Kama wameshakupa internet accounting ID na password, then unaweza kupata huduma zote za internet banking ambazo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye account yako na kwenda kwenye account ya mtu mwingine wa CRDB pekee, hawatoi huduma kama huyo mtu anayemtumia hayupo CRDB. Hii huduma nimeitumia mpaka sasa nina miaka miwili ni nzuri sana sihitaji kwenda kukaa foleni bank ili kumhamishia mtu fedha ambaye yupo CRDB, naingia kwenye internet na kutuma fedha japo wana chaji kila mwezi Tsh 1000. Huduma ya kununua vitu online kama ulivyo eleza hapo chini siyo sawa na huduma ya internet banking, inataratibu tofauti.