Jinsi ya kurudisha account niliyosahau password

Raia mmoja

Member
May 3, 2021
43
111
Habari wanajamvi! Poleni na mahangaiko ya kupambana na maisha.

Kama title inavyojieleza, naombeni msaada kwa anayeweza kunielekeza namna ya kurudisha account yangu ya Facebook ya biashara ambayo kiukweli nimesahau password yake.

Account hii niliifungua mwaka 2012 nikawa naitumia kwa malengo mbalimbali ikiwemo biashara, nili download app yake nikawa na login automatically bila kuweka password.

Sasa juzi nime logout kwa bahati mbaya alafu nimeshindwa ku login kwasababu nimesahau password yake, na bahati mbaya number ya simu niliyoitumia ku register account hiyo nilishaachana nayo miaka mingi Sana, siitumii tena hiyo number.

Natumiwa notifications zote kwa yanayoendelea kwenye account yangu, Kama mtu akinitumia sms au aki comment etc, lakini nikijaribu kuingia nakosea password nimesahau na wananitumia code kwenye number ya zamani ambayo siitumii Tena kwa miaka mingi Sana

Ndugu zangu naomba msaada sana wa kunisaidia kuirudisha tena account yangu!

Natanguliza shukrani! 🙏
 
Sasa hio rahisi piga simu mwenye hio namba yako ya zamani waeleze ukweli waambie wakutumie hizo code wakixipata after hapo u log in alafu change namba
 
Back
Top Bottom