Maneno yako tu yanakutambulisha wewe ni mtu wa namna gani.Pumbafu kabisa wewe ,unadhani sisi biashara hatufanyi???? Wewe ni mmoja ya majizi kwa mfumo huuu
Duhhh!!!...Kwenye hundi ya malipo unaongeza/kupunguza 0 au 00 mfano hundi ya malipo ya shs 1,000,000/= unaongeza 0 inakuwa 10,000,000/= milioni tisa, yes 9,000,000/= 'zako na wenzako'!
...Unarekodi makontena 10 wakati idadi halisi yaliyoingia ni 100, hapo umepunguza sifuri moja, cha juu au 'idadi' ya makontena (90) tisini yaliyosalia 'mnakula na wenzako'.
...anapewa Sheraton 5yrs tax holiday, miaka mitano mingine anapewa Royal Palm 'tunu hiyo', miaka kumi na tano baadae Movenpick nao wanafaidi 'tunu hiyo hiyo', ...bure tu? hapana, kuna commission fulani inakwenda kwa mfuko,
Usanii wa kubadili majina/makampuni ya 'wawekezaji' ni katika 'kula na kipofu bila kumshika mkono!'. i.e Richmonds to Dowans et al...
...kwa wale wataoshangaa hii ndio bongo bwana, mwendo mdundo!
Nimecheka hapo unaposema "anaporudi anaitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya mkutano huo ambao hakuhudhuria.Nasikia kuna katabia ka viongozi wetu kwenda kwenye mikutano ambayo hailingani na vyeo vyao, na pia baadhi ya mabalozi wetu huko nje,
mkutano ni wa maofisa wa chini, lakini waziri mzima analilia kwenda tu, anachukua posho, halafu akifika kule hawezi kuingia kwenye mkutano kwa sababu ni maofisa wa ngazi za chini, mkuu anabaki huko majuu maana alishachukua posho tayari ya mkutano wa mwezi mzima, anapiga mitaa huko majuu na shopping baadaye anarudi bongo na kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya mkutano huo, ambao hakuhudhuria,
nasikia pia kuna baadhi ya mabalozi wetu huko nje nao wana hiyo tabia ya kulazimisha safari hata zisizowahusu, ili mradi tu wapate posho na kusafiri, mwisho kulitia taifa letu hasara na in fact huu ni wizi wa mchana kweupe!
Usitake kupotosha watu mkuu, hata kwenye sheria ya kodi tu neno "mradi" halijatumika.Hiyo ya kubadili jina au umiliki wa mradi ni uwongo. Huwezi kupata fedha kwa kubadili jina la mradi au umiliki wa mradi. Maneno hayo yanazungumzwa na mbumbumbu wa biashara.
Msamaha wa kodi hutolewa kwa mradi na siyo kwenye jina la mradi. Kama mradi ni ule ule hata ungebadili majina mara 1000 haitabadili nafuu ya kodi au muda wa msamaha wa kodi kwa mradi husika. Lakini kwa sababu watanzania wengi hawajui kabisa biashara wakiona jina au mmiliki wa mradi amebadilika, utasikia, 'tayari jamaa wamekwishakula', ujinga mtupu! Nchi ya wapiga majungu. Nchi ambayo mtu ambaye hawezi hata kueleza madini maana yake nini lakini anaamini anaweza kuwaelezea watu uchumi wa madini, au mtu asiyejua hata maana ya X- Ray lakini anaamini ana uwezo wa kuhutubia watu namna ambayo mgonjwa aliyevunjika mfupa anatakiwa kutibiwa!
Kama brela unasajiri makampuni ya uchuuzi sawa! We endelea na makampani yako yakupiga super profit acha wachuuzi tuendeleee kuchuuza!Maneno yako tu yanakutambulisha wewe ni mtu wa namna gani.
Hapa tunaongelea biashara na siyo uchuuzi ambao kuna uwezekano mkubwa, ndiyo unaoufanya.
Fanya utafiti, utaujua ukweli. Misamaha ya kodi hutolewa wakati uwekezaji wa miradi mipya. Mradi unapouzwa na kununuliwa na mwekezaji mpya au mwekezaji wa mwanzo anapotaka kubadilisha jina, haihesabiki kama ni uwekezaji mpya. Mradi unaendelea na benefits zile zile za mwanzo. Kama mwekezaji wa mwanzo alikuwa hajarudisha mtaji wake, akaja mwekezaji mpya kwenye mradi ule ule, akaongeza uwekezaji, kipindi cha msamaha wa kodi kitaongezeka kutokana na mtaji uliongezeka. Na hiyo haina uhusiano na jina la kampuni.Usitake kupotosha watu mkuu, hata kwenye sheria ya kodi tu neno "mradi" halijatumika.
BRELA wanasajili makampuni yote ya uwekezaji na uchuuzi pia. Unaweza kuwa kampuni ya ku-supply stationery. Stationery unachukua India au China unapeleka kwenye ofisi mbalimbali. Huo ni uchuuzi. Na kuna wakati uchuuzi unaweza kukupa super profit kumshinda mwekezaji.Kama brela unasajiri makampuni ya uchuuzi sawa! We endelea na makampani yako yakupiga super profit acha wachuuzi tuendeleee kuchuuza!