47pro
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 1,204
- 332
1: ASIWE KWENYE UHUSIANO
Jambo lingine la kuzingatia kwa mwanaume huyo wakati wa harakati za kumweka mikononi mwako ni kuhakikisha hayupo kwenye uhusiano na mtu mwingine. Kunabaadhi ya wanawake wapo tayari kuwa na mwanaume hata kama yupo na mpenzi mwingine; hilo ni kosa na naweza kusema ni umasikini wa kufikiri.Kama kweli umempenda, itakuwa na maana kama utaweka makazi yamoyo wako kwake milele na siyo kwamuda mfupi tu.
2: JISOGEZE ZAIDI
Tayari umeshakuwa na uhakika kuwa hana mtu, sasa unatakiwa kujisogeza
karibu yake.Jizoeshe kumsalimia mara kwa mara na kumsifia kuwa
amependeza.Kamwe usioneshe dalili kwamba wewe ni ‘maharage ya Mbeya’, ishia kwenye kujisogeza karibu yake kwa kumsifia na kufanya mambo mengine
yanayofanana na hayo na siyo zaidi yahapo.
3: JENGA URAFIKI
Ukaribu wenu sasa unaweza kuwafanya marafiki wa karibu. Kama uko naye ofisi moja au mnaishi mtaa/nyumba moja ni rahisi zaidi. Kuwa rafiki yake wa kweli mwenye kujadiliana naye mambo ya msingi.Katika urafiki wenu, kamwe usiwe mzungumzaji sana (hasa wa mambo yasiyofaa), aidha usipende kukaa
naye katika mazingira yenye vificho ambayo yataweza kusababishakuingia kwenye mtego mbaya.
4: ZUNGUMZIA ZAIDI MAISHA
Kuzungumzia zaidi maisha na kumshauri juu ya mambo muhimu ya maisha, kutamfanya akuone wewe ni mwanamke makini mwenye malengo
mazuri katika maisha yako. Wanaume wanapenda sana wanawake ambao
vichwa vyao vinafanya kazi sawasawa.Hii inaweza kuwa sababu itakayomfanya atamani kuwa karibu yako zaidi, jambo ambalo ndiyo shabaha ya moyo wako.
5: HAKUNA YEYE BILA WEWE
Kwasababu tayari ni marafiki na mnashirikiana baadhi ya mambo,tengeneza mazingira ya kuwa naye karibu zaidi. Mshirikishe kwenye mambo yako, mfanye ajione si mkamilifu bila kuwa na wewe karibu.Hili litawezekana kwa kuishika siku yake, kumtakia siku njema na kumjulia hali yake kazini na maendeleo yake kwa ujumla. Kwa kuwa ni marafiki, kwa ndani lazima hisia za mapenzi zitaibuka juu yako na utamuweka kwenye nafasi ya kufikiri kuanzisha uhusiano na wewe.
6: NI WAKO TU
Ukipitia hatua zote, bila shaka mwanaume huyo ni wako tu. Ikiwa pamoja na vyote hivyo bado haonyeshi dalili au hajafunguka kuwa unamhitaji, basi mwache, siyo riziki yako. Kwanini ung’ang’anie usipopendwa?