Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Nimekaa najiuliza ni jinsi gani watumishi wa serikali kuanzia wa ngazi za chini hadi za juu kabisa wanaweza kuibia serikali na serikali isitambue au ishindwe kuchukua hatua? Inawezekana vipi watu wakawa wanachota fedha za umma kama kuchota maji kwa kata na wakazimeza hata bila ya kuzitafuna? Bila ya shaka kuna mbinu mbalimbali ambazo zinatumika na wajanja hao kula fedha za umma "bila kunawa". Hivi ni mbinu gani zinatumika kuuibia serikali bila ya hata kukamatwa?
NB: Mada hii haina lengo la kufundisha wizi au mbinu za kuuibia serikali bali inataka kuonesha ni mbinu gani zinatumika kuubia serikali. Kama unataka kujua jinsi ya kula fedha za umma, tafadhali jiunge na utumishi wa serikali kwani wapo watu ambao watakuwa tayari kukupa somo "live" as you go along.