Jinsi Ya kutengeneza Print Out za Kwenye System!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Wasalaam...Sijui kama kichwa changu cha Uzi kitakuwa kimeeleweka ila nilikuwa naomba msaada wa kuelekezwa Jinsi ya kutengeneza Kitu kama file ili nikiprint kiwe sawa sawa

Yaani labda tuseme unasystem ya kuingiza jina la mtu..namba yake ID yake kwenye system ila ukiprint inatola kawaida tuu kama imeendaliwa kwenye Microsoft word!

Mfano kuna system ya kuingiza wanunuzi wa bidhaa kwenye computer kisha una print karatasi yake aondoke nayo sasa ukifungua kwenye System Utakuta Taarifa zake zimesha jazwa wewe unaongeza kitu kidogo na ukiprint haitoi ile mibox box ambayo taarifa zake zilikuwa zinajazwa sasa na mm nataka niwe nayo kwenye Computer yangu....Ili niende sawa na Boss hata mimi nikimpa karatasi yangu iwe sawa tuu kama imeprintiwa kutoka kwenye System

Najua mtakuwa mmenielewa mfumo ninao uzungumzia! Kampuni nyingi wanatumia!

Msaada tafadhari
 
Karibu kila programming language ina function ya kuprint page. System yako imetengenezwa kwa kutumia language gani? Je ni Web-Based System? Kama jibu ni ndiyo, basi sio lazima utengeneze print button. Kwenye browser (e.g. Firefox, Opera, Google Chrome) kuna option ya ku-print page.
 
Kauliza jinsi ya kutengeneza we unataka kumtengenezea, kwan ukimuelekeza hapa utapungukiwa na nin .?
Jinsi ya kuteneza ni mambo mengi mno ye kama ni programmer aweke code zake aliposhindwa asaidiwe na sio sisi tufanye from scratch
 
Jinsi ya kuteneza ni mambo mengi mno ye kama ni programmer aweke code zake aliposhindwa asaidiwe na sio sisi tufanye from scratch
Hajakwambia ufanye from scratch, kaomba kuelekezwa, you could atleast highlight out few points aanzie wapi ..

Na pia hakuna sehem aliyosema anataka kutengenezewa..
 
Kwa kuja kuuliza hili swali ni wazi kabisa huna idea yoyote ile na software development.
Jibu ni dogo tu, hata ukielekezwa hutoweza, unaweza hisi ni kitu kidogo tu kuprint ila ni zaidi ya hapo, hadi ukae na mtaalamu aangalie software yenyewe unayotumia ni ipi, document inayoprintiwa ikoje, data zinatunzwa wapi, vipi. Na akimaliza ajue anawezaje kutengeneza the exact copy. Kama huna ujuzi huo huwezi elekezwa ukafanya tena kwenye internet, ni skill inayochukua miaka kumaster sio sawa na kuelekezwa fungua website flani click hapa, hapana.
 
Karibu kila programming language ina function ya kuprint page. System yako imetengenezwa kwa kutumia language gani? Je ni Web-Based System? Kama jibu ni ndiyo, basi sio lazima utengeneze print button. Kwenye browser (e.g. Firefox, Opera, Google Chrome) kuna option ya ku-print page.
Yaani ni Computer tuu ina window 8 na short cut ya hiyo system ukiifungua tuu unaona Kama mtu kafanya malipo Ndio utaona Taarifa zake ila kama hajafanya huwezi kuona taarifa zake....so akiwa amefanya malipo unaingia unamfungua wewe unamalizia kujaza taarifa chache tuu then kuna option ya ku update kisha una print....haihitaji internet sasa mimi nataka niwe na copy ya hio kitu kuwa nikifungua basi mm nijaze taarifa zake zote si atakuwa hayupo kwenye system....so nikienda kwenye computer yangu niwe na uwezo wa kujaza kila kitu chake na nikiprint iwe sawa na ile ya kwenye system japo hii nimejaza kwa mkono wangu.....

Tuseme akiwa amelipa ukifungua kwenye sytem unaona

1.Bidhaa aliyo nunua
2.Namba yake ya Risiti
3.Kanunulia wapi
4.Jina lake
5.Namba yake ya Simu
6.Jinsia Yake
7.Tarehe
Sas mm niwe n uwezo wa kujaza hvyo vitu kwa mkono na nikiprint niweze kuwa sawa na yule alioko kwenye system
 
Kwa kuja kuuliza hili swali ni wazi kabisa huna idea yoyote ile na software development.
Jibu ni dogo tu, hata ukielekezwa hutoweza, unaweza hisi ni kitu kidogo tu kuprint ila ni zaidi ya hapo, hadi ukae na mtaalamu aangalie software yenyewe unayotumia ni ipi, document inayoprintiwa ikoje, data zinatunzwa wapi, vipi. Na akimaliza ajue anawezaje kutengeneza the exact copy. Kama huna ujuzi huo huwezi elekezwa ukafanya tena kwenye internet, ni skill inayochukua miaka kumaster sio sawa na kuelekezwa fungua website flani click hapa, hapana.
Unaweza anza kunielekeza kuwa kinafanyika hiki na hiki na mm nikajua kuwa nikitaka kufanya hivi nimuone fulani
 
mimi nataka niwe na copy ya hio kitu kuwa nikifungua basi mm nijaze taarifa zake zote si atakuwa hayupo kwenye system....so nikienda kwenye computer yangu niwe na uwezo wa kujaza kila kitu chake na nikiprint iwe sawa na ile ya kwenye system japo hii nimejaza kwa mkono wangu.....

Sas mm niwe n uwezo wa kujaza hvyo vitu kwa mkono na nikiprint niweze kuwa sawa na yule alioko kwenye system
Mimi naona ni tatizo la privilege tu, huwezi kuwa na copy sababu huna 'clearance' inayokuwezesha kufanya hivyo, labda mabosi wako watakuwa na hiyo privilege. Sababu ya pili yaweza kuwa mantiki ya unachotakiwa kufanya. System lazima iwe na balance and checks. Mfano kama wewe ni mwalimu, system haitakiwi kukuruhusu ufanye kile ambacho mwanafunzi anafanya-mfano hutakiwi kurekebisha matokeo kama wewe ni mwanafunzi.

Ongea na System administrator wako akueleweshe, hakuna sababu ya kuingiza taarifa upya ili tu uwe na kopi wakati tayari mteja ameshaziweka. Ikikuruhusu ufanye hivyo, itajenga mazingira ya kupiga pesa maana hata wewe unaweza ukajifanya mteja kitu ambacho ni makosa. Nadhan kazi yako wewe ni kuhakiki taarifa walizoweka wateja, hivyo ni sawa kama hupewi nafasi ya kuwa na role ya mteja.
 
Back
Top Bottom