ccm mtoto wao
JF-Expert Member
- Dec 19, 2018
- 562
- 483
Nataka nunua simu used online lakini sijui chochote kuhusu manunuzi online wadau naomba mnisaidia.
get well soon tl
get well soon tl
Jiunge na https://www.paypal.com/tz/home halafu ukiwa na ATM card ya VISA nenda kwenye bank yako waombe wakuunge na huduma za kifedha za kufanya manunuzi mitandaoni. Wakati unafanya hiyo michakato jiunge na maduka ya mitandaoni kama https://www.ebay.com/ https://www.aliexpress.com/ https://www.alibaba.com/showroom/online-shopping-free-shipping.html au https://www.amazon.com/. Passwords (nywila ) zako zitunze vizuri sana andika kwenye notebook ukiweza. Hakikisha kuwa una sanduku la barua (P. O. Box) ili uweze kutumiwa mzigo wako. Baada ya kuweza kuunga akaunti na huduma za kifedha mitandaoni utaweza kulipia simu yako. Unachofanya ni kuingia kwenye akaunti yako ya duka la mtandaoni na kuchagua simu ukilinganisha bei (kuna mpya na kuna zilizotumika na sio simu karibia bidhaa zote kasoro vyakula vinavyoharibika au madawa ndiyo hayauzwi kwenye hizo websites). Ukikubaliana na mnunuzi unalipia kisha simu itatumwa na kukufikia ulipo. Kuna maduka ya mtandaoni ya Tanzania pia kama Kupatana, Zoom, Jumia kama ukipenda. Cha muhimu usiwe mvivu.
Nmb naweza pata huduma hii maana ni bank pekee hapa ndanda
get well soon tl
Kuna sera inaitwa MONEY BACK GUARANTEE kwa hiyo duka litakurudishia pesa zako usipopata kitu ulichonunua. Pia kama hujaridhika na kitu kuna option ya kukirudisha kwa muuzaji ndani ya siku 30 utachagua options wakati unanunua aidha ulipie wewe au muuzaji agharamikie kukirudisha. Naomba mpitie kwenye hizo websites.
Hivi mkuu kama nataka nitumiwe mzigo kwa option nyingine kama dhl nafanyeje?Kuna sera inaitwa MONEY BACK GUARANTEE kwa hiyo duka litakurudishia pesa zako usipopata kitu ulichonunua. Pia kama hujaridhika na kitu kuna option ya kukirudisha kwa muuzaji ndani ya siku 30 utachagua options wakati unanunua aidha ulipie wewe au muuzaji agharamikie kukirudisha. Naomba mpitie kwenye hizo websites.
Chagaua bidhaa kisha wasiliana na muuzaji mkubaliane. Hili litawezekana baada ya kuchagua bidhaa.Hivi mkuu kama nataka nitumiwe mzigo kwa option nyingine kama dhl nafanyeje?
Nina acc ebay ila naona kuna option ya P. O. Box tu..
Sent using Jamii Forums mobile app
Ok sawa nitafanya hivyo mkuu..Chagaua bidhaa kisha wasiliana na muuzaji mkubaliane. Hili litawezekana baada ya kuchagua bidhaa.
Mimi nimenunua kwa mpesa mastercard aliexpress ila sioni hata dalili ya kutumiwa mzigo. Ni wiki sasa imepita
Nimenunua mizigo mingi aliexpress na imefika salama
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulilipa kwa njia gani
Si uangalie status ya order yakoMimi nimenunua kwa mpesa mastercard aliexpress ila sioni hata dalili ya kutumiwa mzigo. Ni wiki sasa imepita
To be shippedSi uangalie status ya order yako
Sent from my SM-G920P using Tapatalk