Jinsi ya kutengeneza keki. Ni rahisi sana

Feb 16, 2019
8
45
Utangulizi

Keki hutengenezwa kutokana na unga wa ngano, mafuta, mayai na vikolezo mbali mbali. Kuna Keki za aina mbalimbali kulingana na umbo, ukubwa vikolezo n.k. Aina za Keki pia hutegemea wakati (Occassions) kwa mfano kuna keki za harusi, kumbukumbu ya kuzaliwa (birthday), na zile za kawaida n.k

Keki hutengenezwa kutokana na unga wa ngano, siagi, sukari, baking powder na mayai . Kadhalika vanila, maziwa na vikolezo vingine vinaweza kutumika.

Unga wa ngano unaotoa matokeo mazuri kwenye keki ni wenye protini nyingi (11 13%). Kama ilivyo kwa mkate keki inaweza pia kutengenezwa kwa kuchanganya unga wa aina nyingine kama mhogo, soya nk.kutegemea na matakwa.

Kanuni za kitekinologia zinazohusiana na utengenezaji wa keki ni :-
Sifa kubwa ya keki ni kuwa nyepesi , kuchambuka na kutokunata mdomoni wakati wa kula.
Muundo wa wepesi wa keki hutokana na hewa nyingi iliyojazwa katika donge wakati wa kukoroga pamoja na viambaupishi vinavyosaidia kazi hii. Ili kufanikisha hili ,ukorogaji lazima uwe wa kuelekea upande mmoja.

Kazi za viambaupishi:-
Sukari- Huongeza ladha kwenye keki , uwezo wa kuhifadhi na huchangia katika kuwezesha keki kuwa nyepesi
Siagi huongeza ladha hasa baada ya kuoka.
Mayai- Husaidia kuongeza na kuhifadhi hewa ndani ya donge na hivyo keki kuwa nyepesi. Pia huleta ladha nzuri ya keki baada ya kuokwa.
Viambaupishi:

Unga wa ngano
1kg.

Siagi
0.4kg

Sukari
0.4kg

Mayai
10

Dawa ya kuokea(baking powder) vijiko vya
chai
6

Vinginevyo: Maziwa, vanilla, chumvi - kidogoVifaa:
Oven
Chekecheo
Mwiko
Mizani
Meza
Bakuli au mashine ya kuchanganyia
Vibati vya kuokea
Vifungashio
Hatua za utengenezaji.

Unga:
Chagua unga mzuri unaofaa kwa keki. Pima kiasi kinachohitajika katika mizani. Chukua baking powder na changanya vipimo kama No.3
Chekecha:
Chekecha unga wako kwa kutumia chekeche lenye matundu madogo madogo. (Chekecha pamoja na banking powder).
Changanya:
Kilo moja ya unga weka gramu 400 siagi, sukari gram 400, dawa ya kuumulia (baking powder) vijiko vya chai 6 - 8, mayai 10, chumvi, maziwa, vanilla kidogo.
Changanya:
Sugua siagi na sukari iliyosagwa mpaka itoe mapovu (creaming method). Piga mayai mpaka yatoe povu, ongeza kwenye mchanganyiko wa siaga na sukari polepole huku ukikoroga mpaka vimechanganyika vizuri. Changanya unga na vikolezo vyote. Ongeza maziwa au maji ili kuweza kupata uji mzito.
Jaza
Weka mchanganyiko kwenye vikopo, au vyombo vya kuokea.
Oka
Kwenye nyuzi joto 225 - 250 oC kwa muda wa dakika10-15 ambayo keki zako zitakuwa na rangi ya kahawia.
Poza
Panga kwenye waya/chombo cha kupozea.
Funga
Weka kwenye mifuko ya plastiki na funga vizuri.


Kuhifadhi na kudumisha ubora.

Kudhibiti ubora na hatua za utengenezaji ni kama kwenye biskuti.
Keki iliyotengenezwa vizuri inaweza kukaa siku 5 - 7 bila kuharibika.

Kutengeneza keki kwa kutumia unga wa muhogo
Malighafi:
Unga bora wa muhogo gramu 500 na unga wa ngano gramu 500
Sukari gram 250
Mafuta mazito (Blue band) gramu 400
Baking powder gramu 30
Vanilla milita 15
Maziwa mililita 300 hadi 500
Mayai 10
Hatua za utengenezaji zina fanana kama ilivyo kwenye keki za ngano pekee.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom