Jinsi ya kuongeza Storage Space kwenye Smartphone yako (Android users)

OleSoft

Member
Jan 21, 2020
24
19
Je, unafahamu kuwa kila unapotumia smartphone yako (Android) kuna file linajitengeneza lenyewe linaitea android?

File hili linaweza kubeba takataka zote na kujikuta limechukua nafasi hata MB 500 au 1GB n.k kulingana na device yako. Lakini pia kuna file la WhatsApp, hapa pia kama unahitaji kuback up, back up kupitia app yenyewe kwenda kwenye google email yako.

Kwenye file folder la WhatsApp kuna file la backup na database ambayo nayo hujitengeneza yenyewe, haya mafile yanaweza kuchukua nafasi.

Cha kufanya:

Ingia kwenye file manager, tap phone storage, kisha chagua android, futa hilo file.

Baada ya hapo, shuka chini kabisa mpaka kwenye folder/file la Whatspp, tap kisha futa database na backup file, na uliache media file/folder.

Hapo hapo, ingia kwenye media, chagua document au voice note, au audio, video au images, tazama ulichokituma kama kina umuhimu kubako au kama hakuna umuhimu futa. Tazama ulizptumiwa, kama zina umuhimu kubaki au kama hakuna basi futa.

Siku hizi kuna improvement, kuna file manager zingine hukupa kabisa taarifa zote na kitu kinachokula nafasi kwenye simu yako, hivyo file manager automatically itapendekeza uyafute hayo mafile.

Lakini hiyo njia niliyotoa ni manually.

Kama una cha kuongezea, maoni au chochote basi weka. Najua lakini sijui zaidi, tupe yako sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ati nini ufute android..... Kama una gemu yale yakuunganisha usifanye huo mchezo... Utaisha
hiyo itakusaidia kama unaona unahitaji nasafi, mfano huna nafasi na hakuna kitu cha muhimu, unaweza fanya hivyo, haina madhara yoyote. Lakini km unakitu cha muhimu unaweza acha, pia siku hizi games zinakuja na file lake yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Can I delete Android data files?

The “cached” data used by your combined Androidapps can easily take up more than a gigabyte of storage space. These caches of data are essentially just junk files, and they can be safely deleted to free up storage space. Tap the Clear Cache button to take out the trash.
 
Toka mwaka 2010 nafanya hivi, wala hamna kipya.

Ila kuna watu hawataamini, tena wakisikia kufuta file la android ndio wanadata

Unforgetable

Tunatofautiana matumizi ya simu sisi wacheza bussid online hatuwez futa Android sababu taarifa za game zinahifadhiwa humo ukifuta ukifungua game itakwambia kuna file una miss utaenda download tena lina 123Mb ....
 
hiyo itakusaidia kama unaona unahitaji nasafi, mfano huna nafasi na hakuna kitu cha muhimu, unaweza fanya hivyo, haina madhara yoyote. Lakini km unakitu cha muhimu unaweza acha, pia siku hizi games zinakuja na file lake yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapana aisee ndani ya folder la android kuna data na obb za apps akifuta hilo apps zote data zake zinafutika ni majanga
 
Can I delete Android data files?

The “cached” data used by your combined Androidapps can easily take up more than a gigabyte of storage space. These caches of data are essentially just junk files, and they can be safely deleted to free up storage space. Tap the Clear Cache button to take out the trash.
Nice - vizuri sana short and clear

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapana aisee ndani ya folder la android kuna data na obb za apps akifuta hilo apps zote data zake zinafutika ni majanga
Hapana sio kweli, ukifuta hilo file Apps hazifutiki, unakuwa salama. Lile file lipo kwaajili ya kukusanya data zote unazofanya kwenye simu yako, mfano cached data, kuna mtu kaelezea vizuri hapa short and clear, pitia utaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana sio kweli, ukifuta hilo file Apps hazifutiki, unakuwa salama. Lile file lipo kwaajili ya kukusanya data zote unazofanya kwenye simu yako, mfano cached data, kuna mtu kaelezea vizuri hapa short and clear, pitia utaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasema app zinafutika bali data za app zinafutika na unapofuta data za app, app zako zinabakia kama urembo tu.

Tusiandikie mate kwanini usianze kufuta hilo folder kwenye simu yako?
 
Back
Top Bottom