Jinsi ya kupika keki ya zabibu kavu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kupika keki ya zabibu kavu

Discussion in 'JF Chef' started by TIMING, Apr 5, 2011.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 145
  JINSI YAKUPIKA KEKI YA ZABIBU KAVU



  [​IMG]



  Tengeneza keki ya zabibu kavu kisha ongezea ladha mbali mbali kutokana na upendavyo fata maelekezo hapo chini



  Mahitaji:


  240gram zabibu kavu

  240garm maziwa ya maji

  240garm siagi (butter)

  ½ chumvi kijiko kidogo cha chai

  240gram sukari

  240gram korosho au walnuts au karanga chochote ulichonacho

  500gram unga wa ngano

  1 kijiko kidogo cha chai baking soda (Baking powder)

  2 mayai



  JINSI YAKUTENGENEZA

  Washa oveni yako katika joto 325 degree F (165 degree C) kisha kipake chombo chako siagi utakacho tumia kuokea keki yako.

  Chukua bakuli changanya unga wa ngano, zabibu na baking soda kasha weka pembeni.

  Chukua bakuli nyingine weka siagi na sukari ndani kisha piga mapaka ichanyanyike vizuri na kua laini kabisa kisha vunjia mayai ndani piga paka mchanganyiko wako uwe laini kabisa.

  Kisha chukka mchanganyiko wa unga mimina kwenye mchanganyiko wa mayai changanya pole pole mpaka upate mchanganyiko mzito wa wastani kama itakua nzito sana ongeza maziwa kama itakua nyepesi sana ongeza unga.

  Kwa kuongeza ladha unaweza kuongezea vitu hiyo hapo chini.

  ½ kijiko kidogo cha chai kungu manga ya unga (nutmeg)

  ½ kijiko kidogo cha chai Mdalasini ya unga (cinnamon)

  1 kijiko kidogo cha chai vanilla ya maji

  Kisha mimina mchanganyiko wako wa keki kwenye chombo utakachotumia kuokea na oka kwa dakika 40 hadi 45 kwa moto ule ulioelekezwa pale juu kama oven yako inamoto mkali zaidi unaweza choma kwa dakika 30 ila hatari ya kuunguza na keki isiive kati kati ni kubwa sana.

  Baada ya dakika 40 chukua toothpick choma keki yako katikati toa angalia kama itakua kavu basi keki yako imeiva kama itakua na maji maji keki yaki bado haijaiva hivyo iache katika oven kwa muda kidogo kisha angalia tena.

  Toa keki yako iache ipoe tayari kwa kuliwa.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Thanx ndg yng! Afadhal umeamua ku2letea maujuz yko! Tehe, tehe, tehe! Ubarikiwe sn!
   
 3. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,041
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  MTM kweli wewe mpishi mzuri, unamkumbuka Rwegasira kwa cake recipe?
   
Loading...