Jinsi ya kumfurahisha mkeo katika Uislam

Jinsi ya kumfurahisha mkeo katika Uislam

Status
Not open for further replies.

Midekoo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
47,774
Reaction score
256,818
1. Mapokezi Mazuri
Baada ya kurudi kutoka kazin, safarini, au popote pale palipowatenganisheni:
* Anza kwa maamkizi mazuri
* Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na tabasamu.
*Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
*Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae.

2. Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha
*Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.
*Shughulika nae unaposema au anaposema yeye
*Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.
* Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano Mpenzi wangu, honey (asali, tamtam), (habibty), swaaliha (mwanamke mwema), n.k

3. Urafiki na maliwazo
* Tumia muda kuzungumza nae
* Mpe habari njema
*Kumbuka kumbukumbu zenu nzuri za kuwa pamoja.

4. Michezo na burudani
*Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha
*Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine.
*Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.
* Jiepushe na mambo ya haram katika kuchagua aina ya burdani.

5. Msaada katika kazi za nyumbani
* Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/ unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa anapokuwa mgonjwa au amechoka.
* La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini/unashukuru jitihada zake katika kazi.

6. Kushauriana
*Hususan katika masuala ya familia
*Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.
* Kuyazingatia maoni yake kwa makini
*Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa maoni yake iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
*Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.

7. Msaada wa kifedha
*Unatakiwa kumpa matumizi kwa mujibu wa uwezo wako wa kifedha. Usiwe bahili na pesa zako (wala usiwe mfujaji).
*Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya kumkirimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa mkono wako (hadiyth).
*Unahimizwa sana kumpa kabla yeye hajakuomba.

8. Kunukia vizuri na kujipamba mwili
* Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za utupuni na kwapani.
* Daima uwe msafi na nadhifu.
*Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)

9. Jimai (Tendo la ndoa)
*Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa,n.k
* Uanze kwa “BismiLlaah” na du'aa zilizo sahihi.
*Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)
*Uanze kwa vitangulizi (vya tendo) ikiwa ni pamoja na maneno ya mahaba
*Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
* Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
* Epukana kufanya tendo wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haraam
* Epuka wakati wa tendo mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.
* Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.

10. Kudhibiti Siri
*Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.

11. Kumuongoza katika kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
*Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho ya usiku kusali “Qiyaam-ul-Layl” (Swalah za ziada za usiku zenye sujuud na ruku’u za muda mrefu).
* Mfundishe kile unachokijua katika Qur-aan na tafsiri zake.
*Mfundishe “Dhikr” (njia za kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za asubuhi na jioni.
* Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya Allaah (Sibhaanahu wa Ta'ala) kama vile kutoa sadaka.
*Mchukue katika safari ya Hijja na 'Umrah wakati unapokuwa na uwezo.

12. Mafunzo ya Kiislam na kumshauri kwa kumrekebisha
Hii ni pamoja na
* Misingi ya Uislam.
*Haki na wajibu wake.
* Kusoma na kuandika.
*Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah (darsa duara za Msikitini na majumbani).
*Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake
*Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.

13. Wivu unaokubalika
*Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili anapotoka nyumbani.
* Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume wasio- Mahram.(wenye uwezo kumuoa)

Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:
1. Kulichambua kila neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.
2. Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
3. Kumzuilia kujibu simu, n.k.

14. Subira na Upole

* Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
* Kumsamehe makosa anayokukosea wewe

Ni namna gani unaweza kumrekebisha makosa yake?

1- Kwanza, mpe ushauri kwa njia ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara
2- Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda kumuonyesha hisia zako). Tanabahi kuwa hii haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia nyumba nyingine, au kutomsemesha
3- Utatuzi wa mwisho ni kumpiga kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie yafuatayo

* Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepukakumpiga kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumpiga mwanamke wala mtumwa

* Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza au kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.
*Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k. au mbele za watu

15. Kusamehe na makaripio yanayofaa

* Mhukumu kwa makosa makubwa tu
* Msamehe makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano kuchelewesha Swalah, n.k
* Kumbuka mazuri yote anayokufanyia kila wakati anapofanya makosa
*Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake katika Uislam bado yamo katika kukua

* Jiepushe na kumgombeza kwa mapishi mabaya kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumlaumu yeyote katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda chakula, hula na iwapo hakukupenda hukiwacha na hatoi maoni yoyote.

* Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi
* Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake
* Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa faragha
* Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako
 
Pamoja na yote hayo bado mnaongoza kwa talaka na umalaya sana.

mnaongoza kutelekeza wake na watoto aisehhh waislam mmelaaniwa kabisa hamtaki kusoma ni kuoa na phd za jinsi gani ya kumpenda na kuoa wanawake 10

yaani kila nikiwasikia natema mate chini
Heri yako we kafiri unaezini kwa kulazimishwa kuwa na mke mmoja.na ndio maana nazidi kuamini dini ya haki ni Islam kwakua haipendi watu wake wazini ndomana tukaambiwa tuanze na Wa wili mpaka wanne na tukishindwa ndo tuoe mmoja,yote nikuiepuka zinaa,kuacha ni matokeo yakutoelewana baina yenu hasa pale atakapoenda tofauti na utakavyo kwa ajiili ya MUNGU,na ndio maana nyie mnajidanganya kwa kutengana chumba au nyumba uku mkiendelea kuzini nje,and ukiwa unaona uzi usio husiana na wewe so lazima uchangie mana sio kila kitu lazima uchangie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakae soma na kuna Liza
Na aheshimiwe

Triple A
 
Somo zuri lakini nina hakika nikifunga tu huu uzi wako na somo zima linayeyuka.
Inabidi nipate binti wa kupractice naye.
 
Pamoja na yote hayo bado mnaongoza kwa talaka na umalaya sana.
mnaongoza kutelekeza wake na watoto aisehhh waislam mmelaaniwa kabisa hamtaki kusoma ni kuoa na phd za jinsi gani ya kumpenda na kuoa wanawake 10 yaani kila nikiwasikia natema mate chini
Kwa kweli kwa kutalakiana tu wanaongoza, sasa sijuwi sababu hawafuati hii list ndefu kama mlima kilimanjaro au ni ruksa kwa wao kuoa na kuacha bila kirahisi rahisi hivyo!
Point zote ni "wishful thinking" kwa maisha ya sasa, na hata atakayeweza kuyafanya hayo haimanishi mwanamke bado ataridhika..ila katika porojo hii list yafaa..
 
Heri yako we kafiri unaezini kwa kulazimishwa kuwa na mke mmoja.na ndio maana nazidi kuamini dini ya haki ni Islam kwakua haipendi watu wake wazini ndomana tukaambiwa tuanze na Wa wili mpaka wanne na tukishindwa ndo tuoe mmoja,yote nikuiepuka zinaa,kuacha ni matokeo yakutoelewana baina yenu hasa pale atakapoenda tofauti na utakavyo kwa ajiili ya MUNGU,na ndio maana nyie mnajidanganya kwa kutengana chumba au nyumba uku mkiendelea kuzini nje,and ukiwa unaona uzi usio husiana na wewe so lazima uchangie mana sio kila kitu lazima uchangie.

Sent using Jamii Forums mobile app

Waislamu walimuuliza bwana Yesu Kristu eti mwanamke huyu aliolewa na wanaume kumi na wote wakafa je siku ya mwisho huyu mwanamke atakuwa wa nani?

Yesu akajibu ukishakufa hakuta kuwa na kuoa wala kuoana ila uzima wa milele kwa waaminio injili yake.

sasa nyie oeni waliokosa bikra na ahera mabikira 72
 
Pamoja na yote hayo bado mnaongoza kwa talaka na umalaya sana.

mnaongoza kutelekeza wake na watoto aisehhh waislam mmelaaniwa kabisa hamtaki kusoma ni kuoa na phd za jinsi gani ya kumpenda na kuoa wanawake 10

yaani kila nikiwasikia natema mate chini

Mh research Yako umeifanyia wapi??
 
Kwa kweli kwa kutalakiana tu wanaongoza, sasa sijuwi sababu hawafuati hii list ndefu kama mlima kilimanjaro au ni ruksa kwa wao kuoa na kuacha bila kirahisi rahisi hivyo!
Point zote ni "wishful thinking" kwa maisha ya sasa, na hata atakayeweza kuyafanya hayo haimanishi mwanamke bado ataridhika..ila katika porojo hii list yafaa..
Kwa Mwenye hofu ya Mungu ni jambo rahisi kwake.
 
Heri yako we kafiri unaezini kwa kulazimishwa kuwa na mke mmoja.na ndio maana nazidi kuamini dini ya haki ni Islam kwakua haipendi watu wake wazini ndomana tukaambiwa tuanze na Wa wili mpaka wanne na tukishindwa ndo tuoe mmoja,yote nikuiepuka zinaa,kuacha ni matokeo yakutoelewana baina yenu hasa pale atakapoenda tofauti na utakavyo kwa ajiili ya MUNGU,na ndio maana nyie mnajidanganya kwa kutengana chumba au nyumba uku mkiendelea kuzini nje,and ukiwa unaona uzi usio husiana na wewe so lazima uchangie mana sio kila kitu lazima uchangie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said braza......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke anafurahishwa na pesa tuu, vitu vingine ni mbwembwe tuu za wazinzi wa mjini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom