Jinsi ya kuflash simu aina zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuflash simu aina zote

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by UncleUber, Jul 20, 2011.

 1. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  kama mwezi umepita nahangaika na ile samsung s4 clone ya mdogo wangu ambayo inajirestart kila muda mpaka betri iishe chaji https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/676587-wataalamu-wa-simu-za-android-clone.html , nimehangaika nayo, mafundi wa mwanza chali, juzi nimeenda kariakoo fundi akaniambia iyo lete 30k nikampa ikamshinda nikaenda kwa wawili watatu chali, sasa nikaamua kutake matter in my hands, jana nimefanikiwa kuiflash na kuiroot kabisa, nikaona si vibaya kushare ugunduzi wangu huu....


  Jinsi ya kuflash simu zenye MediaTek chipset

  naamini clone zote zinatumia mtk pia nahisi hata za tecno nazo zina hii chipset

  1. anza kwa kuandaa mazingira ya kuflash simu yako ambayo labda iko bricked, au ina tatizo lolote kama hii yangu iliyokuwa inajirestart muda wote

  vitu unavyohitaji ni
  a.) drivers za simu (kama chip yako ni MT65xx family download hapa) na
  b.) Smart Phone flash tool download hapa
  c.) Mtk Droid Tools download hapa
  d.) ROM / firmware ya simu yako (hakikisha ni rom sahihi kwa model ya simu yako) Rom karibia zote zinapatikana hapa

  2. Tuanze sasa
  a.) chomeka simu yako na iache ifanye installation ya driver zote, kama zingua install driver hapo juu(kama simu yako ni mt65xx)
  b.)kwa sababu simu za clone hazijulikani model maana zina imitate original, basi tutatumia MTK droid tool kujua model ya simu yetu. fungua application na uiache italeta details zote kuhusu simu

  [​IMG]

  c.) tayari taarifa za simu tumezipata , kinachofuata hapo ni kudownload firmware specific kwa ajili ya simu yetu. ROM/firmware zipo hapa (ili kudownload inabidi ujisajili kwanza) pia unaweza kugoogle utapata tu. hakikisha una extract na ndani kuwe na faili MT(model ya simu yako)_Android_scatter.txt (hakikisha kuna neno scatter kwenye jina la hili file)

  d.) hapo sasa kila kitu tunacho tunaweza kuanza kuflash simu yetu...
  i. ichomoe simu, kisha fungua SP flash flash tools, sehemu ya scatter-loading file weka lile .txt file nililokwambia limo kwenye folder uliloextract kule juu

  pia nenda options > usb mode iwe ticked pia hapohapo kwenye options angalia DA download all > Speed > force high speed inakuwa checked

  [​IMG]

  ii. click download kisha iache (usichomeke simu kwanza mpaka imalize) ikimaliza chomeka simu bila betri ukisikia mlio wa simu imekuwa connected kwenye pc haraka rudisha betri bonyeza "firmware -> upgrade" kisha tulia itaanza kuflash simu

  ii. kama kila kitu kimeenda sawa utaona progress kwa rangi ya njano kama kuna makosa itatokea rangi nyekundu na maelezo

  [​IMG]

  ikikamilisha successiful, itaonesha kiduara cha kijani

  [​IMG]


  hapo sasa unaweza chomoa simu yako na kuiwasha na utaona inaanza kama mpya vile....  ukipenda unaweza kuiroot, kubadili IMEI, kuondoa application za kichina zote kwa kutumia MTK Droid tools


  TAHADHARI: SITAHUSIKA KAMA UTAHARIBU SIMU YAKO, TRY AT YOUR OWN RISK
   
 2. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  pole sana kwa kutokujibiwa...

  ukisema universal maana yake zote zinawezekana. pia inategemea na box kwan zinatofautiana quality na ubora na Cable..pia bei ni tofautii...

  cha muhimu ni box latest na software latest na kujiunga kwenye forums za simu ili uwe uptodate!!

  kama unataka fungua ofisi ya kisasa bila ubabaishaji ni vizuri uka ni PM nikuconnect na watu wanao husika na mambo hayo.

  cheers!!
   
 3. k

  kajembe JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Biashara ya kufungua simu ni nzuri sana kwakuwa kuna wateja wengi lakini kwakuwa unatakuanza unatkiwa na mabox mengi ya kutosha lakini changamoto kubwa ni jinsi ya kujua box gani uwe nazo.

  watengeneza mabox hawana box ambalo kweli ni unique ambalo linafungua simu zote na kimsing universal box uliyosema inatumia software za bure ambazo nyingi ni ama za majaribio au hazina update na hazijitoshelezi kabisa.hata hivyo unahitaji sana kusoma kwenye forums za simu ili ujue ni mabox gani yanatakiwa na jinsi ya kucheza na hizo software,kumbuka pia ktk kazi hiyo utapambana sana vimeo vya kuzimisha simu unapofnya kazi ya ku unlock hivyo inabidi u take time kujifunza sana kwa waliozoea na kuji some wewe mwenyewe.

  Mafundi wengi wa TZ hapa hawasomi kufuatilia jinsi ya kucheza na soft hasa kwa simu kama hizi za kisasa za Blackberry,iphone na zingine nyingi na hata hivyo zingine zinahitaji uelewa mzuri wa computer na kimombo,ushauri wa bure ukiwa mfuatiliaji wa internet utajua mengi kuliko walio sokoni. forums ni kama gsmcity.de,gsmhosting na zingine search kwenye forums masaada zaidi nitumie mail kama unataka,nimefanya muda mrefu naijua vizuri sana hii kazi,ingwaje siku hizi si deak nayo tena kama zamani it is just to help you if you want
   
 4. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkuu universal sio kwa kila simu kwani simu za wajomba wachina zina box lake linalojitegemea na baadhi ya simu hazihitaji box kama vile iphones
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu kama kweli umeamua kuingia katika mambo ya simu basi unaweza kuanza na mabox mawili, 1.infinity box.hili box linauwezo mkubwa wa ku flash aina nyingi za ki china. 2.j.a.f box au ufsx+hwk.haya nayo yatakuwezesha nayo ku flash baadhi ya simu kama nokia,samsung,lg, nk.. Pia ufuate ushauri wa bw sharobaro juu ya kujisomea forum za simu kama vile gsmforum,gsmindia dhaka mobile nk. Naimani kwamba wakati utakapokuwa unajifunza kuyatumia hayo mabox ndivyo utakavyo kuwa unazidi kuvumbua ma ujanja zaidi.
   
 6. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kwa hapa kwetu Bongo ni vyuo gani vinavyotoa kozi hizo za ufundi wa simu kwa undani?
   
 7. k

  kajembe JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Binafsi sijawahi kusikia chuo wanachofundisha kozi hiyo,isipokuwa watu wengi hujifunza kwa watu wenye ofisi zao na uzoefu katka kazi hiyo, mimi binafsi niemwahi kufundisha watu ktk ofisi yangu siku za nyuma na nikagundua vitu muhimu viwili,kwanza unaweza kumfundisha mtu kwa kumpa lectures na akwa anachuka hata notes lakini mwisho wa siku akashindwa kufanya kazi, pili ukamchukua mtu hata shule hajasoma kabisa lakini ukakaa nae ofissini baada ya miezi michache utakuta anajua kuflash na kutengeneza vizuri sana! sasa hapo kama ni mtu mkomaaji kwenye forums na ameisha jifunza kazi kwa vitendo basi atakuwa mtalaam safi kabisa!
   
 8. k

  kajembe JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ni kweli mabox ulyosema unaweza kuanzia lakini angalizo kwa Jaf! sidhni siku hizi kama kuna updte tena! otherwise ni box zuri pia!
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  upo sahihi mkubwa wangu basi kwa kuwa huyo bw mkubwa anahitaji ku flash basi tukubaliane kwamba aanze na hilo infinity na ufsx lenye hwk original.
   
 10. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  tizo1 naona kakimbia maana tangu ka post hata kuchangia mjadala alio uanzisha hamna.
   
 11. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  .

  HAYA SASA. Unataka kuua simu za watu, wewe huna hata kaujuzi kadogo ka haya masuala lakini unangangania, au unataka kuwa kama kinyozi kujifunzia vichwani kwa watu. Ukisikia kuflash simu unachukulia kama toilet tu. nimempenda huyo aliye ulizia kuhusu vyuo au mahali pa kujifunzia lakini hakuana alie mjibu
   
 12. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mchango wako?
   
 13. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  sijakimbia jaman nipo.je hizo box nilizoambiwa na wataalamu zinau9a bei gani kwa pesa ya hapa tz?pia hizo box zinaweza kuflash ZTE phone?NAHITAJ MSAADA ZAID.NILIKUWA KIMYA sababu nilikuwa na matatizo kidogo.
   
 14. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  asante sharo baro.nipe bei ya box ili nitathmin itakuwaje kufanikisha jambo langu.nita ku pm
   
 15. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  acha dharau kwani si uungwana.kumbuka wana tecknolojia hawana maneno ya kike kike.pia ni waungwana sana.
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  ok bro.box la infinity linaweza ku flash ZTEna HUAWEI Na zingine nyingi tu.bei ya hili box nadhan kati ya laki 4 mpk 6 (sina uhakika) mimi nipo kahama ila nafahamu huko dar wanapo uza hayo ma box ni kule kwa naheem.
   
 17. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asante ndugu!Nahee anapatikana maeneo gani kule DSM?mimi nipo TABORA Kwa sasa.
   
 18. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kama sijakose nadhani ni makutano ya uhuru na swahili. Leo nitaku pm nikupe contact za NAHEEM kisha utajribu kutathmin.hapo utapata kila aina ya mabox ila anza na hayo ambayo yamependekezwa na wadau.
   
 19. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nina box ya ufsx +hwk yake ila kebo hazijatimia walinikwapulia ila zipo nyingi tu dar zinuzwa tano elfu tu naiuza ni original.
   
 20. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  nipe bei kaka tumalize biashara!ikiwezeka ni pm .
   
Loading...