KakaJambazi
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 18,711
- 12,067
Naomba wataalam wa kutengeneza zile karanga flani ivi zinakua sijui na mayai ambazo naziona kwenye masuper market au sherehe ambalo wanaita bites anipe recipe yake tafadhali.
CC gfsonwin ladyfurahia charminglady Madame B etc
=================================================
CC gfsonwin ladyfurahia charminglady Madame B etc
=================================================
Mahitaji
-karanga kilo moja
-mayai 2-3 inategemea na ukubwa
-chumvi kijiko kimoja
-sukari kiasi unachohitaji
-unga wa ngano robo kilo(kidogo tu)
Kuandaa
-chukua karanga weka katika sinia, chambua kuondoa karanga mbovu,zilikatika na taka taka.
-baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia, piga mayai katika chombo pembeni na uweke chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
-chukua kiasi cha sukari unachokadiria kitakufaa Tia katika ule mchanganyiko wa karanga,mayai na chumvi kisha changanya ili sukari inate katika karanga zote.
-
Mahitaji:
-Karanga kilo moja.
-Mayai 2-3 inategemea na ukubwa.
-Chumvi kijiko kimoja.
-Sukari kiasi unachohitaji.
-Unga wa ngano robo kilo(kidogo tu).
-Mafuta ya kupikia.
Kuandaa:
-Chukua karanga weka katika sinia, chambua kuondoa karanga mbovu,zilikatika na taka taka.
-Baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia, piga mayai katika chombo pembeni na uweke -Chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
-Chukua kiasi cha sukari unachokadiria kitakufaa Tia katika ule mchanganyiko wa karanga,mayai na chumvi kisha -Changanya ili sukari inate katika karanga zote.
-Chukua unga Tia Katika mchanganyiko wako, changanya vizuri kuhakikisha karanga zote zimekuwa nyeupe kwaku funikwa na unga.
-Weka mafuta kiasi kwenye kikaango, yakichemka anza kukaanga karanga zako hakikisha unazitoa kabla hazijawa Brown sana usijeunguza karanga zako
Pia unaweza kuziandaa kwa njia hii..
- Chukua karanga ziloweke kidogo kwenye maji yenye chumvi kiasi
-zikaushe kwenye kikaango
-vunja yai kisha uchanganye na sukari koroga mpaka mchanganyiko upate rangi nyeupe
-tia karanga zako kwenye mchanganyiko wa yai na sukari
-nyunyizia unga wa ngano kwene mchanganyiko wako kisha ukaange kwa deepfry
-zikiwa brown ipua tayari kwa kula na juisi pia soda!@KakaJambazi
Last edited by a moderator: