Jinsi ya kupika rosti la mayai ya kuchemsha

Presiesy

Member
Jan 28, 2014
40
13
Kuna sehemu nililiona ili pishi nikajaribu kulipika aisee ni tamu asikwambie mtu, hii ni kwa wale wenzangu na mimi wanaopenda kujaribu jaribu mapishiii.

MAHITAJI
1: Mayai Manne.
2: Nyanya tatu.
3:kitunguu maji kimoja.
4:pilipili hoho moja.
5: karoti moja.
6: nyanya chungu(KAMA UKIPENDA) tatu.
7: Nazi moja. 8: Mafuta ya kupikia chupa moja.
9: Chumvi upendavyo.

JINSI YA KUANDAA.

1; Chemsha mayai yako kwa dakika 15, yakisha iva yaepue yaache yapoe halafu yamenye.
2; Weka mafuta ya kula kwenye moto wa wastani yakisha pata moto weka mayai yako ambao umeyamenya na yakapoa yaache mpaka yawe na rangi ya kahawia ila yasikaukeee halafu yaepue ili yajichuje mafuta.
4; katakata nyanya, karoti,nyanya chungu, kitunguu maji na pilipili hoho.
5: kuna nazi yako halafu chuja matui mawili kama unavyounga maharage.
6: weka sufuria jikoni weka na mafuta kidogo ya kuungia mboga halafu weka kitunguu maji kiache mpaka kiwe kahawia halafu weka karoti nazo kaanga mpaka zibadilike rangi kidogo halafu weka pilipili hoho kaanga kidogo halafu uweke nyanya na nyanya chungu halafu funika mpaka ziive kidogo (usisahau kuweka chumvi kwenye huo mchanganyiko).

7: mchuzi ukishaiva iva weka mayai yako ambayo ulishayakaanga halafu weka tui jepesi halafu piga piga mpaka liive(lichemke) likishaiva weka tui bubu nalo piga piga mpaka nalo liive (lichemke) likishaiva likisha iva epua.

Mboga yako ipo tayari kuliwa unaweza kula na kitu chochoteee. Karibuni.....
 
Asante aisee. Umenikumbusha pishi la chuo hahaha.

sasa ukitaka mboga iwe na mvuto haswaa, hilo yai likate nusu kabla ya kuliweka kwenye mchuzi. Mvuto 100%. Ila sasa ili kiini kisichomoke inabidi utie na tui bubu kabisaa, likianza kuchemka unashusha mayai na dakika 2 unaipua.

Wapi ubwabwa, tuanze kujinona��
 
Asante aisee. Umenikumbusha pishi la chuo hahaha.

sasa ukitaka mboga iwe na mvuto haswaa, hilo yai likate nusu kabla ya kuliweka kwenye mchuzi. Mvuto 100%. Ila sasa ili kiini kisichomoke inabidi utie na tui bubu kabisaa, likianza kuchemka unashusha mayai na dakika 2 unaipua.

Wapi ubwabwa, tuanze kujinona��

Alafu juu unanyunyizia majani giligilani for garnishing na ladha pia.....

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Asante aisee. Umenikumbusha pishi la chuo hahaha.

sasa ukitaka mboga iwe na mvuto haswaa, hilo yai likate nusu kabla ya kuliweka kwenye mchuzi. Mvuto 100%. Ila sasa ili kiini kisichomoke inabidi utie na tui bubu kabisaa, likianza kuchemka unashusha mayai na dakika 2 unaipua.

Wapi ubwabwa, tuanze kujinona��

Hahahahahaha ni hatariiii asee
 
Hahhaha upishi mwepesi kabisa...ila nilivyoona mwanzo niliogopa kuona mtiririko wa maandishi....sisi ndo wale wale wavivu wa kusoma lol...
Asante mwaya kwa upishi!
 
Vipi mkuu kuhusu hicho kiini cha ndani? Unakikaanga pamoja ama una kitoa? Thnx
 

ImageUploadedByJamiiForums1401710377.504439.jpg
 
Last edited by a moderator:
Kuna sehemu nililiona ili pishi nikajaribu kulipika aisee ni tamu asikwambie mtu, hii ni kwa wale wenzangu na mimi wanaopenda kujaribu jaribu mapishiii. MAHITAJI 1: Mayai Manne. 2: Nyanya tatu. 3:kitunguu maji kimoja. 4:pilipili hoho moja. 5: karoti moja. 6: nyanya chungu(KAMA UKIPENDA) tatu. 7: Nazi moja. 8: Mafuta ya kupikia chupa moja. 9: Chumvi upendavyo. JINSI YA KUANDAA 1; Chemsha mayai yako kwa dakika 15, yakisha iva yaepue yaache yapoe halafu yamenye. 2; Weka mafuta ya kula kwenye moto wa wastani yakisha pata moto weka mayai yako ambao umeyamenya na yakapoa yaache mpaka yawe na rangi ya kahawia ila yasikaukeee halafu yaepue ili yajichuje mafuta. 4; katakata nyanya, karoti,nyanya chungu, kitunguu maji na pilipili hoho. 5: kuna nazi yako halafu chuja matui mawili kama unavyounga maharage. 6: weka sufuria jikoni weka na mafuta kidogo ya kuungia mboga halafu weka kitunguu maji kiache mpaka kiwe kahawia halafu weka karoti nazo kaanga mpaka zibadilike rangi kidogo halafu weka pilipili hoho kaanga kidogo halafu uweke nyanya na nyanya chungu halafu funika mpaka ziive kidogo (usisahau kuweka chumvi kwenye huo mchanganyiko). 7: mchuzi ukishaiva iva weka mayai yako ambayo ulishayakaanga halafu weka tui jepesi halafu piga piga mpaka liive(lichemke) likishaiva weka tui bubu nalo piga piga mpaka nalo liive (lichemke) likishaiva likisha iva epua. Mboga yako ipo tayari kuliwa unaweza kula na kitu chochoteee. Karibuni.....

hii kitu umenikumbusha kwa mama lishe wa kigamboni mama ebenezer wali yai nikomoeni uwiii...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom