Jinsi ya kuua moyo wa mwanamume

Jinsi ya kuua moyo wa mwanamume

Kufa moyo. Ukirudi usiku sikuulizi nasubiri useme mwenyewe usiposema napotezea kuzeeshana kwa stress noo
Kauli yako inaonesha hujawahi olewa wewe
1158b34826e18794c70a58ea2fbf6ce7.jpg
 
Asanteh kwa kutukumbusha, ila jitahidi uongeze points zifike hata ishirini maana mambo ni mengi sana aiseeh
 
Wakuu habari ya leo. Nina imani afya zenu Ni njema kabisa. Mimi si mwanachama hai wa jukwaa hili, lakini leo nimeona nitoe mchango wangu kama njia ya kuboresha mahusiano.

Kuna tabia ambazo kwa namna moja ama nyingine zinachangia sana kuua mapenzi kati ya mke na mume. Sababu kubwa Ni kuwa ghafla mume humwona mkewe kama mgeni moyoni mwake. Baadhi ya tabia hizo zinaweza zisiwe za ajabu sana, lakini zina madhara makubwa moyoni mwa mume.

1. Kumlinganisha mumeo na mwanamume mwingine. Mfano unamwambia mbona wewe hauko kama flani? Usidhani itampa motivation. Badala yake utamfanya ajione hatoshi kuwa mwanamume. Kumbuka kuwa mumeo Ni yule yule ambaye ulimjua kabla hajakuoa. Mara nyingi tamaa ya kuolewa huhadaa ufahamu, kiasi cha kutia upofu usiweze kuona udhaifu wa mwenzi wako. Hii hupelekea watu kuoana pasipo kujua kama kweli wanafanana. Kumbuka ndoa si kufaana bali Ni kufanana. Unapomlinganisha mwanamume na mwanamume mwingine unaufunga moyo wake kwako. Moyoni atakuwa akiwaza, kwa nini basi kuolewa na mimi? Ina maana amemwona yule mwanamume kuwa bora kuliko mimi!!?

Itaendelea........

2. Kumtazama kwa dharau. Baadhi ya wanawake siku hizi wamekuwa na tabia ya kumtazama mwanamume kwa dharau, kunyonga midomo, kumtazama juu mpaka chini kwa dharau. Kitendo hiki unaufunga moyo wa mumeo. Ni kama kumwonyesha kuwa hana thamani tena kwako. Kabla hajakuoa ulikuwa mwepesi wa kuomba msamaha hata pale anapokosea! Yes, anapokosea yeye, ulimweleza kwa lugha ya upole akakukasirikia, ukamwomba akusamehe. Lakini baada ya muda akarudi kukiri kwamba ni kweli ulichomwambia. Mwishowe mshindi ukawa ni wewe mwanamke. Sasa baada ya kuolewa unataka kila unachotamka kifuatwe kwa utii. Umesahau msingi ulioujenga wakati wa uchumba. Mume anakuona kuwa mgeni kwake, si yule waliyerekebishana kwa upole, kwa nafasi. Asilimia kubwa ya wanaume hawawezi kukiri makosa moja kwa moja. Pia Pia mnapopishana mitazamo anatarajia mwanamke ajishushe, Kisha yeye atakuwa anafanyia marejeo hoja zake. Badala yake mke anamtazama mume kwa dharau, anampima chini mpaka juu. Hii inaujeruhi moyo wa mwanamume.

3. Kumwonyesha kuwa humhitaji sana kwenye maisha yako. Kabla ya kuolewa ulikuwa ukilia na kusaga meno kutaka uolewe. Baada ya kuolewa unaanza kumfanyia dharau mumeo, ukidai kwa Mfano, hukufukuzwa kwenu na kwamba asikubabaishe. Kila mkipishana kidogo tu, unajidai kumwonyesha kuwa hakuna jipya unalopata kwake. Je, Ulipata kujiuliza Kabla ya kuolewa, ni kitu gani hasa unachohitaji kwake ambacho huna? Sio kwa habari ya sex tu. Je, ni nini ambacho ungependa akupe ili ujione umekamilika kuwa mwanamke? Au ndio ndoa za fasheni? Mfanye mume wako ajione mwanamume, hakika utauteka moyo wake.

4. Kubadili mfumo wa maisha. Kabla hajakuoa ulikuwa ukivaa mavazi fulani na kujipamba kwa namna fulani. Ni kwa mwonekano huu mumeo alijikuta ametekwa bakunja! Akanasa kwenye mtego, asione mwingine zaidi yako. Sasa baada ya kuolewa, unadhani umemaliza jukumu. Ghafla ukabadili utaratibu wa kujipamba. Sasa tena hujipambi ili kumfurahisha mumeo, bali unajipambamba kuwafurahisha wanaokutazama huko barabarani. Ghafla mumeo hamwoni tena yule aliyekuwa akiichanganya akili yake. Anabaki kujishangaa ilikuwaje akakuoa wewe? Anahisi labda kuna uchawi ulitumika. Mumeo alikupenda ukiwa hujichubui, huweki makeup, yeye alipenda kukuona uko simple tu. Baada ya kuolewa unaanza kukimbizana na wanawake wengine mtaani. Hakika utawavutia wakware wengine, lakini mumeo hatokuwa na furaha na wewe. Huishi tena kwa ajili ya mumeo, bali unatafuta sifa kwa mapapa wa mtaani. Hapo lazima utajiweka majaribuni na hakika utahatarisha ndoa yako.
6064bbb2185f11d34105b5b121740c99.jpg


5. Mawasiliano na wapenzi wako wa zamani. Hili nalo Ni jambo ambalo litamfanya mumeo asiwe na imani na wewe asilani. Kabla ya kuolewa uliua mawasiliano yote na wanaume wako wa kale, baada ya kuwekwa ndani ukaanza kufufua mahusiano. Jiulize, kama hao unaowasiliana nao, ambao huenda walioa kabla hata hujachumbiwa, wamekuwa wanakupenda hivyo, kwa nini walichagua wanawake wengine badala yako? Ungetarajia wakuoe wewe basi! Walikuchezea, ulipofika wakati wa kuoa, wakaachana na wewe, wakaenda kutafuta wanawake ambao wangewafaa kuwa wake wa ndoa. Sasa wewe umeolewa unaendelea kuwa kipozeo kwao. Muheshimu mumeo aliyekutoa kwenu akakujengea heshima mbele ya jamii. Hakuna mwanamume atakaye vumilia urafiki wa mkewe na mwanamume mwingine. Usijiweke kuwa easy target. Utakapoachika, hao hao wanaokudanganya watakaa mbali nawe kwa kukwepa aibu ya jamii. Mheshimu mumeo, mtunzie heshima yake kwa kuzuia tamaa. Ndicho kiapo cha ndoa.

6. Marafiki. Mke mwema hawezi kuwa na wanawake marafiki mashangingi, wasio na maadili ya familia. Kabla ya kuolewa ulijipambanua kama mwanamke mwenye hekima na ujuzi wa kuchagua marafiki. Baada ya kuolewa unaanzisha urafiki na wanawake wasio na mwelekeo. Hakika utatekwa na Ujinga wao. Lazima utafanya kile wanachokifanya wao.

Itaendelea.......

na nyie wanaume muwe Romantic jamani khaaaaa Tabia ya mwanamke hubadilishwa na mwanaume kwa asilimia 98% Hakuna kinachoniudhi mimi kama wakati mkiwa wachumba ana ku hug kiss za kutosha akisha kuoa laptop ndio wake zenu hizo kiss utaziona kwenye tamthilia na hug, hadi unasahau mara ya mwisho kukuambia I LOVE YOU ilikua lini, hajawahi kukuambia hata umependeza zaidi atasema kila siku unaenda saluni kuchezea tu pesa Khaaaaaa, mi nachooooooka sasa kwanini nisimkumbuke EX hapo jamani, kama hamjui wanawake tunapenda kuambiwa NAKUPENDA kila wakati kwenu ni ugonjwa kaka zetuuuuu
 
Kwenye namba 4.

3ed64-before-after-make-up-black-girls-4.jpg



3b759d43e726f6ac66ba169cefa24f5a--makeup-transformation-make-up.jpg
Ngoja nikupe hii. Wanaume wengi tunaamini wanawake warembo sana hawaoleki. Unajua kwa nini!!? We men feel insecure! Ni hivyo tu. Mume hatokuwa na amani kabisa. Halafu mke naye atatumia muda mwingi kupangua hoja zake wakware. Atatongozwa asubuhi, mchana na jioni. Atatongozwa kuanzia nyumbani mpaka kanisani. Sasa hajazaliwa bado mwanamke mwenye ujasiri wa kuwapangua wanaume wote waliodhamiria kumlaza chali.

Sasa mume kacheza na warembo kabla ya kuoa, mpaka pale alipokusudia kuoa. Akatafuta mwenye vigezo vya mke mwema, (urembo kando). Mke anapowekwa ndani, ghafla anatamani kuwa kama Jlo ama Beyonce. Hapo mwanamume atawaza kuwa mkewe anajiweka mnadani kwa wakware. Hicho alichokikwepa wakati anakuchagua ndicho anakileta ndani. Anahisi alificha tabia zake ili apate ndoa.
 
Nyenyere mfano unakuwa Na mwanaume humkosei unafanya kila kitu ila bado anakusaliti nieli tuachane namapenzi maana hakuna wanaume wakweli hakuna wanaojua Upendo bwana aaaaah minishayakinai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na nyie wanaume muwe Romantic jamani khaaaaa Tabia ya mwanamke hubadilishwa na mwanaume kwa asilimia 98% Hakuna kinachoniudhi mimi kama wakati mkiwa wachumba ana ku hug kiss za kutosha akisha kuoa laptop ndio wake zenu hizo kiss utaziona kwenye tamthilia na hug, hadi unasahau mara ya mwisho kukuambia I LOVE YOU ilikua lini, hajawahi kukuambia hata umependeza zaidi atasema kila siku unaenda saluni kuchezea tu pesa Khaaaaaa, mi nachooooooka sasa kwanini nisimkumbuke EX hapo jamani, kama hamjui wanawake tunapenda kuambiwa NAKUPENDA kila wakati kwenu ni ugonjwa kaka zetuuuuu
Umesema kweli, lakini kuna pande mbili hapa. Kabla ya kukuoa, kuna kanuni ya kumteka mwanamume uliitekeleza bila kujua, the power of the visual. Hisia za kiume huamshwa mara moja kwa kutazama tu. Nikuulize: ni lini umewahi ona magazeti ama mitandao ikichapisha wanaume wamevaa vibukta kuonesha miguu yao inavyovutia? Au Ni lini Umeona media zikizungumzia vichupi vya kuogelea vya kiume? Hii ni kwa sababu Ni mara chache mno mwanamke atavutiwa na mwanamume kwa kutazama tu kiungo fulani cha mwili.

Unajua asilimia kubwa ya wanaume watalipa kuona show ya wanawake wakicheza wamevaa vichupi ama uchi wa mnyama! Labda ulikuwa hujui, mitandao inayoongoza kwa kutazamwa sana duniani kote ni ya ngono, picha za wanawake uchi n.k. watazamaji wakubwa ni wanaume. Mwanamke akimkuta mwanamume amekaa korodani zikiwa nje atawastua wanaume wenzie wamsitiri mwenzao. Lakini mimi nikiingia bar kwa mfano, nikakuta mwanamama ameketi kachanua kidogo tu miguu nikaona mpaka chupi kajisahau, nitatafuta kiti kinachomkabili ili niendelee "kuinjoi" zaidi. Nitalaani jaribio lolote la kumshtua afunike mapaja (kimoyomoyo).

Hoja ni kwamba, ulipokuwa hujaolewa, ulijitahidi kuwa mpya kila siku kwa mpenzi wako. Mwonekano, lugha tamu, adabu njema. Ulijaribu kumwonesha Ni Jinsi gani bila wewe hajakamilika.

Baada ya kuolewa, ukaacha kumpa hivyo vionjo. Utavua nguo na kupanda kitandani, atakuja hapo kisha unamwambia I love you. Yeye atakujibu, thanks, basi. Utaumia moyo. Elewa kuwa wanaume wanatekwa kwa vitendo sio maneno. Mwonyeshe kwa vitendo usiseme kwa mdomo. Mumeo akipita uchi mbele yako haitakupa ashki, lakini jaribu wewe upite mbele yake ukiwa na na kijinguo cha kuonesha uone pumzi inavyompanda. Halafu mwambie leo nataka tulale tu, sijisikii. Nakuhakikishia ataanza kukutongoza upya
 
Wanaume mmezid kulalamika siku hizi, pambaneni na hali zenu mbona wanawake wamekandamizwa karne na makarne hawaongei.

Mtoto wa kiume kulinganishwa na mwanaume mwingine aliyekuzid maendeleo unaanza kulia lia mitandaoni. Hii inatokea kwa wanaume wa Dar tu[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahaaa.....
 
Endeleeni tuu kushupaza shingo zenu ata roho asemapo nanyi! Siku yaja, hakuna sketi wala hips za mtu zitasalia juu ya nyumba yake
 
Back
Top Bottom