JINSI YA KUKABILIANA NA HASIRA

JINSI YA KUKABILIANA NA HASIRA

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,992
Reaction score
5,969
Hasira ni hisia ya kawaida ya kibinadamu, lakini namna tunavyoikabili ndiyo huamua kama tunajiumiza,tunajiponya ama kuwaumiza wengine.
Hapa kuna mwongozo wa hatua kwa hatua wa kukusaidia kuikabili hisia ya hasira kwa umakini:
1. Tambua Hasira Yako
Usijifanye hujaudhika unapokuwa umeudhiwa.
Usiipuze hisia uliyonayo,tambua ama kubali kwamba una hasira/umechukia
Kitendo cha kujitambua kuwa umekasirika ama kuchukia ni hatua ya kwanza ya kuweza kuikabili hali ya hasira.
2. Tafuta Chanzo cha Ndani
Mara nyingi hasira siyo juu ya jambo la sasa tu ni mkusanyiko wa maumivu ya zamani.
Jiulize: "Je, kuna jambo la zamani ambalo halijapona ndani yangu?"
Kwanini kitendo hiki/jambo hili limenijeruhi hivi ama kunifanya kuwa hivi?
Mfano;
Kwa wanawake wengi wanaolea watoto peke yao mara nyingi kutokana na ule ugumu wa malezi hujikuta wakitunza maumivu kwa muda mrefu kiasi hupata hasira sana inapotokea mtoto amekosea ama limetokea jambo lisilofaa kwa mtoto wake.
Inakua tukio la sasa+maumivu ya muda mrefu= hasira na ukali uliopitiliza.
Unapogundua chanzo cha hasira yako ni rahisi kupokea tiba ama kuweza kukabiliana na hali hiyo isiwe na madhara kwako ama kwa wengine.
3. Jfunze Mbinu za kupata Utulivu
Miongoni mwa mbinu za kutengeneza utulivu ndani ya akili ya mwanadamu ni pamoja na kuvuta pumzi kwa mtindo wa kuvuta pumzi kutoka nnje kisha kuipeleka ndani kupitia pua, kisha kuitoa pumzi hiyo kupitia mdomo.
Unaweza pia kutembea kidogo,kukimbia,kusikiliza mziki,kuimba,kusali,au kukaaa kimya dakika chache kabla ya kuchukua hatua yoyote.
4. Andika Hisia Zako
Elezea kwa maandishi unavyohisi badala ya kufoka au kupiga kelele.
Kupitia kuandika mtu huweza kujiponya maumivu aliyonayo.
Kwa kuandika husaidia kupunguza mzigo wa hisia na kuleta uwazi.
5. Zungumza Kwa Hekima
Ongea ukiwa mtulivu itakusaidia kuikabili hasira kwa ujasiri.
Ukiwa na hasira unapaswa kuongea kwa hekima.
kama:
“Nimeumia sana kwa sababu umenisaliti.
Nilikuamini mnoo kwanini umenitenda hivi?.”
badala ya “Wewe malaya umenisaliti,kwanini huridhiki mbwa wewe,nakupa kila kitu huridhiki.”
Kwenye mazungumzo lengo lako halipaswi kua kushinda mabishano, bali kueleweka kile unachopitia ama unachotaka ueleweke.
6. Jifunze Kusamehe
Msamaha si kwa ajili ya yule aliyekukosea tu, bali ni zawadi kwa moyo wako.
Kukaa na hasira ni kama kunywa sumu na kutarajia mtu mwingine afe.
Msamehe aliyekukasirisha ili upate amani moyoni mwako na hasira ipate kuondoka katika moyo na akili yako.
7.Zingatia Faida katika hisia zako.
Mwanadamu hatakiwi kuendelea kutawaliwa na hisia zisizo na faida kwake.
Jiulize: "Ninapata faida gani kwa kuendelea kuwa na hasira?"
Tambua ni nini kinakuchochea, kisha ujifunze kukiepuka au kukimudu.
Hasira ni hasara,hakuna faida katika hisia za hasira.
8. Tafuta Msaada wa Kitaalamu
Ukiona hasira inakuzuia kuishi kwa amani au inakuathiri wewe na wengine: Usione aibu kuzungumza na mshauri wa afya ya akili au mshauri wa maisha.
Kliniki ya Furaha ipo kwa ajili ya wewe anayehitaji mwongozo wa kina wa kiroho, kihisia na kisaikolojia.
Zingatia;
Hasira ni kiashiria cha hisia hasi.
Ni sauti inayosema: “Kuna jambo ndani yangu linahitaji kutazamwa kwa umakini.”
Jisikilize kwa upendo, usijifungie ndani.
JiKubali, jitulize, jieleze, na jifunze kuachilia.
 
Back
Top Bottom