Jinsi ya kujenga leo na kesho yako

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,563
10,549
Kama kijana kuna wakati unapaswa kuutumia vizuri maana muda haumsubiri mtu, na muda ni rasilimali tosha.

Niende kwenye hoja saidizi.

1- Jitahidi kuwa Mchaguzi (selective)
  • Uchaguzi wa Vyakula + Vinywaji
  • Uchaguzi wa Mavazi
  • Uchaguzi wa Marafiki
  • Uchaguzi wa Mtu utakayekuwa nae ktk Mahusiano.
*Uchaguzi wa Sehemu ya kuishi (Mkoa, wilaya etc)
*Uchaguzi wa Dini (Imani)
N.k

Yaan jitahidi uwe mtu wa kuchagua sana sio unajizolea zolea tu kila kilichopo mezani, kuna watu huwa hawazingatii hayo wao hawafikirii wala hawafanyi "reasoning" kujihoji je hichi nilichochagua ni sahihi? Kwanini? Ili iweje.

Ubaya wa kutofanya machaguo mazuri ni kuishia pabaya, mfano kwa ambaye si mchaguzi mzuri wa Marafiki atabebelea marafiki Sumu (Toxic friends) vivohivyo kwa ambae si mchaguzi mzuri wa vyakula atapata magonjwa ya kisukari, unene kupitiliza shinikizo la damu etc.

2- Wekeza katika Kujifunza mambo mapya:
Napendekeza kujifunza yale yaliyo magumu, pia yale yenye tija.
Mfano kama ni mfanyakazi jitahidi ujue vitu vitakavyo kupa msaada ktk utekelezaji wa Majukumu yako hapo kazini mfano matumizi mazuri ya programu ujuzi wa miundo sanifu n.k

Kwa aliyejiajiri anaweza kujifunza zaidi Biashara nyingine zaidi ya ile anayoifanya hivyo atapata wigo mpana wa kuboresha biashara yake na kuongeza mapato.

Kwa asiye na ajira: ni fursa pia kujifunza mambo mengi kadri ya siku zinavyokwenda hii itakusaidia kujitenga na kundi ambalo mtaringana core qualifications wewe utakuwa upo extra miles kudemonstrate una nini cha ziada.

3- Ishi kwa TAHADHARI
Hii mbinu nilipewa na Mzee mmoja wa kijerumani hivi karibuni ktk taasisi nayofanyia kazi. Aliniambia kuwa katika Maisha unatakiw uwe na TAHADHARI kubwa kwa kila jambo unalotaka kulifanya ili kumpunguzia MWENYEZI MUNGU lawama. Sio kila kitu unajifanyia kiholela matokeo yakija mabaya unamsingizia Mungu alipanga yatokee. Hapana.

Mfano: Umefanya Chaguzi vizuri ukampata Mchumba/Mrembo ukaanzisha mahusiano nae ila bila kuwa na tahadhari basi ukamtia/ukanasa ujauzito ambao hamkupanga iwe hivyo. Hapo tyr ushafeli.

Tahadhari imekwenda mbali zaidi hata katika Maswala ya Malezi kwa watoto ikumbukwe hata future ya mtoto inaandaliwa akiwa bado yupo tumboni.

(Hapa nitakuja na Uzi wake nitaelezea jinsi ninavyomlea Mwanangu mwenye Mwaka 1 Sasa).

4- Mahusiano mazuri katika Jamii pamoja na MIPAKA:
Ili ujenge leo na kesho yako yenye afya, jitahidi kuwa na mahusiano mazuri sana na jamii. Kuna watu wanaona ni ufahari kujiita (Antisocial) hii si nzuri hata kidogo, kuna shuhuda nyingi sana zinawatokea watu wa aina hii na matokeo yake huwa ni mabaya ktk jamii maana wanakosa mtu wa kuwasaidia kwa hali na mali.

Nimejifunza kuwa na uhusiano mzuri na Majirani + watu kazini (hata wale wafanya usafi wana role yao ktk Maisha yako).

Mipaka inajengwa na wewe mwenyewe ukiwa mtu wa umbea umbea lazima watakufata mpk nyumbani kukuletea habari. Cha msingi ni kuishi na watu kwa kutumia busara na upendo zaidi ukizingatia yale yanayokuhusu tu.

Nihitimishe kwa kusema Leo na Kesho yako unaipanga wewe mwenyewe, tuepuke kutoa lawama zisizo na tija tuamke na kila mmoja acheze nafasi yake.

Weekend Njema.
 
Kuhusu uchaguzi wa vyakula na mahali (mkoa au wilaya) pa kuishi inategemea na Hali uliyonayo kipindi hicho kiuchumi, kijamii nk...vingine vyote nakubaliana na wewe.
 
Kuhusu uchaguzi wa vyakula na mahali (mkoa au wilaya) pa kuishi inategemea na Hali uliyonayo kipindi hicho kiuchumi, kijamii nk...vingine vyote nakubaliana na wewe.
Ni kweli Kila mtu ana External and Internal forces.

Mfano kuna mtu akiwa Mbeya hapati madeal mengi kutokana na kazi anayofanya same applied kuna mtu yupo DSM but anafit sana Mkoa wa Mbeya kutokama na Harakati zake. Hapo ni swala la kujitambua tu.

Kuhusu Vyakula. (Watu wenye kipato cha chini ndio wanaongoza kula vyakula vya Afya) hawana Selection/ Uchaguzi wa Expensive food's ambavyo vingi ni Junk foods.

So.. Swala la Kipato ktk upande wa chakula ina rely na utashi na hulka ya mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom