali zetu maana hakuna namna.
Hahaha.....hapa umemakila kila kitu....lkn ikifikia hiyo hali hamna ndoa tena...ni kuzalishana na kulala nyumba moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaangalia movie starring ana six pack mwanamke anasema eeeeeeh sasa huyo ndo mwanaume

Mko ktk ki vitz chenu anakatiza jamaaa na vogue asema eee hizo ndizo gari za wanaume

Afu siku umemtibua akuuliza hivi wakiambiwa wanaume watoke mbele na wewe utatoka?

Tupambane tu na hali zetu maana hakuna namna.
Hahahaahaa uwiiiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na nyie wanaume muwe Romantic jamani khaaaaa Tabia ya mwanamke hubadilishwa na mwanaume kwa asilimia 98% Hakuna kinachoniudhi mimi kama wakati mkiwa wachumba ana ku hug kiss za kutosha akisha kuoa laptop ndio wake zenu hizo kiss utaziona kwenye tamthilia na hug, hadi unasahau mara ya mwisho kukuambia I LOVE YOU ilikua lini, hajawahi kukuambia hata umependeza zaidi atasema kila siku unaenda saluni kuchezea tu pesa Khaaaaaa, mi nachooooooka sasa kwanini nisimkumbuke EX hapo jamani, kama hamjui wanawake tunapenda kuambiwa NAKUPENDA kila wakati kwenu ni ugonjwa kaka zetuuuuu
Hapo chacha, sijui wamekusikia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nikupe hii. Wanaume wengi tunaamini wanawake warembo sana hawaoleki. Unajua kwa nini!!? We men feel insecure! Ni hivyo tu. Mume hatokuwa na amani kabisa. Halafu mke naye atatumia muda mwingi kupangua hoja zake wakware. Atatongozwa asubuhi, mchana na jioni. Atatongozwa kuanzia nyumbani mpaka kanisani. Sasa hajazaliwa bado mwanamke mwenye ujasiri wa kuwapangua wanaume wote waliodhamiria kumlaza chali.

Sasa mume kacheza na warembo kabla ya kuoa, mpaka pale alipokusudia kuoa. Akatafuta mwenye vigezo vya mke mwema, (urembo kando). Mke anapowekwa ndani, ghafla anatamani kuwa kama Jlo ama Beyonce. Hapo mwanamume atawaza kuwa mkewe anajiweka mnadani kwa wakware. Hicho alichokikwepa wakati anakuchagua ndicho anakileta ndani. Anahisi alificha tabia zake ili apate ndoa.
Mawivu tu yanawasumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika umeongea vitu vya msingi sana, katika vitu ambacho sikipendi kulinganishwa na hii inatokea kwa sababu ya onjwa onjwa kabla ya ndoa inakera sana, wenye akili wamenote kitu ambao akili zao zinaenda fasta kwenye kukoment bila kusoma ujumbe watabaki kama walivyo, haya mambo siku hizi hayafundishwi sijui kwenye kitchen party wanafundishwa kukata mauno tu sijajua, any way ubarikiwe sana
Thanks mkuu.
 
Kama haujaelewa maada ungesoma tu, kila siku mnalalamika ooh wanaume hawatulii sijui wanaume wako hivi Leo unaambiwa mambo ambayo huwavunja moyo wanaume katika mahusiano mtaendelea kuachika, kwa asilimia kubwa ukiangalia hao michepuko wanayafanya hayo ndo maana wanaume wanatulia kwao
Tena Umesema kweli mkuu. Huu ndio uchawi wa michepuko. Sijawahi sikia michepuko ukimlinganisha mwanamume na mwanamume mwingine asilani. Mchepuko atahakikisha unajiona wewe ni mtu spesho, yaani duniani kote hayupo wa kukulingana. Hiki ndicho anatakiwa afanye mke wa ndoa.
 
Ubaya kwa dunia yetu ya sasa hiyo michepuko ndio hao wake zenu. Yaani mke wako ni.mchepuko wa mwanaume mwingine na anajua kumtuliza ila hawezi mtuliza Mme wake.
 
Tena Umesema kweli mkuu. Huu ndio uchawi wa michepuko. Sijawahi sikia michepuko ukimlinganisha mwanamume na mwanamume mwingine asilani. Mchepuko atahakikisha unajiona wewe ni mtu spesho, yaani duniani kote hayupo wa kukulingana. Hiki ndicho anatakiwa afanye mke wa ndoa.

Ubaya hao wake zenu ndio.michepuko ya wanaume wengine na huko wanakuwa na heshima tu. Michepuko hawezi kukulinganisha na mwanaume mwingine coz anajua anataka pesa tu ila akitoka hapo unaitwa majina yote ya ajabu kwa mashosti zake ukipiga simu kabla hajapokea utasikia jinga hilo linapiga, au buzi hilo. Wanawake ni viumbe hatari sana haswa akiwa anataka kitu. hao wake zenu kuna vitu wanakosa ndio maana madharau wanawaonyesha. Mwanaume anayejua responsibilities zake sioni kwa nini adharauliwe na mke wake.
We jione MTU special wakati mwanamke anabehave Ka Delilah kwa Samson ukisthuka ulipoteza kila.kitu.
 
Nyenyere mfano unakuwa Na mwanaume humkosei unafanya kila kitu ila bado anakusaliti nieli tuachane namapenzi maana hakuna wanaume wakweli hakuna wanaojua Upendo bwana aaaaah minishayakinai

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo nakushauri ujitazame upya. Je, kabla ya kuolewa mlisomana vya kutosha? Ulimfahamu vizuri huyo mumeo? Au ndio wale wa mahusiano ya wiki moja halafu unalazimisha ndoa? Kama uliolewa kwa vigezo vya siku hizi kwamba "wanaume waoaji ni wachache" hivyo ukatega kuwa yoyote atakaye omba kukuoa uko tayari, basi fahamu kuwa unavuna matunda yake.. Vinginevyo kama mumeo alikuwa mwema na mwenye mapenzi ya dhati kwako lakini sasa amebadilika, basi ziangalie njia zako. Jiulize kabla hajabadilika, mliishije na sasa Ni nini kimepungua? Je mlivyoishi mwanzo ndivyo muishivyo sasa?

Pia kuna jambo jingine. Waswahili wana msemo "mwanamke hupigwa kwa upande wa kanga. " Sasa mimi nakwambia hivi, mwanamume hupigwa kwa unyonge wa mwanamke. Kiasili mwanamke ni kiumbe dhaifu, anahitaji protection. Usipambane na mumeo kwa mashindano. Akikosea muulize kwa upole, akikujia juu wewe shuka chini, tena mwombe sana msamaha. Nakuhakikishia hakuna mwanamume mjinga kiasi hicho, dhamira yake lazima tu itamla, ataanza kujutia hayo anayokutendea. Lakini kama utang'ang'ania kupambana naye verbally, ujue utaufanya moyo wake uwe mgumu. Atataka akuonyeshe kuwa yeye ndiye mtawala na si wewe.

Mwisho isije kuwa uliolewa ukiyajua fika mapungufu ya mumeo, lakini ukajidanganya kuwa utamrekebisha. WRONG IN ALL ACCOUNT. Mwanamume mpaka anafikia umri wa kuoa maana yake ameshakomaa na amechagua njia yake. Keshavuka umri wa kurekebishwa. Kama wazazi wake walishindwa kumrekebisha, wewe ni nani hata uweze? Huo utakuwa ni msiba wako daima.
 
Bado sijaolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubaya hao wake zenu ndio.michepuko ya wanaume wengine na huko wanakuwa na heshima tu. Michepuko hawezi kukulinganisha na mwanaume mwingine coz anajua anataka pesa tu ila akitoka hapo unaitwa majina yote ya ajabu kwa mashosti zake ukipiga simu kabla hajapokea utasikia jinga hilo linapiga, au buzi hilo. Wanawake ni viumbe hatari sana haswa akiwa anataka kitu. hao wake zenu kuna vitu wanakosa ndio maana madharau wanawaonyesha. Mwanaume anayejua responsibilities zake sioni kwa nini adharauliwe na mke wake.
We jione MTU special wakati mwanamke anabehave Ka Delilah kwa Samson ukisthuka ulipoteza kila.kitu.
Ama hujaelewa mada, ama upeo wako Ni finyu. Lakini nitakujibu tu. Mada hii imelenga kuonesha matatizo yanayozikumba ndoa, ikijikita upande wa mwanamke tu. Haimaanishi wanaume nao hawana matatizo. Ukisoma mada Jitahidi kuelewa context.

Mwanamke aliye kwenye ndoa anaweza kuchepuka kwa sababu tofauti. Ni vema umekiri bila kujua kwamba huenda kuna vitu anavikosa kwa mumewe. Na huu ndio msingi wa mada hii. Kutafuta kujua ni kwa sababu gani anavikosa hivyo vionjo mpaka anaamua kuchepuka na pia afanye nini ili amani ya ndoa irejee.

Habari ya mwanamume anayejua" responsibilities zake nakuachia wewe utupelekee mada. Ila nakutahadharisha wewe na wengine wenye mtazamo kama huo, wanawake wengine hutafuta mwanamume aliyekamilika kila idara. Wazungu wanamwita MR PERFECT! Nikuambie tu kuwa mpaka ninaposoma makala hii hajazaliwa bado mwanamume wa aina hiyo. Happy hunting!!
 
Back
Top Bottom