Jinsi ya kutafuta kazi nje ya Nchi

Jinsi ya kutafuta kazi nje ya Nchi

454

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
136
Reaction score
193
Wakuu habari zenu,Natafuta kazi nje ya Nchi hususani Dubai,Abudhabi,Kuwait,Bakhrain Mimi ni dereva ninauzoefu na kazi yangu nimejaribu kutumia Maagent hapa Dar Lakini wamenitapeli sitaki hata kusikia habari za Maagent.Kuna mtu amenishauri niombe Visiting Visa Dubai kisha nikifika Kule nitafute Kampuni niombe kazi.Je njia hii itanisaidia maana passport ninayo na nauli pia ya kwenda Dubai ipo pia
 
Pata kwanza kazi nzuri kulingana na fani yako hapa ndani ya nchi na Mungu akukujalia kupitia hiyo kazi utaweza kubahatika kuunfanishiwa nje ya nchi. Ila sehemu zote ajira ni shida, kazana sana!
 
Unapoomba visa ya nchi yoyote na ukapata kama ni visit visa huwezi kuomba kazi kwani umeenda kutembea tu
Agents wengi ni matapeli kwa ushauri ungeenda katika Balozi hizo na kuuliza taratibu zao za kazi utapata jibu la kukuridhisha.
 
nimeiishi abudhabi miaka 25 nini cha kufanya chukua visit viza nenda dubai kama una sehemu ya kufikia bora zaidi anza kutafuta kazi ukipata kazi na ukajaza formu ya kazini kampuni yako inaaza kukuombea viza ya kazi wakati wanakuombea viza ya kazi wewe unakuwa umeacha contact zako za tz na hapo unarudi tz kuisubiria ikitoka wanakutumia na unaingia bila wasiwasi na unaanza kazi ila kazi ya udreva utachukua mda mpaka upate ya kwao na pia kazi hiyo hailipi mbona kuna kaxi nyingi tu air port au sharjah
 
Back
Top Bottom